(Kumbukizi)Humphrey Polepole - Rais lazima ifike siku ashtakiwe kwa uhaini, kinga kwa viongozi haikubaliki

(Kumbukizi)Humphrey Polepole - Rais lazima ifike siku ashtakiwe kwa uhaini, kinga kwa viongozi haikubaliki

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
TOKA Maktaba
05 Agosti 2014


NONDO KALI ZA HUMPHREY POLEPOLE AKIZUNGUMZIA HITAJI LA KATIBA MPYA

HUMPHREY POLEPOLE - RAIS LAZIMA IFIKE SIKU ASHTAKIWE KWA UHAINI, KINGA KWA VIONGOZI HAIKUBALIKI​


Polepole kuhusu katiba mpya kinga kwa viongozi

🅻🅸🆅🅴 HakiTv: Remembering Polepole breaking down the New Constitution Draft

View: https://m.youtube.com/watch?v=oRT_KlHC2Lo

Humphrey Polepole alishiriki kama mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (Tume ya jaji Joseph Sinde Warioba) na amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa misingi ya Katiba mpya inapaswa kuondoa mfumo wa kinga ya kisheria inayowakinga viongozi wa umma dhidi ya uwajibikaji na mashtaka, ili kuzuia viongozi kutumia madaraka yao vibaya au kusababishia taifa hasara bila kuchukuliwa hatua.

Msimamo na hoja kuu za Humphrey Polepole na wadau wa Katiba Mpya kuhusu kinga ya viongozi zinajumuisha:

Kuondolewa kwa Kinga: Katiba inayopendekezwa au mpya inapaswa kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi aliye juu ya sheria, na kwamba kinga ya kutoshitakiwa kwa viongozi wa umma inapaswa kuondolewa au kubadilishwa ili kuruhusu uwajibikaji wa moja kwa moja.

Maslahi Binafsi : Polepole amewahi kueleza kuwa moja ya vikwazo vikubwa katika kupata Katiba mpya yenye misingi thabiti na muundo unaotakiwa na wananchi ni uwepo wa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wanaotaka kulinda nafasi zao na kinga zao za kisheria.

Utawala wa Sheria na Maadili: Msimamo wake wa awali ulisisitiza maadili ya viongozi, uwazi, na kusimamia rasilimali za umma badala ya kuruhusu mifumo inayowalinda watawala kufanya maamuzi yenye hasara kwa nchi bila kuwajibishwa.

Uhalali wa bunge Maalum la Katiba Mpya

Hatua nne muhimu :
1. Wananchi kutoa maoni
2.
3.
4.
1790351332118.png

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Makame Mshimba @ year 2014


TAZAMA MCHANGO WA MJUMBE MMOJA MMOJA NDANI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA PART 3/4 15 APRIL 2014

View: https://m.youtube.com/watch?v=6CaCvoAJWNI


1790351889949.png

Samwel Sitta mwenyekiti

1790351967816.png

Wajumbe wakiapishwa Bunge Maalum la Katiba 2014
 

06 Agosti 2014​

Bunge Maalum la Katiba limeanza kutimua vumbi Dodoma!​


1_0_817651.JPG









Hotuba ya Mwenyekiti wa Bunge Samuel Sitta


Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta katika ufunguzi wa awamu ya pili ya Bunge hilo, Dodoma tarehe 5 Agosti 2014.

Karibuni tena Dodoma Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la kutunga Katiba ya nchi yetu. Sote tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu wetu kwa kuendelea kutupa uhai na afya hadi leo kutuwezesha kuwepo ndani ya ukumbi huu. Tupo humu ili tuitekeleze kazi waliyotukabidhi Watanzania wenzetu milioni arobaini na sita (46) ya kuwapatia Katiba mpya. Dhamana hii ni nzito na haistahili kufanyiwa ajizi.

