Kumbukizi: Ruge Mutahaba, shujaa jasiri muongoza njia

BenKaile

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
443
Reaction score
375
HII NI MOJA YA CONVERSATION KUHUSIANA NA YEYE BINAFSI KIUFUPI NA JUHUDI ALIZO FANIKIWA;



SWALI: Ruge mutahaba ni nani?

RUGE: Nimezaliwa Brooklyn, New York, Marekani, mwaka 1970. Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.



SWALI: Nini kilichotokea hadi ukajikuta uko clouds FM.

RUGE: Wakati nipo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo tuka-build good friendship. Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment. Hii ikazaa Clouds FM 88.4, ikazaa pia Prime Time Promotions iliyokuwa ina deal na matamasha ya muziki kuanzia Summer Jam ambayo baadaye ikawa Fiesta. Na pia ilihusika kuleta wanamuziki wote wa nje kuanzia kina Koffi (Olomide), Wenge BCBG, Chaka Khan, Sean Kingston, Jay-Z na Beyonce, 50 Cents, Rick Ross, Buster Rhymes, Shaggy, Cabo Snoopy, Davido, na wengine wote uwajuao wa kimataifa. Ni wengi kwa kweli. Afrika Mashariki na ya Kati hakuna aliyeweza na anayeweza kuleta wanamuziki nyota wa dunia kama Prime Time.




SWALI: Tuambie kuhusu THT.


RUGE: Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri.
Hivyo nikaona ni bora nianzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika. Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kama Maunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo.



- REST IN PARADISE RUGE MUTAHABA
 
Huyu jamaa alikuwa ni dhahabu,elimu ya USA sio mchezo,alisoma mambo ya finance,lakini alikuwa na uelewa mpana katika mambo ya muzik!
Hakika tumepoteza lulu.
 
Kila nikiona mafanikio ya Diamond, Barnaba, Ben Paul, Nandy, Tuddy Thomas na wengineo namkumbuka Ruge
 
Akili kubwa,,Juzi nimetoka kucheki interview ya Nandy kaongea mengi kuhusu Ruge kwenye Ayo TV..Doooh aya bhana.
 
Umeanza lini kufuatilia music, nani alimsaidia kukutana na davido unaijua diamonds are forever
Sallam sk ndiye aliyemuunganisha Diamond na Davido,sababu Sallam alikuwa muwakilishi wa Davido Africa mashariki kama ilivyokuwa kwa Sanday (meneja wa wizkid) ana mmeneja wa Diamond kwa nchi za magharibi.Kwa maelezo zaidi ingia Global publisher tafuta mahojiano ya Sallam sk na kama hujui behind ya mafanikio ya AY sallam ndiye alikuwa akimmeneji AY pamoja na kampuni yake ya Unity.
Soma thread ya mahojiano ya Sallam na Global Publisher utamuelewa Sallam Sk.

Diamond mtu wa kwanza kuamini uwezo wake ni Papaa misifa ndiye aliyekuwa meneja wake wa kwanza,wa pili ni Raquel mmiliki wa kampuni ya upiga picha,graphics na kudesign website na utengenezaji tamthilia (I-VIEW) ,baadaye Ruge akaona dogo ana potential katika market,so akaamua wafanye biashara na ndio Diamond are forever zilipo anza.Ila mwenye mchango mkubwa mwenye mziki wa Diamond na aliyekubali kuwekeza kwa Diamond mwanzoni ni PAPA MISIFA yy ndiye anaye style sifa.
Rip Ruge.
 
Papa Misifa na Bob Junior.
 
Mhh Ruge jamani Endelea kupumzika kwa Amani but we miss you brother [emoji24][emoji24]
 
Papa Misifa na Bob Junior.
Sorry nimekosea kukutag sio wewe ki kijana hapo nilikua namuelekeza
Nani alimleta Davido mara ya kwanza tanzania unajua remix ya number one imefanywa na Tuddy Thomas unajua Thomas alikua THT ndipo kijana alipounganishwa afanye wimbo, unaijua One africa music festval unajua zile nyimbo za collabo kama cocoa n chocolate aliunganishwa na nani. Sema ni vile alikua hapendi showoff
 
Umesoma mahojiano aliyofanya na Global publishers au kwa makusudi umeamua kuwa mbishi.Sallam si mtu mdogo yeye na AY ndiye walikuwa maagent wa wasanii wengi wa Nigeria kwa upande wa EA.Sasa Tuddy ktk number one kafanya nini zaidi ya kukopi na kupesti alichofanya Shed Clever.

Wewe jiulize kama yy ndiye aliyesimamia collabo mbona kashindwa kwa wasanii wa THT kupata collabo za kimataifa,pamoja na kuleta wasanii wengi kwenye Fiesta au nitajie msanii mmoja wa THT aliyeunganishwa na akapata collabo ya kimataifa?kama hamna jiulize kwa nini walishindwa.Collabo zote kubwa za AY basi jua moja ya mtu aliyezisimamia ni Sallam,usimwone Diamond mjinga kumwingiza Sallam kwenye timu yake ya mameneja.

Ila sikulazimishi ila ukweli ndio huo,kama hujui meneja wa Diamond Sallam ndiye anayesimamia kazi za Wizkid EA na meneja wa Wizkid Sunday ndiye anaye simamia kazi za Diamond platnumz Nigeria na Africa Magharibi.

Kwa kuwa umeamua kubisha na reference nimekuwekea basi endelea kubisha ila huwezi kubadilisha ukweli,ulio wazi.
 
Pumzika rugemarila mahaba! Hata sijui Yamaha la fiesta mwaka huu itakuwaje! Maana wewe ulikuwa entertainment genius
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…