Kama ilivyo kawaida, makabila mengi yalipewa majina ya makabila yao na watu wengine.Wenyeji wa Mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, yaani Wazaramo walipewa jina hilo na ndugu zao Waluguru!
Mambo yalianza vipi?
"Eneo ambao leo linajumuisha Mkoa wa Pwani lilikuwa likikaliwa na watu wa kabila la Wandengereko kuanzia Rufiji, Marui mpaka maeneo ya Maneromango," anasema Ali Kaskasi, mmoja wa wakazi wa asili wa eneo hili.
Anaendelea: "Katika enzi za kupigania maeneo ya kuishi na kutawala, Wandengereko walivamiwa na Wakamba kutoka Kenya na walipozidiwa nguvu, wakaomba msaada kutoka kwa Waluguru ambao walituma vijana kuwasaidia.
Simulizi hiyo inasema Wakamba walishindwa na kutimuliwa katika ardhi ya Wandengereko kwa msaada wa Waluguru."Hata hivyo, vijana wengi wa Kiluguru waliamua kubaki katika ardhi ya Wandengereko baada ya kupata wachumba na kuyapenda mazingira yake. Hawakurudi Morogoro," anasema Kaskasi na kuendelea kwamba wale waliorejea Morogoro waliulizwa walikowaacha wenzao.
Nao wakajibu kwamba wenzao walikuwa ‘wamezarama' yaani walikuwa wamelowea au ‘kuzamia'. Huo ukawa ndiyo mwanzo wa kuibuka kwa kabila la Wazaramo, yaani watu (hususani Waluguru) waliolowea pwani. Ni simulizi tamu na ya kweli ambayo inahusisha makabila makubwa matatu ya ukanda wa Pwani ambayo ni ndugu – Wandengereko, Waluguru na Wazaramo.