Kumbukumbu maridhawa kabisa

Kumbukumbu maridhawa kabisa

vibertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
2,474
Reaction score
4,726
Msimu wa 2019/2020 Yanga na Simba zilipata kuwakilisha nchi katika michuano ya Klabu Bingwa. Yanga walianzia nyumbani dhidi ya Township Rollers na huku Simba ilianzia ugenini dhidi ya UD Songo. Timu ya Yanga ilipocheza nyumbani hawakuweza kupata matokeo mazuri hivyo wakaruhusu goli na kufanya matokeo yawe sare ya goli moja kwa moja wakati watani wao Simba wakiwa ugenini wakapata sare ya bila bila.

Maneno, kejeli, na tambo zilikuwa nyingi sana za kuinanga timu ya Yanga kuwa wakienda ugenini watayaoga mengi mno maana wamepigiwa mpira mkubwa mno uwanja wa Mkapa, huku mashabiki wa Simba wakijikatia tiketi ya kwenda hatua inayofuata kwavile wameona wanakzi nyepesi mno.

Mpira wa ukakosa kanuni, Yanga ndiye aliyeanza kunusa hatua inayofuata kwa kushinda ugenini goli moja huku wakiwangoja wazee Ligi ya Mabingwa kesho yake watavuna kipi.

Ila kilichotokea ni kwamba waliokuwa na uhakika wa kufuzu hawakufuzu na waliokejeliwa hawana timu ya Klabu Bingwa ndiyo waliofuzu hatua inayofuata. Tubakishe akiba ya maneno, kuna dakika 90 za Sudani hivyo atakayechanga vyema karata ndiye atakayefuzu.
 
Back
Top Bottom