Tunaendelea na shughuli zetu za Bunge Maalum kwa kuzingatia Kanuni ya 30 (1) inayosema "Akidi kwa kila kikao cha Bunge Maalum isipokuwa wakati wa kupitisha uamuzi wa Bunge Maalum itakuwa ni nusu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum". Nimetaarifiwa na Katibu kwamba wajumbe waliokuja Dodoma kuhudhuria ni zaidi ya robo tatu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum. Nawashukuruni nyote kwa kuja hapa Dodoma ili kutimiza wajibu wenu.

Kwa niaba yenu, nawashukuru Watanzania wenzetu wote ambao kwa mamilioni wamedhihirisha utashi mwema wa kisiasa kwa kuunga mkono hatua ya Bunge Maalum kuendelea na kazi zake hadi tuipate Katiba inayopendekezwa ambayo wataipigia kura ya maoni. Kipekee na kwa niaba yenu, nawashukuru kwa dhati viongozi wetu wa dini wa madhehebu yote wanaloliombea Taifa hili mafanikio Bunge Maalum, wakitanguliza utaifa pamoja na amani ya nchi na umoja ndani ya nchi na siyo ubinafsi na maslahi ya makundi.

Kwa leo sikupenda sana kuzungumzia hoja mbali mbali zinazotawala magumzo ya mchakato wa Katiba mpya hapa nchini, magumzo yanayoendeshwa na makundi maalum kwa jazba na hata matusi. Hata hivyo nalazimika kutoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu upotoshaji mkubwa unaoendeshwa na baadhi ya watu kuhusu Bunge Maalum. Nikiwa Mwenyekiti wenu ninao wajibu wa kuwafafanulia wananchi kuhusu uhalali wa shughuli za Bunge Maalum linaloendelea na utaratibu wa shughuli zetu.

Ni Rasimu ya Tume au la

Wapo wanaodai kuwa eti hapa Bungeni hatujadili Rasimu ya Tume. Tuhuma hii haina ukweli hata kidogo. Msingi wa majadiliano yote tangu tumeanza ni Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Katiba. Utaratibu ni kwamba pale ambapo wajumbe wanaona panafaa kurekebishwa wanafanya hivyo. Maana ya rasimu ni andiko ambalo halijajitosheleza bila kupata ithibati ya taasisi ya juu zaidi.

Anayekabidhiwa rasimu anayo haki na mamlaka ya kuirekebisha. Vinginevyo kujadili rasimu hakuna sababu. Itakuwa ni jambo la ajabu na lisilo na mantiki yoyote kuwa taasisi iliyopewa mamlaka ya kujadili Rasimu ikishaijadili iiache ibaki kama ilivyokuwa wakati ilipowasilishwa!

Je suala ni muundo wa Muungano tu?
Maudhui ya Rasimu yanajumuisha baadhi ya masuala muhimu yafuatayo:
  • Kuimarisha Muungano wetu kwa kuleta uwiano bora zaidi wa mamlaka ya Zanzibar na Tanzania Bara ndani ya Muungano
  • Kuimarisha haki za binadamu ili kuwawezesha raia wa kawaida kufaidi uhuru wa demokrasia bila ubabe na dhuluma
  • Kuzuia wachache kufuja rasilimali za taifa bila kujali maslahi ya wengi na ya vizazi vijavyo.

  • Kujenga uwiano sahihi na wenye haki baina ya wanawake na wanaume katika nafasi za uongozi.
  • Kubainisha hatua zenye kuleta matumaini mapya ya maendeleo kwa makundi maalum ya vijana wakulima wadogo, wafugaji, wafanyakazi wa ngazi za kawaida, walemavu, wafanya biashara wadogo na wajasiriamali wengine.

- Kuweka msingi imara wa kutungwa kwa sheria kakamavu za kuzuia ukandamizaji wa raia, unyonyaji, wizi wa mali ya umma, rushwa, hujuma dhidi ya uchumi na kuzuia mapato haramu na fedha chafu.

