Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, alisema kuwa pendekezo la Tume lilikuwa kuunda muundo wa Muungano wenye uwiano zaidi kwa kuipa Tanganyika mamlaka yanayofanana na Zanzibar, huku Serikali ya Muungano ikibaki kushughulikia masuala ya pamoja kama ulinzi, uraia na sarafu.
Akizungumza katika mahojiano na ITV Aprili 30, 2014, Warioba pia alieleza kuwa Tume ilibaini baadhi ya mambo ya Muungano yaliondolewa kwa vitendo bila kufuata utaratibu wa kikatiba na hivyo kupunguza mamlaka ya Serikali ya Muungano.