The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Sauti Ya Watu – Nay Wa Mitego
UTANGULIZI:
Hii sio sauti ya kiharakati wala
Ukombozi wa musa na fimbo yake
Bali haya ni maumivu ya mnyonge
Anaye wakilisha walala hoi wenzake
Kwenye kinywa kilichokosa
Pa kusemea hisia zake
UJUMBE:
• Natanguliza samahani kwa wale nitakao wakwaza
Yamenifika hapa nimeshaidwa kunyamaza
Wapo wengi kama mimi wenye sauti kama mimi
Sijui ni ubinafsi hawasemi kama mimi
Anko alisema kwamba tuko uchumi wakati
Haya tudanganyeni tena tupo uchumi wa ngapi
Wapigaji waliotumbuliwa ndio wamerudi mzigoni
Kamradi kamillion mnataja mabilioni damn!.
Amna huruma ninyi na sisi masikini.
Hivi hio bajeti si mngeweka hospitalini
Na huyu ndio Yule binti aliemaliza chuo
Ila uhakika wa kazi aliyosomea uko chuo
Hajui atafanya nini amebaki na vyeti vyake
Anajuta alisoma nini si angejiuza ka wenzake
Panya road jina la pili la kijana asiekua na ajira
Na risasi ndio hukumu inamfika hata asie na hatia.
•Hakuna uafadhali wa maisha vyuma vimezidi kukaza
Mambo yanaharibika na wapinzani wamenyamaza
Kama ulimpenda baba huwezi mwelewa mama
Na kama hukumpenda baba bado utamchukia mama
Yani kumpenda mama na kumchukia baba ni sawa
Kuipenda nyama halafu upendi mchuzi wake.
>_Mmmh, hii ni sauti ya watu
(Na hili giza tunaenda wapi?
Tunafanya nini?
Tutaishi vipi?
Hata mwanga hauonekani!._<
• Ukiona mtoto halii njaa na nyumbani hakuna chakula
We mchunguze vizuri kuna sehemu anakula
Mwambieni ukweli mama hali mbaya sio tandale sio masaki.
Kilio cha kila mtu pesa hakuna imefichwa wapi?
Siku hizi mpaka vigenge vya nyanya TRA wanataka kodi,
Masikini amejichanga vipesa benki anakatwa tozo.
• Hizo V8 mnazonunua si hela zetu za kodi
Naona mna enjoy kuliko hata walipa kodi.
Mnajenga hospitali madawa hakuna,
Mnatujengea shule lakini walimu hatuna,
Kudanga ndio kimbilio kubwa la dada zetu
Ndio mtaji asiokopeshwa hakatwi tozo wala kodi.
Hivi mna akili nyinyi!? Mnashauri tujiajiri
Wakati nyinyi wenyewe mpaka sasa mmeajiriwa
Achieni nafasi zenu na nyinyi mkajiajiri.
Hapo ndipo nitapoamini kweri nyie washauri wazuri
•Kati ya mtawala na mpinzani hapa muogo nani
Mtawala aliekataza mikutano isifanyike;
Au mpinzani asieifanya na anajua ni haki yake?