Kumbe Wabongo iko gonjwa!

Kumbe Wabongo iko gonjwa!

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Wabongo jamani wana bongo, kumbe wengi spana mkononi! Nimeamini kabisa kwamba usianzishe ugomvi ukapigana unaweza kuua.

Karibu Wabongo wote ni wagonjwa, ukitaka uthibitisho mwulize Babu wa Loliondo. Msururu ule wa wazee, vijana, wanawake kwa wanaume, kwenda Samunge ni uthibitisho tosha kabisa, kwamba tulikuwa tunajikausha tu kumbe iko gonjwa.

Vigogo na masikini, sooote maselule tupu. Kikombe cha Babu kimetutanabahishia kuwa kumbe ni ujanja tu, hatuna kitu, nani atabisha kuwa hajakanyaga miwaya, lakini akifika kwa Babu anasingizia kisukari? Wapo wengi wa aina hiyo, tunashukuru Babu hapimi.

Na kama Babu angekuwa na hadubini za kupimia virusi, naamini Wawa Lali asingepiga marufuku haya mapaparazzi kumuhoji na kumpiga picha Babu, kwa sababu hata hivyo nani angejipanga msururu ule kupimwa ngoma?

Thubutu!
 
Kazi kwelikweli
 
We unafikiri mchezo kuanzia Jk, pinda mpaka watoto.
 
solution ni ku check afya zetu mara kwa mara hata kama hatuumwi na siyo kwenda kwa babu loliondo
 
Babu anaweza kutoa statistics nzuri sana ya idadi ya wagonjwa Tanzania,
 
Back
Top Bottom