Kumbukizi kutoka kwa Polepole: Viongozi wote wa CCM tuna V8 unaijua wewe, AC muda wote

Kumbukizi kutoka kwa Polepole: Viongozi wote wa CCM tuna V8 unaijua wewe, AC muda wote

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
608
Kila jambo lina wakati wake amini nawaambia tukumbuke kesho yetu ipo mikononi mwa Bwana kuna lakujifunza usikute ametekwa na V8 ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Niwatakie Jioni Njema.
 
Context:
Alikuwa anajibu hoja ya Lissu kuwa wametumia hela za vitambulisho kununua V8.

Kwa chama Chenye Umri na historia ya CCM utakuwa mjinga ukianza kushangaa kwanini kinamiliki V8.
Sioni kosa hapo, ni kweli CCM wanatembelea V8, na Ukwasi wa chama chao wanauwezo wa kununua hizo V8 bila hata kuiba.

Mtu anioneshe ubaya wa hiyo statement uko wapi? Alikuwa kazini katika kazi yake ya Itikadi na uenezi.
Ulitarajia kuskia nini kutoka kwa muenezi?
Nachopata tabu ni kuelewa uhusiano wa kutekwa kwake na statement za zamani.

HAKUNA BINADAMU ANASTAHILI KUPOTEZWA SIMPLY KWAKUWA AMEONGEA AU AMEKOSOA KITU FLANI, HUU UFARISAYO KAMA SIO PROPAGANDA ZA WALIOMPOTEZA.
 
Swali lilikatwa makusudi tu ionekane anajikosha ila lilikuwa ndiyo jibu sahihi kwa swali aliloulizwa.

Slowdown kajichetua mwenyewe tu,angeamua kukaa zake kimya angejilia mema ya nchi wala hakutemwa na mfumo km akina Muro!
 
Magufuli Polepole wote wameondoka wamemuacha Tundu Lissu ni uwezo wa Mungu tu.
 
Alikuwa anaongelea nini na kwa muktadha upi na content gani ?

Naendelea kusema two wrongs don't make a right, hata adui yangu siku nikiona anatendewa ndivyo sivyo nitalalamika (sio kwamba sababu ni yeye bali sababu ya tendo halifai)
 
Kwa hivyo kwa kuweka hio video unataka tumchukie Polepole ? baada ya kutoka Cuba mbona hujazungumza alipo mtetea Lissu na kusema aachiwe? mbona hujazungumza alipoikosoa CCM dhidi ya wizi wa kura?

Mbona hujazungumza alipokosoa ufisadi ndani ya CCM?

acheni unafiki.
 
Back
Top Bottom