JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tarehe kama ya leo Julai 19, 1977 miaka 46 iliyopita Timu ya Simba ilitoa kipigo kikubwa cha kihistoria kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga, mshambuliaji Abdallah ‘King’ Kibaden alifunga magoli matatu ‘hat trick’ na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuwahi kufunga hat-trick katika mchezo baina ya timu hizo.
Waliofunga magoli katika mchezo huo ni Kibadeni (Dakika ya 10, 42 na 89), Jumanne Hassan ‘Masimenti’ (60 na 73) na Selemani Sanga aliyejifunga (20). Tangu wakati huo haijawahi kutokea kipigo kikubwa kama hicho katika mechi baina ya timu hizo.
Pichani Kibadeni ni wa tatu kutoka kushoto.