Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Mlinzi wa West Ham United, Arthur Masuaku amefungiwa Mechi sita na Chama cha soka nchini Uingereza FA baada ya kumtemea mate mchezaji mwenzake.
Mchezaji huyo ambae ni raia wa Ufaransa alimtemea mate Nick Powell wa Wigan katika mchezo wa FA waliopoteza lakini hata hivyo beki huyo mwenye miaka 24 tayari ameomba radhi kwenye mitandao ya kijamii akisema sio tabia yake.
Masuaku hatocheza mpaka West Ham itakapo ikaribisha Manchester United katika uwanja wa London Machi 18.
Meneja wa West Ham United, David Moyes anawakosa idadi kubwa ya wachezaji kutokana na kuwa majeruhi ambapo amesema Masaku alifanya ujinga. “Masuaku anastahili adhabu yoyote itakayo tolewa nasi pia tutapata tunachostahili.” alisema Moyes.
Masuaku atakosa mechi dhidi ya Crystal Palace, Brighton, Watford, Liverpool, Swansea na Burnley.