Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Ilikuwa Februari, 6, 1958, Timu ya Manchester United ilikuwa ikitokea Belgrade, kucheza na timu ya Red Star. Manchester ilikuwa chini ya Kocha Matt Busby; wachezaji wake walijulikana kama "Busby Babes".
Sare ya 3-3 waliyoipata kwenye mchezo huo iliifanya Manchester United kutinga nusu fainali ya Kombe la Uropa.
Ndege yao ilicheleweshwa saa moja kwa sababu mmoja wa wachezaji alisahau pasipoti yake ikabidi wasimame katika Uwanja wa ndege wa Munich-Riem ili kuongeza mafuta.
Wakati huo Munich ilikuwa na hali mbaya ya hewa, theluji ilienea katika maeneo mengi.
Rubani James Thain alifanya majaribio matatu ya kurusha ndege mawili yakashindikana sababu ya shida ya injini.
Jaribio la tatu, liliifanya ndege iweze kuondoka lakini haikuwa na Kasi ya kutosha ya kuiwezesha kuacha Ardhi na mwisho iligonga uzio wa uwanja na kuanguka kwenye kibanda kilichokuwa karibu na maeneo hayo.
Watu 22 kati ya 43 waliokuwa kwenye ndege walifariki papo hapo. Wachezaji 7 wa Manchester ni miongoni mwa waliofariki kwenye ajali huku wa 8 Duncan Edwards akifariki wiki mbili baadae na kufanya jumla ya vifo 23.
Kocha Busby alisumbuliwa na majeraha kwa wiki kadhaa. Nahodha wa ndege alinusurika ajali hiyo na baadae akatuhumiwa kwa kosa la uzembe wa kudharau theruji iliyokuwa imeganda kwenye mbawa za ndege hiyo.
Miaka 10 baadae Kocha Busby aliiongoza Manchester United kuchukua kombe la kwanza la mashindano ya Ulaya .Kikosi kilihusisha Wachezaji wawili walionusurika ajali.
Mwaka 2004 Mwanamuziki Morrissey alitunga wimbo wa kuelezea tukio hilo uliokwenda kwa jina la " Munich Air Disaster 1958"