Kumbukizi za watani wa Jadi,Simba vs Yanga

Kumbukizi za watani wa Jadi,Simba vs Yanga

chillo clan conscious

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
850
Reaction score
1,567
Tushukuru wawekezaji kwenye swala zima la mpira wa ligi yetu ya ndani hebu angalia hiki kiatu alichovaa PAPE NDAU no 25 mgongoni mchezaji wa simba ndicho kilicho tumika kwenye mechi ya Kariakoo Derby tar 26 mwezi wa 9 mwaka 2015.

Kumekuwa na kasumba sana kwenye mambo tofauti tofauti,pia tukija kwenye swala zima la kusakata boli kasumba hizo zipo.

Star wa Real madrid na Timu ya Taifa German mwenye uwezo wa kutosha Toni Kroos ana kiatu alikitumia kwenye mechi ya Kombe la dunia kilimpa matokeo chanya na kufanya kukihifadhi kiatu hiko na kukitumia baadhi ya mechi,vivyo hivyo Star wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ali Samata alie kipiga ligi tofauti tofauti barani afrika na ulaya na bado anaburuza boli kwenye ligi ya Ubelgiji nae niliwahi kusikia hivyo juu ya kiatu kinachompa matokeo chanya hukiamini na kukitunza vizuri kisha kuendelea kubunda boli na kiatu hiko hiko katika baadhi ya mechi tofauti.

Jee star huyo wa simba sc tuseme nae alikuwa anaendeleza kasumba hiyo ya kuvaa kiatu chakavu kiasi hiko kwa sababu mojawapo ya kuwa kilimpa matokea chanya,jee kwa uwekezaji uliofanyika kipindi hiki,Tanzania football federation {TFF} Na bodi ya ligi pamoja na kilabu husika jee wanaweza ruhusu mchezaji kutumia kiatu kama hiko?.

Shuka hapa,pia kama kuna kitu unachojua kufahamu na kuonekana ni kigeni kwako kwenye mechi za hawa watani elezea hapa,me nimeanza na hili la PAPE NDAW kijana wa ki Senegal
Screenshot_20221112_095011.jpg
 
Ni kumbukumbu nzuri sana
 

Attachments

  • 20221029_122128.jpg
    20221029_122128.jpg
    54 KB · Views: 4
Simba ni timu ya kimaskini sawa! Kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikiendeshwa kwa jasho la ukoo wa akina Dewji! Usikute hapo akina Dewji walikuwa hawajanunua viatu na jezi za wachezaji! Hivyo kila mchezaji akaamua kuvaa malapulapu yake.
 
Back
Top Bottom