Kumbukizi: Arthur afungiwa Mechi sita baada ya kumtemea mate Mchezaji mwenzake

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Mlinzi wa West Ham United, Arthur Masuaku amefungiwa Mechi sita na Chama cha soka nchini Uingereza FA baada ya kumtemea mate mchezaji mwenzake.



Mchezaji huyo ambae ni raia wa Ufaransa alimtemea mate Nick Powell wa Wigan katika mchezo wa FA waliopoteza lakini hata hivyo beki huyo mwenye miaka 24 tayari ameomba radhi kwenye mitandao ya kijamii akisema sio tabia yake.

Masuaku hatocheza mpaka West Ham itakapo ikaribisha Manchester United katika uwanja wa London Machi 18.

Meneja wa West Ham United, David Moyes anawakosa idadi kubwa ya wachezaji kutokana na kuwa majeruhi ambapo amesema Masaku alifanya ujinga. “Masuaku anastahili adhabu yoyote itakayo tolewa nasi pia tutapata tunachostahili.” alisema Moyes.

Masuaku atakosa mechi dhidi ya Crystal Palace, Brighton, Watford, Liverpool, Swansea na Burnley.
 
Na Augustino Mabalwe


Chama cha soka nchini Uingereza FA kimemfungia mechi 6 beki wa Manchester United Jonny Evans kwa kosa la kutemeana mate na mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse.

Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 38 ya mchezo katika mechi hiyo iliyopigwa katikati ya juma hili kwenye uwanja wa St.James Park huku Manchester United ikiibuka na ushindi wa 1-0 katika dakika za mwisho.

Awali Evans alikataa kufanya tukio hilo na kushangazwa na vyombo vya habari kwa kuzidi kumzonga lakini kwa upande wa Cisse alikiri kumtemea mate beki huyo na hivyo kupokea adhabu ya kufungiwa michezo 7 kutoka kwa chama cha soka nchini humo.

Adhabu hiyo itafanya beki huyo wa Manchester United kukosa mchezo wa robo fainali dhidi ya Arsenal utakaopigwa keshokutwa jumatatu kwenye uwanja wa Old Trafford na mechi nyingine atakazokosa ni dhidi ya Tottenham machi 15,Liverpool machi 22,Aston Villa April 4, Manchester City April 12 na ile ya April 18 dhidi Chelsea.

Aidha taarifa kutoka FA inasema kuwa wachezaji hao wamepewa adhabu hiyo kwa kuzingatia sheria namba E1(a) na Cisse amefungiwa mechi moja zaidi kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 aliyoipata mwanzoni mwa msimu huu.
 
Moutaz Abdullah wa ash Sha'ab ya Imarati afungiwa mechi 6 kwa utovu wa nidhamu



Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Umoja wa Falme za Kiarabu imetoa hukumu ya kumfungia Moutaz Abdullah mlinda mlango wa timu ya ash Sha'ab mechi sita na faini ya dirham 12,000 (ambazo ni sawa na dola 2,700 ) baada ya kumpata na hatia ya kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumtemea mate mchezaji wa timu ya Baniyas mwezi uliopita.

Moutaz Abdullah alimtemea mate mshambuliaji Carlos Munoz raia wa Chile wa klabu ya Baniyas baada ya kumalizika pambano kati ya timu ya al Sha'ab na Baniyas, pambano ambalo lilimalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana bao 1-1.

Wakati huohuo, Salim Bahyan al A'miri Mkuu wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Imarati amesema kuwa, kamati hiyo pia imemuondoa hatiani Carlos Munoz ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kufanya vitendo vya kibaguzi.
 
Chama cha Soka cha England (FA), kimemfungia kucheza mechi saba straika wa Newcastle United, Papiss Cisse kutokana na kukiri kumtemea mate beki wa Manchester United, Jonny Evans.
Evans ameendelea kukomaa kwamba hakumtemea mate Msenegali huyo ingawa picha zinaonyesha naye alifanya hivyo. Suala lake litasikilizwa leo.
 
Watuwanatafuta justification ya alichokifanya YONDAN? Ya kwake hayakuwa mate ya kawaida??? nadhani lile ni shambulizi la kujiandaa kabisa maana ni KOHOZI lile zito kabisa la rangi ya njano , hata kwasi alivyojaribu kulifuta bado lilingangania kwenye shavu. Yangekuwa mate yangedondoka yenyewe
 
sad
 
Mjinga yondaniii...!
nilishangaa sana mwamuzi tukio ameliona na anaoneshwa KOHOZI kabisa halafu anamgusa tu Kwasi arudi kwenye mchezo, mbaya zaidi akajaribu kurudia kipindi cha PILI yule Yondani alikua wa RED kabisa
 
Nakumbuka Abdi Banda alifungiwa mechi mbili baada ya refa kutoliona kosa la kumpiga ngumi George Kavila lkn lilipoonekana uningani alifungiwa
 

BEKI wa Simba aliyesimamishwa na kamati ya masaa 72 kucheza ligi kuu kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar George Kavilla Katika mchezo uliofanyika Kaitaba Bukoba na Simba kufungwa Kwa mabao mawili Kwa moja, Sasa yuko huru kuitumikia klabu yake ya Simba baada ya adhabu yake kuwa imeisha.

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la Soka Tanzania (Tff) ilimpa Banda adhabu ya kukosa mechi mbili za ligi kuu kwa kosa la kumpiga ngumi Kavilla.

Kwa maana hiyo Banda yuko huru kuendelea kuitumikia klabu yake Kwani adhabu ya mechi mbili za mwanza Tayari alishazikosa simba ilicheza na Mbao Fc na kushinda Kwa mabao matatu Kwa mbili (3-2) baadae wakacheza dhidi ya toto African na kutoa suluhu (0-0) Michezo yote hiyo Simba wamecheza bila beki Wao Abdi Banda.
 
Luis Suarez (Uruguay) afungiwa mechi tisa za kombe la dunia
Kabla ya kumng'ata mchezaji wa Chelsea, aliwahi kumtemea mate Patrice Evra, kwa hiyo wamng'oe na ulimi? Kwa kuwa mate yanazalishwa na glands unaonaje...

Hii HAIKUBALIKI kabisa. Lazima apewe adhabu kali na faini juu. Yale ni zaidi ya mate, ni makohozi maana yalimnata kabisa Kwasi shavuni. Yaani Yondani alikuwa ameyaandaa mdomoni na kuyashikilia kwa muda wote mdomoni akisubiri wa kumtemea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…