Maofisa wa Ubalozi wa U.A.E Wanalalamikia polisi kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya Kimataifa vya habari na Wananchi wa Tanzania kupitia Waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi kuwa raia wao wanahusika na tukio la Uhalifu lililotokea Arusha.
Kimsingi wametoa muda kwa Serikali ya Tanzania kuwaachia raia hao kwani nchi hiyo inaamini kuwa hawahusiki kwa namna yeyote na tukio la Arusha na kwamba kukamatwa kwao ni kinyume cha taratibu za sheria za Kimataifa.
Taarifa zinadai kuwa watuhumiwa wawili kati ya hao ni "ASKARI POLISI"wa nchi hiyo ya Falme za Kiarabu na Mwenzao mmoja ni Ofisa wa Ushuru wa Forodha wakati raia wa Saud anayeishi U.A.E ni mtaalamu wa maswala ya Moto.
Taarifa zinaonyesha kuwa vijana hao ambao wote ni watumishi wa Serikali waliwasili Jumatano iliyopita kwa likizo fupi ya kutembelea nchi za Afrika Mashariki na walitarajiwa kurejea U.A.E alhamisi wiki hii.
Taarifa zaidi zinabainisha kuwa baada ya kuwasili Tanzania na kutembelea jijini Dar es salaam kwa siku mbili vijana hao waliwasili Arusha Jumamosi wakitumia gari dogo la rafiki yao ambae ni Mtanzania mwenye asili ya kiarabu na kufikia hoteli ya Aquiline iliyopo jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi Jijini Arusha.
Usiku huo jumamosi taarifa zinaonyesha kuwa vijana hao walikwenda kustarehe katika Vilabu mbalimbali vya starehe wakihama kutoka Kilabu vitatu tofauti.ilipotimia saa 9 alfajiri walirejea ktk Hoteli waliyoifikia.
Asubuhi ya Jumapili ambayo kanisa ililipuliwa kwa Bomu vijana hao waluanza Maandalizi ya kwenda Nairobi nchini Kenya kumalizia ratiba yao ya Starehe ilioanzia Tanzania lakini kabla ya kuondoka ndipo walipo kamatwa.
TAARIFA ZAIDI: Soma gazeti la Raia mwema.
Soma After Arusha Bombing Is NOT Time for TZ to Adopt CCTV Culture?