  • Kutambua haki za ardhi kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali wengine ili kupunguza migongano na migogoro.
  • Kuweka Misingi ya utawala bora inayozingatia uadilifu, sifa stahiki na ufanisi.
  • Kuwezesha kutungwa kwa sheria bora zaidi zitakazosimamia chaguzi zilizo za haki na huru zaidi pamoja na kuwepo Tume za Uchaguzi zilizoboreshwa.

Zaidi ya hivyo, yapo mapungufu katika Rasimu iliyopo kwa kuachwa masuala ya kuwezesha Serikali za mitaa; kutoa maelekezo kuhusu masuala ya matumizi ya ardhi na rasilimali nyingine za Taifa. Nini kinatuzuia kuiboresha Rasimu kwa kuyaongeza mambo haya ndani ya Katiba kwa faida ya Taifa?

Yote haya ni masuala muhimu ambayo yamo ndani ya rasimu na wakati wake wa kuyaweka sawa ndiyo huu. Pamoja na umuhimu wake suala la muundo wa Muungano si suala la kutulazimisha tuyaahirishe mazuri yote yaliyomo katika Rasimu tuliyopewa.

Uhalali wa Shughuli za Bunge Maalum

Pamoja na uhalali wa kisheria wa Bunge hili Maalum kuendelea kufanya kazi zake, linao pia uhalali wa kisiasa kutokana na sifa za uwakilishi wetu na pia maudhui yaliyomo ndani ya Rasimu. Kutofautiana maoni hakuwapi hadhi tofauti baadhi ya wajumbe kujiona wao wana uhalali zaidi mbele ya wananchi kuliko wenzao. Ndiyo maana utaratibu umewekwa wa kupiga kura na wa maridhiano. Utamaduni mpya unaoanza kujengwa na baadhi ya viongozi wa jamii wa kususia mijadala halali na kwenda nje kuelezea hoja za upande mmoja hauna nafasi katika Tanzania jamii isiyotaka fujo na utengano.
Wajumbe wa Bunge Maalum wanaoendelea na kazi mjini Dodoma ni wateule wa Rais kwa niaba ya wananchi kwa kazi ya kutunga Katiba. Kazi hii haiwezi kusitishwa kwa sababu tu wajumbe wachache wameisusia. Tutazingatia matakwa ya sheria katika kufikia hatma ya mchakato wa Katiba.

Mabadiliko ya Kanuni
Kamanilivyoeleza hapo mwanzo, Rasimu ina jumla ya sura kumi na saba (17) zenye mambo mengi yenye maslahi kwa Watanzania wote. Kwa muda tuliopewa wa siku sitini (60) isingewezekana kuikamilisha kazi tuliyopewa ndani ya muda. Ikumbukwe kwamba kwa Kanuni zilivyo, kila sura mbili zinahitaji siku tisa kuzifanyia kazi. Kwa njia hiyo, ingetuchukua siku takriban mia moja thelathini (130) ili kuikamilisha kazi hii!

Pendekezo la msingi hapa ni kwamba Kamati zetu kumi na mbili (12) zizingatie na kuzijadili sura kumi na tano (15) za Rasimu na pia zikamilishe uandishi wa sura mbili zilizojadiliwa awali na ikibidi ziongeze sura ambazo zitadhihirika kuwa ni muhimu.

Naamini mtiririko huu utatuwezesha kuwa na mpangilio bora zaidi wa sura na ibara katika Katiba mpya. Tusingependa na wala isingefaa kuomba tena muda wa ziada wa kazi ya Katiba ndio maana tunafanya mabadiliko ya Kanuni. Kamati ya Uongozi iliyoketi Dar es Salaam tarehe 28 Julai 2014 imependekeza yafanywe mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum kuwezesha kazi ikamilike ndani ya muda tuliopewa. Kwa hiyo nitawaomba tuyatafakari mapendekezo ya mabadiliko ya Kanuni na hatimaye kuyapitisha ili ratiba ya kazi zetu iende sawa. Nitawaomba muikubali ratiba iliyogawanywa leo na pia mkubali kuzibadilisha Kanuni kwa lengo nililolieleza hapa.

