Kumbukizi ya Magufuli: Nami Niseme Mambo Sita na Danis Mpagaze

Barca

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
1,629
Reaction score
1,960
Kumbukizi ya Magufuli: Nami Niseme Mambo Sita!

Denis Mpagaze
_________________________

Ni mwaka wa nne sasa Mzee John Pombe Magufuli amelala!

Namisi sana ziara zake, hotuba zake, utani wake, ukali wake, Kiswahili chake na ucheshi wake!

Magufuli aliongozwa na mambo sita! Nimeyaita
Umagufuli wa Afrika yaani Magufulification of Africa.

Hili neno nimeliiba kwa Prof. Patrice Lumumba wa Kenya!

Lengo la Umagufuli wa Afrika ni kuufanya utendaji wa Magufuli kutumika Afrika nzima!

Ni utendaji ambao tukiutumia Afrika lazima tutoboe walahi! Haki ya nani sitanii😀! Mambo yenyewe haya hapa!

Jambo la Kwanza: Punda Haendi Bila Viboko!

Ukimbembeleza punda atakupiga mateke halafu mzigo hautafika. Dawa yake ni viboko tu.

Mtangulizi wa Magufuli yaani Mzee Jakaya Kikwete aliwabembeleza watu wakamuangusha!

Alipomkabidhi Magufuli kijiti akasema mtanikumbuka na kweli wakamkumbuka!

Ila enzi za Kikwete kuna watu walikula bata!

Watu walimwagiana zawadi za pesa na magari siku za birthday.

Enzi za Magufuli ukaja mtindo wa kumwagiana maji siku za birthday😀😀. Kwakweli ilikuwa ghafla sana!

Halafu tuliishi maisha ya kibabe sana.

Unakuta na mtu anakwambia unanijua mimi nani? Nitakutwanga halafu nikulipe.

Loh kuna watu walikuwa na jeuri ya pesa nyie!

Tuliishi maisha ya huna jina haki yako utalipwa na Mungu!

Watumishi wa umma walikuwa miungu watu; mitaani watu waliogopana!

Pesa ilisambaa mtaani. Mwenye nacho alikuwa nacho hasa na fukara alikuwa fukara haswa.

Vijana wadogo waliwatuvimbia mpaka wazee na mvi zetu huku mtaani.

Vibinti vidogo vilisukuma ndinga kali na wakati masela wakisukima mikokoteni kwa jasho😀😀

Sekta binafsi walitoa huduma nzuri kuliko serikali iliyokusanya kodi.

Dhuluma ilinuka na waliofanya hawakufanywa lolote.

Magufuli alipokamata kijiti akasema katika serikali yangu tajiri anaweza kufanywa lolote na walifanywa kweli.

Watu walibatizwa kwa moto kama ilivyotabiriwa na Yusufu Makamba, baba yake na Januari Makamba.

Januari ni yule kijana aliyesema madaraka ni sawa na koti la kuazima, unapopewa usilivae kwa mbwembwe maana siku mwenye nalo akilichukua utafedheheka.

Lakini tuache na matani, watu walijisahau sana enzi za Jakaya.

Magu alitembea na tumbua tumbua nchi ikakaa kimya, mikwara mtaani ikaisha. Starehe na safari za bata kimyaaa🙊🙊.

Watu wakaishi maisha ya hatujui siku na saa ya kutumbuliwa kwetu amina!

Nidhamu ya kazi ikarudi hata kama ilikuwa nidhamu ya woga.

Watu wakachapa kazi Tanzania tukaibukia uchumi wa kati hata kama hatukula na kushiba.

Mzee Magu hakuwa na muda wa kubembelezana kama tunavyowabembeleza watoto wa siku hizi.

Yaani kunywa uji hadi uwekewe katuni.

Zamani mtoto ukigoma kunywa uji ulizibwa pua ili uchague moja; kunywa uji au kufa!

Enzi za Magufuli watu walibanwa mapua ili wajenge nchi, watu wakamshambulia Magufuli anavunja haki za binadamu.

Sasa hapa Magufuli alivunja haki za binadamu au haki za wezi? Kwani mwizi ni binadamu?

Kwakweli mwizi siyo binadamu. Kama huamini subiri uibiwe ndiyo utasema mwizi ni binadamu au mnyama.

