Kumbukizi: Tarehe kama ya leo Mwaka 1977, Simba iliifunga Yanga magoli 6-0

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Tarehe kama ya leo Julai 19, 1977 miaka 46 iliyopita Timu ya Simba ilitoa kipigo kikubwa cha kihistoria kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga, mshambuliaji Abdallah ‘King’ Kibaden alifunga magoli matatu ‘hat trick’ na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuwahi kufunga hat-trick katika mchezo baina ya timu hizo.

Waliofunga magoli katika mchezo huo ni Kibadeni (Dakika ya 10, 42 na 89), Jumanne Hassan ‘Masimenti’ (60 na 73) na Selemani Sanga aliyejifunga (20). Tangu wakati huo haijawahi kutokea kipigo kikubwa kama hicho katika mechi baina ya timu hizo.

Pichani Kibadeni ni wa tatu kutoka kushoto.
 
Watu mnabandua magamba ya vidonda.@scars waitwangwa kunu.
 
Viewers watakuwa wengi kwenye uzi huu ila swala la kuchangia litakuwa gumu especially kwa wana uto
 
Abdallah KIBADENI mputa aliweka goli tatu.

Aliweka hatrick-3.
Simba 6
YANGA 0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…