HITIMISHO:

Pamoja na maoni ya kila namna yanayoendelezwa kujadili mchakato wa Katiba nje ya Bunge hili, ni muhimu wahusika wapunguze jazba, chuki na upotoshaji. Bunge Maalum lisaidiwe kwa mawazo chanya ili limalize kazi yake.

Sisi tuliomo humu katika Bunge Maalum tuna wajibu wa kuifanya kazi yetu kwa umakini na kwa uadilifu ili kazi yetu iwe bora. Tujadiliane kwa uungwana. Tofauti za mawazo zisitufanye tuingize chuki na maneno yasiyofaa. Katika mabadiliko ya Kanuni nashukuru sasa Kiti kimepewa mamlaka ya kushughulikia utovu wa nidhamu ndani ya wakati. Lakini ninaamini haitakuwa lazima kwangu mimi au Makamu Mwenyekiti kutumia nguvu za mamlaka yetu ila tu pale itakapobidi.

Nawatakia nyote Mkutano wenye mafanikio kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!
Samuel Sitta - MB
MWENYEKITI BUNGE MAALUM LA KATIBA
 
Polepole aliona mbali sana, naunga mkono hoja ya uhaini iwe inaweza kumkabili mkuu wa nchi pale anapokengeuka rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
25 September 2026

Madaraka Yanakuwaje Halali ? | Uhalali wa Serikali EP. 3

View: https://m.youtube.com/watch?v=BR6RrXQCt_U

Madaraka yanakuwa halali kwa misingi gani?Katika sehemu hii ya tatu ya mfululizo wa Uhalali wa Serikali, tunaangazia muundo wa misingi ya uhalali wa madaraka kwa kutumia mawazo ya Max Weber na David Beetham, na kuyaweka katika mazungumzo na uchambuzi wa Profesa Issa G. Shivji kuhusu Tanzania.

Tunaangazia misingi mitatu muhimu: sheria au kanuni, uhalalishaji, na ridhaa inayodhihirishwa, na kuuliza misingi hiyo inatusaidiaje kuelewa matumizi ya madaraka katika mazingira ya Tanzania.

Pia tunaangazia masuala ya ushirikishwaji wa wananchi, uchaguzi, sheria na kanuni za uchaguzi, pamoja na mjadala kuhusu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

ElimUraia — kwa ustawi wa fikra tunduizi.

Kujua ni kuchagua.

*** VYANZO / SOURCES:

Max Weber — Economy and Society: An Outline of Interpretive Sociology. Edited by Guenther Roth & Claus Wittich. University of California Press, 1978. Vol. 2Kurasa zilizotumika: pp. 951–955.
[https://books.google.d...]

David Beetham — The Legitimation of Power, 2nd ed. Palgrave Macmillan, 2013.Chapter 3: “The Normative Structure of Legitimacy,” pp. 64–99.[https://www.bloomsbury...]

Issa G. Shivji — “The Rule of Law and Ujamaa in the Ideological Formation of Tanzania.” Social & Legal Studies, Vol. 4, No. 2 (1995), pp. 147–174.DOI: 10.1177/096466399500400201.
[https://repository.uds...]

The United Republic of Tanzania — The Independent National Electoral Commission Act, 2024 (Act No. 2 of 2024).Sheria inayohusu muundo, uteuzi na majukumu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. The official government legal collection confirms Act No. 2 of 2024. [https://emaktaba.judic...]

The United Republic of Tanzania — The Presidential, Parliamentary and Councillors’ Elections Act, 2024 (Act No. 1 of 2024).Sheria inayosimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.[https://emaktaba.judic...]
 