Kumbe kumuenzi Magufuli kwa dhati ni kumtandika punda viboko vya kutosha mpaka mzigo ufike.

Jambo la Pili: Ukicheza na Nyani Utavuna Mabua.

Tanzania tulicheka na nyani kwa muda mrefu mali zetu zikaenda kujenga maisha ya wakubwa sisi tukashindwa hata kununua panado.

Yaani kunywa maji mengi ndo ikawa tiba ya kila ugonjwa Tanzania.

Ukiugua malaria utasikia kunywa maji mengi, ukiugua kichwa kunywa maji mengi, ukijisikia uchovu kunywa maji mengi.

Yaani kila mtu alikuwa daktari wa maji mengi. Mapafu yakijaa maji ukafa tunasema mapenzi ya Mungu. Kweli ujinga hauna huruma.

Watu waliiba hadi wizi ukawa fasheni. Ukipata cheo usiibe uliitwa fala. Ukiiba ukakamatwa uliitwa fala pia.

Utakamatwaje? Ilifikia kipindi cheo kikaitwa ulaji badala ya dhamana.Hadi madiwani walisumbua mjini.

Unakuta eti diwani naye kashikilia tenda ya kujenga barabara na wakati hata toroli hana.

Watu walikuwa na pesa kuliko serikali. Leta kama tulivyo ndo kilikuwa kibwagizo katika kumbi za starehe!

Magufuli alipoingia Ikulu hakucheka na nyani. Mtumishi aliyevurunda kwa Magufuli alivuliwa nguo hadharani, halafu anatumbuliwa.

Tabia hii ya kuwavua watu hadharani atakuwa aliiga kwa Mwl. Nyerere.

Enzi za Nyerere ukikamatwa na rushwa ulikula mboko kabla ya kuingia jela na nyingine wakati unatoka ili ukamuonyeshe mke wako.

Nyerere bhana. Ina maana wezi ni wanaume tu? Wakati mwingine wanaume wanaiba ili kulisha familia, michepuko na mabaamedi.

Huo ni ukarimu wa mwanaume. Sasa je, kwani mchepuko naye simtu? Ulitaka ale wapi?

Gonga cheers mwaume unayelisha familia, michepuko na mabaa medi. Utalipwa na Mungu!

Magufuli hakuwakazia wezi wa ndani tu. Aliwakazia hadi wezi wazungu tukaogopa ati tutatengwa na dunia.

Mwamba aliwabana kila kona hadi Richard Mgamba, mwandishi nguli wa habari za uchunguzi katika sekta ya madini akagonga cheers.

Kulikuwa na mambo ya ajabu sana huko kwenye madini. Mgamba anakwambia kuna siku waziri wa madini Tanzania alikatazwa kuingia mgodini kwa sababu hakuwa na appointment.

Imagine! Madini ni yenu, ardhi yenu, nchi yetu halafu mnaambiwa hamna apointment, subirini tutwaambia tulichozalisha.

Upuuzi kama huu ndo Magufuli alishindwa kuuvumilia. Akajitoa kulala nao mbele hadi tukapata share, from ziro share to 16 percent share.

Kumuenzi Magufuli kwa dhati ni kuacha kucheka na nyani ili tuijenge Afrika! Afrika siyo masikini,

Afrika siyo bara la giza, lingekuwa bara la giza wazungu na wachina wangeshinda huku?

Jambo la Tatu: Ukimrushia mawe kila mbwa anayekubwekea hutofika uendako!

Endapo Magufuli angesikia kelele zilizomzomea kutoka ndani na nje ya nchi asingefanya lolote.

Wapo waliomuita dikteta, wengine walimuita mlipa visasi, wengine walimuita Mungu mtu, wengine mjuaji, wengine mbinafsi na wengine mgonjwa.

Wote aliwaona kama ngoma inayopiga kelele lakini ndani hamna kitu. Akina debe tupu haliachi kupiga kelele.

Kelele mara nyingi hutoka kwa vitu visivyokuwa na thamani. Sarafu zinapiga kelele, noti hazipigi kelele. Aliwapuuza wote.

Wahenga walisema anayekula bila kupiga mswaki atasema chakula si kitamu. Hata samaki akioza kichwa ndo kinaanza kunuka.

Kwa miaka sita ya utawala wake yalifanyika maendeleo yenye hadi ya miaka 60!

