hapa yaaani sijaelewa hata kidogo unamaanisha nini
Labda kukusaidia kwa kiswahili ...
Kabila la Mosuo lipo huko china, na wao mama ndio kiningozi wa familia. Urithi ni kwa watoto wa kike tofauti na huku kwetu.
Mtoto wa kike akishafikia kubalehe anapewa chumba chake. Na baada ya hapo ana ruksa ya kumkaribisha mwanamme yoyote anayetaka yeye chumbani kwake usiku. Na anaruhusiwa hata kubadilisha anavyoataka.
Mwanamme ukija chumbani kwake usiku ana haki ya kukukyubali au kukukataa. Ukikukataa inabidi ugeuze kwa aibu. Akikukubali basi ndio kama vile, ila uhakikishe unaondoka kabla ndugu zake hawajaamka asubuhi, na urudi nyumbani kwako. Maana yake ni kwamba uhusiano wenu huo hauwahusu wengine.
Mwanamke akipata mimba hivyo na mtoto kuzaliwa, mtoto anatunzwa na familia ya mwamke. Na baba yake anaweza akawa hata hajulikani. Familia ya mwanamke na wajomba wa mtoto ndio wanajukumu la kulea mtoto. Baba hatakiwi hata kuleta uso wake, hakuna anayemjua anyway. Baba huyo yeye jukumu lake ni kusaidia kule watoto wa dada zake katika familia ya mama yake.
Kwa jinsi hiyo basi kwenye kabila la Mosuo hakuna ndoa.
Kwa kabila la Mosuo hakuana kumilikiana. Jamii zetu zina mfumo wa ajabu sana. Yaani mtu akishakuwa gf wangu basi ndio anataka amiliki mimi, muda wangu, etc. Mtu akishakuwa bf wako basi ndio unakuwa kama mali yake. Mwanamke akiwa na mtoto basi mtoto ndio kama mali yake.
Kwa watu wa Mosuo mtoto ni wa jamii nzima na jukumu la kulea ni kwa familia ya mama yake. Ila si ajabu ukakuta watu wanabadilishana watoto, kwa mfano kama familia moja ina watoto wa kiume wengi na ina badilishana na familia yenye watoto wa kike wengi. Na mtoto akiletwa hivyo anatunzwa kama mtoto mwingine wa familia ile.
Kwa watu wa Mosuo hakuna matatizo kama haya ambayo ni uzao wa mfumo wetu mbovu:
1. Hakuna yatima,
2. Kamwe hakuna ugomvu wa mme na mke, au ugomvi wowote unaohusiana na mapenzi
3. Hakuna kupeana talaka
4. Hakuna kuoneana wivu
Na matatizo mengi mno mengine yamefutika .... Na kwa namna hiyo Musuo society inaweza kuwa the most stable societies in the world.
Umeelewa hata kidogo sasa mamii? Au niendelee kukutafunia wa umeze tu?