PreGE2025 KUMBUKIZI: Kama Tembo ndio wana thamani, Serikali ya Samia ikapigiwe Kura na Tembo porini. Isituone sisi ni mabongolala

PreGE2025 KUMBUKIZI: Kama Tembo ndio wana thamani, Serikali ya Samia ikapigiwe Kura na Tembo porini. Isituone sisi ni mabongolala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu!

Mwananchi mmoja kutoka mji mdogo wa Lamadi, wilayani Busega, huko Simiyu amevuta hisia kuhusu tofauti kubwa ya thamani inayowekwa kati ya maisha ya binadamu na wanyamapori, hususan Tembo.

Masalu Ndunga anadai kuwa mwananchi akiuawa na Tembo, Serikali hutoa pole ya Tsh 50,000/- pekee. Lakini, mwananchi akimuua Tembo, anatakiwa kulipa faini kubwa ambayo si rahisi kuimudu.

Akiwa na hasira amesema:

"Serikali ya Samia ikachaguliwe na tembo! Isituone sisi ni mabongolala. Kama wao wanaona tembo wana thamani zaidi, basi waende porini wakae na Serikali yake Samia, wakapigiwe kura na tembo."

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

 
Wakuu!

Sikiliza huyu mwananchi anavyolalamika kuhusu utofauti wa thamani inayowekwa kati ya Binadamu na Tembo.

Anadai kuwa mwananchi akiuawa na Tembo, Serikali hutoa pole ya Tsh 50,000/- pekee. Lakini, mwananchi akimuua Tembo, anatakiwa kulipa faini kubwa ambayo si rahisi kuimudu.

Akiwa na hasira amesema:

"Serikali ya Samia ikachaguliwe na tembo! Isituone sisi ni mabongolala. Kama wao wanaona tembo wana thamani zaidi, basi waende porini wakae na Serikali yake Samia, wakapigiwe kura na tembo."

Tembo ni wachache na adimu kuliko binadamu inabidi walindwe kwa wivu mkubwa zaidi.
 
Tembo naye ana haki zake
Kwanza nyie ndiyo mnavamia
Makazi yao
Alafu nyie binadam msijifanye
Kama ndiyo mna haki ya kuishi
Duniani pekee

Ova
 
Kwa akili zake huyo mwananchi hata nyau ana thamani kuliko yeye
 
Naona mwaka 2024 Serikali ilipeleka mapendekezo wizara ya fedha ili kutekeleza malipo ya viwango vipya kama ilivyoelekeza kanuni ya kifuta jasho kwa waathirika.

Je, imekwisha anza kutekelezwa?

Fidia ya kifuta machozi kwa wafiwa (1,000,000/=).

Fidia ya madhara baada ya kupelekea ulemavu wa kudumu kwa muathirka (500,000/=).

Fidia ya kumfariji muathirika aliyepata maumivu au majeraha ya muda mfupi (200,000/=).

Fidia kwa kifo cha mifugo mikubwa (hasa ng’ombe) ni elfu hamsini (50,000/=)

Ingawa pia walalamikaji wana makosa, wanaacha makazi yasiyo ya hifadhi wanajipenyeza kufuata makazi ya tembo.

Wahame huko.
 
Tembo ni wachache na adimu kuliko binadamu inabidi walindwe kwa wivu mkubwa zaidi.
Hujamsikiliza anayeongea hapo

Ako na pointi

Aliyetakiwa kuwajibishwa ni mchunga Tembo, kwa nini anawaachia waingie kwenye miji na mashamba ya kijiji?

Mchunga ng'ombe akilisha mazao, huwajibishwa mchunga ng'ombe, sasa kwa nini mchunga Tembo anaposhindwa kuwachunga vema waingie mtaani kuwadhulu watu, ikitokea watu wamejitetea wakauwa mmoja, wanawajibishwa wao?
 
Ni sheria ya kipumbavu sn, ukiua fisi milioni 7 hata ukigonga kwa bahati mbaya na gari lakini fisi akiiua mtu fidia laki 5, waliotunga ni hawa wajinga wa CCM
 
Back
Top Bottom