Kwahiyo kumuenzi Magufuli kwa dhati ni kuchana na mbwa wanaokubwekea na kuelekeza nguvu, akili na utashi katika kujenga nchi.

Huwezi kujenga nchi kwa kusifiwa. Chukua hii. Maendeleo ni vita. Vitani hakuna kuchekacheka kama wehu!

Jambo la Nne: Greatest Happiness to the greatest number of people.

Msingi wa huu ulianzishwa na wanafalasafa Jeremy Bentham na John Stuart Mill.

Maana yake ni kwamba, unapofanya maamuzi yoyote yale angalia kama matokeo yake yataleta furaha kubwa kwa watu wengi.

Yaani kama unadhani ukichinja wala rushwa watu wengi watafurahi na kupata ahueni ya maisha chinja tu.

Wamefanikiwa sana kule China. Halina utu lakini hakuna namna, maana hata hao wanaoshughulikiwa hawakuwa na utu.

Kadhalika maamuzi ya Magufuli yaliangalia watu wengi walitaka nini bila kujali hadhi yao.

Wengi wakifurahia uamuzi wako, wachache wakanuna kanyaga twende.

Magufuli akiuliza "Nimtumbue nisimtumbueee?" Wengi wakasema tumbua anatumbua bila kujali una kisukari au presha kwa sababu sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

Hii ndiyo siri ya maskini wengi kumlilia Magufuli hadi wengine kuzimia na kufa kabisa. Ukikuta maskini anamponda Magufuli ujue amelamba!

Ni kutokana na kanuni hii ndo maana Magufuli hakulipa uzito suala la nyongeza ya mishahara maana aliamini lingefurahisha watu wachache tu.

Nchi hii sasa inatakribani Watanzania milioni 62 lakini wanaolilia nyongeza ya mshahara ni chini ya milioni moja.

Kwa Magufuli ilikuwa ni bora kupeleka huduma za afya kwa maskini ili nao waishi kabla kufa kuliko kuwaongesha mishahara wachache.

Alipambana maskini wapate umeme wakapata, watibiwe vizuri wakatibiwa, vituo vya afya vikatapakaa hadi vijijini, tena vina hadhi ya hospitali za wilaya.

Alipambana maskini wasome vizuri wakapewa elimu bure, barabara na maji vikawafuata maskini.

Ukweli ni kwamba alifanya hivyo kwa sababu maskini hana kitu zaidi ya umaskini wake. Maskini ni mtaalamu wa shida.

Msingi Tano: Mtegemea vya nduguye hufa maskini!

Siku zote Magufuli alituaminisha Tanzania ni tajiri, hatuna haja ya kujikomba kwa wazungu kwani tutakula hata visivyolika.

Hata ushoga ni chakula lakini chenye laana. Alisisitiza tufanye maendeleo kwa fedha zetu.

Alipenda kusema tusiwaamini sana wazungu na misaada yao tukidhani wanatupenda.

Wazungu ni kama fundi majeneza, ukifa ndo fursa kwake.

Akikuuzia jeneza akasema karibu tena usichukie, ile ndo kazi yake maana hali kwako. Hata hongera na pole jibu lake ni asante.

Magufuli hakutufundisha kuwachukia wazungu bali alitufundisha kwamba ukiona mbuzi anakula nyama badala ya nyasi huyo siyo mbuzi, ni simba, usimsogelee utakugeuza kitoweo.

Msaada wa mzungu ni mbuzi mla nyama! Itoshe kusema tu hakuna vya bure duniani.

Kwanza vya bure vinadhalilisha bana. Hata kijana anayetumia gari la baba yake hawezi kufungua mdomo kwenye kikao cha vijana wanaomiliki baiskeli zao.

Alisisitiza tupige kazi tutatoka tu! Ngoma haipigwi kwa mkono mmoja ikaburudisha! Maana yake serikali peke yake haiwezi. Kila mtu ashiriki. Mkono mmoja hausongi ugali.

Tutafute vya kwetu. Magufuli alilisimamia hilo. Hakupeleka pua yake Ulaya kuombeleza.

Mwamba ulisafiri kutoka nyumbani kwenda nyumbani, tena mara nyingi alitumia usafiri wa barabara na njiani aliwabatiza wahalifu kwa upanga.

Ilifikia kipindi viongozi wakisikia Magufuli anafanya ziara kwao walisali sala zote!