Polepole alikuwa mnafik, kwanini alipopata madaraka hakuyapa uzito hayo aliyokuwa akiyaamini na kuyafanya kwa vitendo.
Alikaa kimya na kejeli juu.
Ukitaka kujua mswahili alivyo "mpe hela"
 
28 September 2026

PAUL CHACHA MHAINI, CCM Haimiliki Jeshi': MADELEKA Ajibu Kauli ya CHACHA 'Vyombo vya Ulinzi na Usalama ni Mali ya CCM'



View: https://m.youtube.com/watch?v=kOezFb1ZnNE

Wakili Peter Madeleka amesema vyombo vya ulinzi na usalama havimilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikatiba, bali kauli ya Katibu wa NEC wa CCM, Paul Chacha, inaonyesha chama hicho kinavyovichukulia kama mali yake

Sababu na Mjadala wa Kauli

Kauli ya Paul Chacha: Septemba 26, 2026, huko Iringa, Katibu wa Oganaizesheni wa CCM, Paul Chacha, alidai kuwa vyombo vyote vya ulinzi, usalama, na mawaziri ni mali ya CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kilichoweka viongozi katika nafasi hizo

Msimamo wa Madeleka: Wakili Madeleka alijibu akisema kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, CCM haina umiliki wowote wa majeshi au vyombo vya dola, akiongeza kwa utani wa dharau kwamba "kwa mujibu wa Chacha, ukiitwa polisi, umeitwa CCM"

Kidiplomasia na Kikatiba: Wakosoaji na wataalamu wa sheria wanakumbusha kuwa Ibara ya 147 ya Katiba ya Tanzania inakataza mtu au chama chochote cha siasa kumiliki jeshi au vyombo vya ulinzi, ambavyo vinapaswa kuwa vya Jamhuri ya Muungano na vinavyofuata sheria badala ya maslahi ya chama kimoja
 
28 September 2026

MCH. PETER MSIGWA - HATA CCM YENYEWE INASHIKILIWA MATEKA, SISI WATANZANIA NI MATEKA" .

View: https://m.youtube.com/watch?v=YwAoXVl_wIk

Peter msingwa amesemwa anashangazwa na viongozi wa chama cha CCM kujimilikisha vyombo vya usalama wakisema wao ndo wanamiliki kijumla viko chini...
 
28 September 2026

Wakili Chegula Amkosoa Paul Chacha Kuhusu "Vyombo vya Serikali ni Mali ya CCM"


View: https://m.youtube.com/watch?v=ox_5skhQRiM

Wakili Chegula na wadau wengine wa sheria na siasa wamemkosoa vikali Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM anayeshughulikia Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, kufuatia kauli yake kwamba vyombo vya dola na viongozi wa Serikali ni mali ya CCM

Mukhtasari wa Mzozo wa Kauli Hii:
Kauli ya Paul Chacha: Wakati akihutubia mkutano maalum mkoani Iringa mnamo Septemba 26, 2026, Chacha alidai kuwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa Serikali ni mali ya CCM kwa sababu chama hicho ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo kupitia mfumo wake wa kuunda Serikali.

Ukosoaji wa Wakili Chegula na Wengine: Wakosoaji na wataalamu wa sheria, akiwemo Wakili Chegula, wamepinga kauli hiyo wakionya kuwa inakiuka misingi ya Katiba na sheria za nchi ambazo zinafanya vyombo vya dola kuwa mali ya wananchi na Taifa kwa ujumla, badala ya kuwa mali ya chama chochote cha siasa

Athari ya Mjadala: Kauli hiyo imeongeza kasi ya mjadala mpana nchini Tanzania kuhusu udharura wa kupata Katiba Mpya itakayotenganisha kabisa utumishi wa umma na itikadi za vyama vya siasa
 
Kwa ufisadi unaoendelea chini alikuwa sahihi
 
Back
Top Bottom