Kumbe wazaramo wamelowea

Kumbe wazaramo wamelowea

Quezon

Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
42
Reaction score
18
Kama ilivyo kawaida, makabila mengi yalipewa majina ya makabila yao na watu wengine.Wenyeji wa Mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, yaani Wazaramo walipewa jina hilo na ndugu zao Waluguru!

Mambo yalianza vipi?

"Eneo ambao leo linajumuisha Mkoa wa Pwani lilikuwa likikaliwa na watu wa kabila la Wandengereko kuanzia Rufiji, Marui mpaka maeneo ya Maneromango," anasema Ali Kaskasi, mmoja wa wakazi wa asili wa eneo hili.

Anaendelea: "Katika enzi za kupigania maeneo ya kuishi na kutawala, Wandengereko walivamiwa na Wakamba kutoka Kenya na walipozidiwa nguvu, wakaomba msaada kutoka kwa Waluguru ambao walituma vijana kuwasaidia.

Simulizi hiyo inasema Wakamba walishindwa na kutimuliwa katika ardhi ya Wandengereko kwa msaada wa Waluguru."Hata hivyo, vijana wengi wa Kiluguru waliamua kubaki katika ardhi ya Wandengereko baada ya kupata wachumba na kuyapenda mazingira yake. Hawakurudi Morogoro," anasema Kaskasi na kuendelea kwamba wale waliorejea Morogoro waliulizwa walikowaacha wenzao.

Nao wakajibu kwamba wenzao walikuwa ‘wamezarama' yaani walikuwa wamelowea au ‘kuzamia'. Huo ukawa ndiyo mwanzo wa kuibuka kwa kabila la Wazaramo, yaani watu (hususani Waluguru) waliolowea pwani. Ni simulizi tamu na ya kweli ambayo inahusisha makabila makubwa matatu ya ukanda wa Pwani ambayo ni ndugu – Wandengereko, Waluguru na Wazaramo.
 
Mkuu kumwe na Wewe unafuatilia Kipindi cha Antonio Nugaz wa Cloud TV Kambi Popote
Maana ndio uchambuzi huu ulifanyika wa kina sana.

Hongereni Sana Clouds Media na Pongezi Zaidi Antonio Nugaz kwa Kipindi cha Kambi Popote.
Tumejifunza mengi sana na ikiwemo post hii ambapo nahisi kabisa ni Zao lako.Maana uliwahoji wenye Kujua Historia ya Makabila na wao wenyewe wakaelezea Chimbuko la Makabila hayo Katika kipindi chako cha Kambi Popote Morogoro.
Nasubiria sasa Mambo ya Tanga wiki hii
 
Hii ina ukweli nlishawahi sikia pia chifu kingalu mwana banzi wa waluguru alikuwa na mahusiano makubwa na wazaramo
 
Kwa ninavyojua mimi mzimu wa kingalu chimbuko lake ni wanyamwezi.

Huko zama za kale wanyamwezi walikuwa wakihamisha mizimu yao kuelekea ukanda wa pwani na targeted area ilikuwa ufikie bagamoyo lakini baadhi ya mizimu iligoma kufika pwani baada ya joto kuzidi kadri walivyokuwa wakielekea pwani hivyo mzimu ukatimkia milima ya unguu na ulugulu.

Na inasemekana kipindi kile Ditopile Mzuzuri alipompiga risasi dereva mjukuu wa mzee Mbonde(Bagamoyo nyumba kubwa) alienda kuomba tambiko kwenye mzimu wa kingwalu baada ya kuandamwa na roho wa mauti kwa muda mrefu.

Alienda na jogoo wake kabla hata ibaada haijaanza yule jogoo alioza ghafla mzimu ukamfukuza ikifuatiwa na radi kubwa sana!!!

Hatimae usiku wa siku hiyohiyo Ditopile akaaga dunia!!!

Inasemekana mzee Mbonde ni mtu hatari sana kule Bagamoyo. Sasa baada ya mjukuu wake kufa alijiapiza hakuna msamaha Dito lazima afe licha ya akina Kikwete na yule rafiki kipenzi aliyeondolewa ikulu kumsihi mzee amchunie Dito... Sheikh Mbonde aligoma katakata!!!

Mahujaj wanamjua vizuri huyu mzee huwa anaenda Macca bila usafiri wowote na anawahi kufika kabla ya waliotumia usafiri wa ndege za wazungu...😕😕:banghead::what:
 
Na inasemekana kipindi kile Ditopile Mzuzuri alipompiga risasi dereva mjukuu wa mzee Mbonde(Bagamoyo nyumba kubwa) alienda kuomba tambiko kwenye mzimu wa kingwalu baada ya kuandamwa na roho wa mauti kwa muda mrefu. Alienda na jogoo wake kabla hata ibaada haijaanza yule jogoo alioza ghafla mzimu ukamfukuza ikifuatiwa na radi kubwa sana!!!
Hatimae usiku wa siku hiyohiyo Ditopile akaaga dunia!!!

