The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Mchungaji na Askofu wa makanisa ya GCTC - Ufufuo na Uzima duniani Brother Josephat Gwajima bado yuko chimbo, lakini hekima na mafundisho yake yako wazi na yanasema na ku - reflect kinachoendelea ktk maisha yetu wanadamu ktk nyanja za kiroho, kisiasa, kijamii, kiuchumi nk...
Katika video hii anasema, Mungu anapotaka kumwinua mtu mwenye haki kuiendea hatima (destiny) yake, kabla hajafanya hivyo huruhusu mfululizo wa matukio mabaya ya kufungua midomo ya watu wasiojua njia za Mungu kubeza, kutukana, kudhihaki nk kabla hajakuweka mahali unapostahili...
Hali hiyo "isiyopendeza" na "inayoumiza" mwili na roho, kibiblia ndiyo huitwa "majaribu". Lengo kuu la jaribu ni kupima resilience ya mtu huyo namna anavyoweza kukabiliana na matukio hayo pasipo kumtukana au kumkana Mungu Yehova....
Akiona kuwa umehimili kila tukio na bado uliendelea kumwamini na kutembea naye; Hukutafuta njia zingine kutafuta nafuu ya changamoto; mfano kwenda kwa wachawi, wasihiri, waganga - wachawi, wasoma nyota, wapiga ramli na watoa kafara za binadamu, hapo Mungu hutokea na kukupa stahili yako...
Chunguza na watazame hawa mapito waliyopitia kabla hawajatukuzwa (glorified) na Mungu: Yusufu, Musa, Eliya, Ayubu, Yesu Kristo mwenyewe, Nelson Mandela na wengi wengi...
♦️♦️Mtazame na msikilize♦️♦️