MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Lucius Domitius Aurelianus,
Hili ni jina kubwa mno kwenye historia ya dunia: Huyu alikuwa ni jemedari mahiri kabisa wa vita (Impeator) na baadaye akaja kuwa mfalme wa bora wa Dola la Roma (Caesar). Wengi humkumbuka kama The Emperor Who Saved The World, japo alitawala kwa miaka mitano tu na akauwawa na wasaidizi wake.
Tatizo lilianza pale ambapo walinzi na wasaidizi wa mfalme walikuwa na nguvu kubwa za kisiasa hadi kujihisi kwamba na wao pia wanaweza kufanya kama mfalme. Yote haya yalianzisha na siasa za makundi zilizokuwepo nchini Roma tokea mwaka 235 AD baada ya kumuua mfalme Severus Alexander. Kwa miaka yote hii hadi kufika 285 AD, Roma ilikuwa inapata wafalme ambao hawatawali zaidi ya miaka 5 bila kupigwa kisu au sumu.
Sasa baada ya miaka mingi akatokea huyu mwanajeshi anaitwa Lucius Domitius Aurelianus, ambaye aliliunganisha dola la Rumi upya ndani ya muda mfumi na kuwafukuza wageni waliovamia na kukata vipande taifa na kuzaa vijitaifa vingine vidogo.
=========================================================================
CHANGAMOTO KUBWA aliyokutana nayo Aurelian ni kwamba wanajeshi wake, wanasiasa wenzake, majasusi, wasaidizi wake na walinzi wake (The Praetorian Guard) walikuwa wameshazoea siasa chafu za makundi na kuuana, hivyo hata dola lilipotulia na kusukwa upya, bado akili za hawa watu zilikuwa zimekaa vibaya na kukataa kujirudi kuwa za kawaida.
Wanajeshi walikuwa wakishinda vita ni lazima waibe mali (Pillaging), wabake (Rape), kuua (Murder), na kufanya uharibifu jambo ambalo lilikuwa linaleta shida kwa Aurelian ambaye alikuwa na lengo la kurudisha nchi kwenye mstari. Hawa watu wameshazoea vyakunyonga, vya kuchinja hawaviwezi.
Basi kuna siku moja, msaidizi wa Aurelian akiwa anajiandaa na vita msaidizi wake mmoja wa karibu aitwaye Eros alifanya makosa, na akifahamu fika kwamba atapewa adhabu nzito na Aurelina, aliamua kujilinda kwa kughushi nyaraka za kijasusi na kuweka muhuri wa mfalme. Nyaraka hizo zilikuwa na orodha ya majina ya majasusi wa mfalme (The Praetorian Guards) ambao walitakiwa kuuwawa kwasababu ya makosa yao mbalimbali ya kiuongozi ambayo waliwahi kuyafanya.
Majasusi baada ya kupata barua waliitisha kikao na watu mbalimbali kwamba Mfalme lazima achinjiliwe mbali kwasababu alikuwa anapanga kuwaua wenyewe. Hivyo ilikuwa ni lazima wamuwahi yeye. Basi wakasuka mpango mzito na baadaye Aureliana akachinjwa vibaya. Wakati huu mkakati unaendelea Bunge la Roma ambako alikuwa na mahasimu wengi wakapitisha waraka wa kulaani vitendo vya mfalme aliyekufa "Damnatio Memoriae" kama njia ya kufuta kumbukumbu zake na kuwatishia wengine wasiige. Kiufupi zilikuwa ni harakati za kufuta LEGACY.
Bahati Mbaya, ikaja kufahamika kwamba nyaraka zile hazikuwandikwa na mfalme bali zilighishiwa na msaidizi wake wakisaidiana na majasusi. Mfalme alikuwa mkali kweli, lakini hakuwa na lengo la kumuua mtu yoyote yule.
=======================================================================
Majasusi na Wasiaidizi walizoea siasa chafu za kuua wafalme, na kutumia kila mbinu chafu kufikia malengo. Hata nchi ilipoanza kutulia watu kama wale hawakuweza kurudi kwenye hali ya ubinadamu wa kawaida.
Ndiyo maana Adolf Hitler alivyochukua nchi, kitu cha kwanza kukifanya ni kuhakikisha anaua maelfu ya majasusi na mgambo kama The Brown-Shirts aliowatumia kufanya siasa chafu zilizomuingiza madarakani. Kule Urusi, Stalin aliwatumia majasusi kufanyanya siasa chafu za kuwaua kina Kamenev, lakini baadaye akafahamu kabisa kwamba katika kutawala kipindi cha amani, hawezi kuwatumia tena hawa walioozea vya kuny'onga. Hadi kufika mwaka 1935 Stalin alikuwa ameua vijana wake majasusi na wanajeshi 15000, ambao walitumia kuua mamilioni ya warusi wasio na hatia.
Alifahamu fika, kwamba kama wamezoea damu, hawawezi kuacha!
Hili ndilo lilimkuta Mfalme Aurelian.
Na ndilo linaendelea huko katika nchi ya iitwayo KUSADIKIKA.
========================================================================
ENIWEI, pray for discernment....