Mkongwe Mzoefu
JF-Expert Member
- Aug 10, 2018
- 861
- 2,515
Kwako Mwalimu Nyerere;
Wiki hii tunaitumia kukukumbuka wewe na uongozi wako.
Sisi wazee tunakumbuka mbali zaidi hasa zile nyakati za vita Kagera ambavyo wapo wenzetu ambao waliambulia vilema na mpaka leo tunao wakiwa hai na huku wakilipwa Pension ya Laki 1 kwa mwezi na Hazina na hakuna msaada wowote.
Wapo Waalimu, Waganga na wahandisi, makarani na wengine wengi waliokuwa Permanent and Pensionable wote bado wanalipwa hiyo laki mojamoja.
Cha kusikitisha Mwalimu, wale ambao Mungu amewaacha wawe hai kwa serikali hii ya CCM yako uliyoiacha wanaonekana ni chukizo na hasara, kwamba bora fedha zitumike kwa mambo yao ya anasa na sio kuwaongezea sehemu ya pension kama sheria isemavyo.
Waziri wa Fedha na huyu Rais aliyeko madarakani walituambia kupitia Bunge wameunda tume kuangalia jinsi ya kuboresha lakini hakuna lilofanyika.
Ila leo wanajinasibu kuwa eti wanafata falsafa ya mwalimu, jee hii ya kutowajali wazee ilikuwa ndio falsafa yako au wanakusingizia kwa vile uko Kaburini?
Tunaenda kwenye uchaguzi, bora tuwaeleze watoto wetu na wajukuu kuwa ANAYEMDHARAU MZAZI WAKO HASTAHILI KUPEWA HESHIMA YA KURA.
Mwalimu huko uliko tuombee mwisho mwema