Kumbukumbu enzi za sekondari

Kumbukumbu enzi za sekondari

Dr Ismaily

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2016
Posts
289
Reaction score
552
Tometoka mbali sana aiseee

Nakumbuka nilivyokuwa sekondari ilikuwa nikifanya kosa sichapwi kijinga jinga! Nilikuwa najitetea kivyovyote vile nisiguswe hahaahaaaa.

Walimu waligundua hiko kitu, daaah!! basi nikiitwatu staff sipewi chance ya kujitetea ni mikwaju kwanza halafu ndio kujitetea!!

Daaah wengine walienda mbali sana, eti nijiteteee kwa Kiingereza ilikuwa kimbembe!

Je! Wewe unakumbuka nini enzi hizo.
 
Nilikacha option ya french vipindi kadhaa, mwalimu wa somo hilo ambaye alikuwa sista wa kikatoliki alinishitaki kwenye cabinet ya school assessment nikaitwa kujitetea, mzee nilishindwa ikabidi nifutiliwe mbali kwenye option hiyo. Ila chapchapu nilijiunga na option nyingine niliyoipenda zaidi na masomo yaliendelea
 
Ebwanae, unaambiwa enzi hizo tulisoma na watoto wa vigogo wakubwa nchi hii sina ruhusa ya kuwataja vigogo hao ambao walikuwa wabunge, wakuu wa mikoa, wilaya, wafanyabiasha wenye asili ya asia na wengine wengi. Tofauti na siku hizi vigogo watoto wao hawasomi shule hizo
 
Enzi hizo mwenye kubamiza one ya saba mtamjua jina lake na shule anayotoka tanzania nzima tofauti na siku hizi hata upate A zote hakuna atakayetaka kukujua
 
Miaka hiyo ukifaulu kwenda sekondari wazazi watachinja mbuzi/kondoo kukupongeza kwani tayari ajira umeshapata na utaitoa familia kwenye lindi la ufukara na umasikini mkubwa, ukirudi nyumbani wakati wa likizo utachinjiwa kuku na wakati wa kuondoka kurudi shule utaondoka na take away ya kuku aliyebanikwa ukale huko safarini
 
Enzi hizo kulikuwa na mabasi na mabehewa maalumu ya kusafirisha wanafunzi kwenda na kurudi mikoani mwao na allowance wanapewa na serikali. Enzi hizo elimu ya sekondari ilikuwa ina thamani kubwa nchini, ajira nje nje hata wa la saba anapata
 
Nipo zangu form II, nimekaa nimetulia mara ghafla namuona namba moja wetu yani mikondo yote kiufupi yule dada alikuwa ana balaa kitaaluma halafu Mimi nkiwa na ufaulu wa wastani tu yani wale kumi bora na mimi nakuwemo.

Sasa tunapiga stori za hapa na pale ikabidi nifungue daftari langu angalau hata nipitishe macho lahaulaa KUNGUNI tena anatembea kwenye ukurasa yani pale peupe hahaha! Nkamuwahi chap chap kumuua huku sitaki kujua kama yule dada kaona au hajaona na hata sikutaka kujua kama ameona na nkakaa kimya tulii!
 
Back
Top Bottom