Mleta mada unakosea Sana kumfananisha Trump na Magufuli.
Trump was not a career politician yule ni mfanyabishara mkubwa, hafahamu siasa za Washington DC, hakuwa na uzoefu wowote ule wa uongozi kwa nafasi yeyote ile serikalini, hivyo matendo yake yalitokana tu na hisia za yale iyokuwa akiyaona sio sawa kwa wanasiasa wa marekani wanavyoyafanya.
Hata hivyo baadhi ya watu wanasema kuwa kafanya reforms nyingi Sana ambazo ni nzuri kwa manufaa ya uchumi wa Marekani, na kwa kudhihirisha hilo kapata kura zaidi ya Milioni 70, alikuwa na wafuasi twitter zaidi ya milioni 80. Huwezi ita mtu kama huyo mkurupukaji kama Trump ni mkurupukaji how come spare kura zaidi ya 70 million unataka kusema watu wote hao hawajitambui?? Unakosea.
Unapokuja kwa Magufuli yeye ni mzoefu wa siasa, ana uzoefu wa miaka 20 kwa nafasi ya Uwaziri, anafahamu vyema namna serikali inavyofanya kazi.
Reforms zake zinatokana na observation na pia experience yake kwa namna serikali inavyofanya kazi, huyu kwa mtu mvivu na mpiga dili hata weza kuwa rafiki yake kwakua refoms zake zimelenga kuondoa utamaduni wa muda mrefu uliokuwepo wa kufuja mali za uma.
Baada ya kusema hayo sioni ni kwa namna gani mleta mada umefikia na hitimisho lako hili.
Kufanana kwa mtu, huwa siyo lazima wafanane kwa yote...
Trump vs Magufuli wanafanana kihulda na aina yao ya uongozi kwa zaidi ya 90%...
Wote;
å Wako high tempered
å Ni waongo
å Hujifanya wanajua kumbe hawajui
å Hawapimi madhara ya kauli zao
å Wanapenda madaraka na wanaweza kung'ang'ania kwa kadiri wawezavyo
å 2020 USA na Tanzania zilikuwa na chaguzi. Wote Trump & Magufuli walikuwa ni maRais wagombea wanao omba kuwa re - elected for their 2nd terms.
å Wote wameshindwa vibaya ktk chaguzi hizo
å Magufuli kwa sababu ya taasisi dhaifu za nchi ya Tanzania, akafanikiwa kufanya manipulation na kujishindisha. Here he is, "The president". Mwenzie Trump akajaribu kutumia njia kama za Magufuli ili abaki madarakani, kashindwa. Kwanini?
å Ni kwa sbb taifa la Marekani limejengwa ktk msingi wa taasisi imara, halimtegemei mtu kusimama bila kujali mtu huyo ni nani hata kama ni Rais na Amiri Jeshi mkuu..!
å Hitimisho la ujinga wake (Trump) mwenye akili na mtazamo ulio sawa na wa Magufuli, ilikuwa ni jaribio la ku - incite insurrection dhidi ya mamlaka halali ya kisiasa na serikali ya Marekani. Sasa anapata adhabu yake..
å Trump anaamini kuwa Marekani ni " yeye" na yeye ni "Marekani" kama ambavyo Magufuli anaamini yeye ndiye "serikali ya Tanzania" na serikali ya Tanzania ni "Magufuli". Lakini ukweli ni huu, " Serikali ya Marekani" ni watu wa Marekani na kamwe siyo Rais Trump kama tu ambavyo ilivyo hapa kuwa "serikali ya Tanzania" ni Watanzania na kamwe siyo "Rais Magufuli"..