Inasemekana mzee Mbonde ni mtu hatari sana kule Bagamoyo. Sasa baada ya mjukuu wake kufa alijiapiza hakuna msamaha Dito lazima afe licha ya akina Kikwete na yule rafiki kipenzi aliyeondolewa ikulu kumsihi mzee amchunie Dito... Sheikh Mbonde aligoma katakata!!!
Mahujaj wanamjua vizuri huyu mzee huwa anaenda Macca bila usafiri wowote na anawahi kufika kabla ya waliotumia usafiri wa ndege za wazungu...😕😕:banghead::what:

Cc Sikonge
 
Last edited by a moderator:
Quezon

Eti INNOVATOR, habari hii si ingefaa iende kwenye kale ka-subforum ka historia? I strongly feel so.
 
Last edited by a moderator:
Kwa ninavyojua mimi mzimu wa kingalu chimbuko lake ni wanyamwezi.

Huko zama za kale wanyamwezi walikuwa wakihamisha mizimu yao kuelekea ukanda wa pwani na targeted area ilikuwa ufikie bagamoyo lakini baadhi ya mizimu iligoma kufika pwani baada ya joto kuzidi kadri walivyokuwa wakielekea pwani hivyo mzimu ukatimkia milima ya unguu na ulugulu.

Na inasemekana kipindi kile Ditopile Mzuzuri alipompiga risasi dereva mjukuu wa mzee Mbonde(Bagamoyo nyumba kubwa) alienda kuomba tambiko kwenye mzimu wa kingwalu baada ya kuandamwa na roho wa mauti kwa muda mrefu.

Alienda na jogoo wake kabla hata ibaada haijaanza yule jogoo alioza ghafla mzimu ukamfukuza ikifuatiwa na radi kubwa sana!!!

Hatimae usiku wa siku hiyohiyo Ditopile akaaga dunia!!!

Inasemekana mzee Mbonde ni mtu hatari sana kule Bagamoyo. Sasa baada ya mjukuu wake kufa alijiapiza hakuna msamaha Dito lazima afe licha ya akina Kikwete na yule rafiki kipenzi aliyeondolewa ikulu kumsihi mzee amchunie Dito... Sheikh Mbonde aligoma katakata!!!

Mahujaj wanamjua vizuri huyu mzee huwa anaenda Macca bila usafiri wowote na anawahi kufika kabla ya waliotumia usafiri wa ndege za wazungu...😕😕:banghead::what:

Kamba😂😂😂
 
Nilikuwa sijaelewa kwanini tabia za watu wa pwani zinafanania na Waluguru na Wandereko ila baada ya kusoma hiii mada nimeanza kuelewa nini chanzo
 
Kwa ninavyojua mimi mzimu wa kingalu chimbuko lake ni wanyamwezi.

Huko zama za kale wanyamwezi walikuwa wakihamisha mizimu yao kuelekea ukanda wa pwani na targeted area ilikuwa ufikie bagamoyo lakini baadhi ya mizimu iligoma kufika pwani baada ya joto kuzidi kadri walivyokuwa wakielekea pwani hivyo mzimu ukatimkia milima ya unguu na ulugulu.

Na inasemekana kipindi kile Ditopile Mzuzuri alipompiga risasi dereva mjukuu wa mzee Mbonde(Bagamoyo nyumba kubwa) alienda kuomba tambiko kwenye mzimu wa kingwalu baada ya kuandamwa na roho wa mauti kwa muda mrefu.

Alienda na jogoo wake kabla hata ibaada haijaanza yule jogoo alioza ghafla mzimu ukamfukuza ikifuatiwa na radi kubwa sana!!!

Hatimae usiku wa siku hiyohiyo Ditopile akaaga dunia!!!

Inasemekana mzee Mbonde ni mtu hatari sana kule Bagamoyo. Sasa baada ya mjukuu wake kufa alijiapiza hakuna msamaha Dito lazima afe licha ya akina Kikwete na yule rafiki kipenzi aliyeondolewa ikulu kumsihi mzee amchunie Dito... Sheikh Mbonde aligoma katakata!!!

Mahujaj wanamjua vizuri huyu mzee huwa anaenda Macca bila usafiri wowote na anawahi kufika kabla ya waliotumia usafiri wa ndege za wazungu...😕😕:banghead::what:
duuuh! simulizi tamu sana hii.
 
Back
Top Bottom