Changamoto nyingi alizimalizia njiani ndio maana wananchi waliposikia Magufuli anapita walimlaki barabarani mithili ya Yesu alivyolakiwa enzi zile.

Kumbe kujifunza kujitegemea ndiko kumuenzi Magufuli kwa dhati.

Jambo la Sita: Liwezekanalo leo lisingoje kesho!

Waha wanasema supu ya mbwa inanywewa ikiwa ya moto ingawa wanaokula mbwa siyo waha, ni wahehe na wachina.

Magufuli alifanya mambo mengi kwa wakati mmoja maana alijua maisha ya mwanadamu ni mafupi mno, leo upo kesho umenyauka.

Yaani ndani ya miaka sita amefanya mambo ya miaka 60 kama alivyoimba Obedi Dube, Afrina Poet!

Magufuli hakuwa mtu wa tuko mbioni kutekeleza, Magufuli hakuwa mtu wa kero zenu nimezibeba, Magufuli hakuwa mtu wa njoo kesho, Magufuli hakuwa mtu wa kuna mishe nasikilizia! Alikuwa mtu wa papo kwa papo!

Katika kusema kwake nyeusi iliitwa nyeusi na nyeupe ikaitwa nyeupe.

Katika hilo Mgufuli akawa gumzo kwa mamluki na wazalendo, gumzo kwa mashetani na malaika, gumzo kwa washenzi na waungwana, gumzo kwa wataka shari na wataka shere, gumzo ndani ya nchi na nje ya nchi, gumzo mijini na vijijini.

Hakika ya kujifunza kwa Magufuli ni mengi! Moja kubwa kuliko yote ni kwamba kuna umri ukifika unatakiwa uache kuwa rafiki wa kila mtu. Wengine salam tu inatosha.

Watu wanaweza kusafiri umbali mrefu kuja kukuzika, lakini wakashindwa kutembea hatua kumi kuja kukusaidia wakati wa shida.

Magufuli pia ametufundisha kwamba Afrika kumbe tumekua. Tunaweza kujisimamia. Tuache kunyonya dole gumba. Tuache utoto.

Tusiwe kama mtu aliyelala njaa maana ukimuuliza hujambo? Atakwambia sijambo!

Leo namuenzi Magufuli kwa kutoa ofa ya vitabu vyangu 13 kwa Sh 13,000 tu. Ofa ni kwa softcopy. Mpesa hii 0740590451. Tuma hela sasa. Ukitaka hardcopy piga 0753690907!

Vitabu hivi hapa!

1. Malezi: Muandae Mwanao na Hadhi
2. Biashara Huanzia Kichwani Siyo Mfukoni
3. Fikra Tunduizi: Tungo za Kufikirisha
4. Wasomi Huru Gerezani
5. Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana
6. Ukombozi wa Fikra za Mwafrika
7. Fungua Ubongo
8. Miamba ya Afrika
9. Viongozi Walioandika Majina yao Vibaya
10. Mbinu 16 Alizotumia Yesu Kutoboa
11. Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa
12. Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa!
13. Ukombozi wa Fikra

Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!
 
Silazimishi mtu kumkubali JPM, kwangu mimi, huyo ndo alikuwa Rais haswaa, mpenda nchi, mtetezi halisi wa watu, mtetezi wa rasilimali na alikuwa tayari kufa yeye na kumtumbua yeyote yule na hata vinginevyo, hasa inapotokea au kubainika ni mtu mwenye kushirikiana na wapolaji, mabeberu na walanguzi wa rasilimali zetu!

Huyu ndiye anatakiwa awepo mtu wa aina yake tena siku za usoni katika nchi hii ya wajinga wajinga na wezi waliokubuhu
 
Ingawa Magufuli alikuwa na mapungufu kama binadamu mwingine yeyote, kusema kweli alikuwa Rais mwenye maono na uwezo mkubwa (kuliko watangulizi wake wote) wa kutafsri maono yake kwa vitendo.

Angemaliza mihula yake yote miwili, Tanzania angeifikisha mahali ambapo ingekuwa shambadarasa la Africa. Wito wa PLO Lumumba wa Magufulification of Africa (Kiswahili chake nadhani ni Umagufulishaji wa Africa) ungeitikiwa kwa kishindo na kasi kubwa!
 
Back
Top Bottom