Kumbe wa kimataifa nao wanaamini ushirikina!!

Rajab_Omar

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2016
Posts
16,482
Reaction score
27,182
Baada Ya Wakimataifa Kujichimbia Kisiwani PEMBA- ZANZIBAR katika Eneo La Chake Chake Kujitayarisha Na Pambano lao Dhidi Ya Wekundu Wa Mzimbazi, Hatimae Baadhi Ya Viongozi Wao Waonekana Katika Kijiji Kimoja Kilichopo Mkoa Wa Kusini Pemba, Wailaya Ya Mkoani, Jimbo la Kiwani! Kijiji Hicho Kinaitwa Mwambe Chenye Wakazi Ambao 99% ni Wenye Asili Ya Kaskazini Unguja Wakijuilikana Maarufu Kama ni Watumbatu! Kijiji Hicho Ni Maarufu Kwa Waganga Wanaohusika Kuwafanyia Ushirikina Viongozi Mbali mbali Wa Kisiasa.

Wakimataifa Nao Mara Zote Wanazokuja Zanzibar Ni Lazima Viongozi Wao Wafike Katika Kijiji Hicho Hasa Nyakati Za Usiku ili Wasifahamike Kiurahisi Kwa Lengo La Kutumia Njia Za Kishirikina Kuroga Dhidi Ya Mchezo Wao na Simba! Na Ndiyo Maana Wakimataifa Huwaoni Kueka Kambi Unguja! Bali Ni Lazima Wake Kambi Pemba ili Kuwa Karibu Na Kijiji Hicho Chenye Waganga Wao.

Source: Ni mimi Mwenye Niliyekaribu na Maeneo Yao Ya Mazoezi Chake Chake ninaewaangalia Movements Zao Chafu Zote Usiku na Mchana.
 
Reactions: DBA
Ulijua wa matopeni tu ndio wenye imani za uchawi japo wewe hatukuamini sana ila najua unawasiwasi
 
Mkuu ulizani huko pemba wamefuata viwanja vizuri vya mazoezi, au kuwaepusha wachezaji na kusawishiwa kuchua fedha za Simba, viko viwanja vingi tu huku bara, pia wanajua kama kuna mchezaji kanunulia, kanunuliwa mapema hii mechi ilijulikana mapema kwenye kalenda ya TFF. Yanga Pemba wamefuata UCHAWI/ULOZI/UWANGA/ KIGAGURA, A.K.A USHIRIKINA. na sio vinginevyo.
 
Mshaanza kutafuta visingizio vya kufungwa eeh?tulieni kesho dawa iwaingie vizuri.
 
Nawe ni mchawi... Huo ni utalii wa ndani mshamba wewe, watu wasitembee, wanatafuta uchawi... Ila nimefurahi ulivyokiri na kuwatumbua wa KIMATAIFA...
 
pinga kwa hoja, nini kilichowapeleka yanga pemba.
Atapingaje hoja ambayo wewe mwenyewe hujaithibitisha kwa ushahidi? Ama kweli Rage hakukosea kuwaita wanachama wa Simba "mambumbumbu" [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Nawe ni mchawi... Huo ni utalii wa ndani mshamba wewe, watu wasitembee, wanatafuta uchawi... Ila nimefurahi ulivyokiri na kuwatumbuawa KIMATAIFA...
Aliekiri kuwatumbua wa kimataifa ni nani huyo tena, kawatumbua kwa sababu zipi. Kumbe Yanga wameenda kutembea Pemba, mbona unavyoandika tu, unaonyesha kutaka kujionyesha kuwa wewe wa mjini, illa mimi nakuona hata kama mimi ni mshamba, basi nitakua naishi mkuranga wewe uko Kibiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…