Kumbukumbu muhimu ya Wayne Rooney

Kumbukumbu muhimu ya Wayne Rooney

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
SINTOSAHAU:

Wayne Rooney anatukumbushia tukio la kupata kadi nyekundu dhidi ya Ureno katika kombe la Dunia 2006[emoji471]
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
[emoji860] “Mchezo ulikua unaendelea vizuri. Gafla, mapema kwenye kipindi cha pili, ikaja kadi nyekundu. Ilibidi niwe vile kwa refa ili anipe 'free kick'. Ilikua ni faulo ya wazi kabisa nilichezewa, beki wa zamani wa Chelsea Ricardo Carvalho alikua ananivuta na kunisukuma na Petit akaja akitokea upande mwingine.
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
“Elizondo hakufanya chochote na nilimkanyaga Carvalho kimya kimya mguuni kwa hasira — ni moja ya nyakati ambazo huwezi kufikiria sawasawa juu ya maamuzi unayoyafanya kama mchezaji. Kwa kitendo kile nilijua tu! ni kadi nyekundu.

Na kule kwenye vyumba vya kubadilishia nguo nilimalizia mchezo ule kwa kuutazama katika luninga [emoji342], huku nikiwaza: ‘kama tutashinda hii mechi, nitakua nimesimamishwa kucheza nusu fainali ya World Cup na hata fainali yenyewe, na kama tukipoteza basi kosa ni langu na taifa zima litanigeukia mimi’.

Nilikua na mawazo yenye maumivu na ya kustaajabu kuwai kuyapata katika maisha yangu ya soka.
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
“Nikiwa nafuatilia mchezo kutokea vyumba vya kubadilishia nguo, nilikua na simu yangu mkononi na nilikua napokea meseji nyingi sana kuhusu Ronaldo Kiukweli, Alipomkimbilia Elizondo (refa) kumshawishi nipewe kadi nyekundu ili nitoke, nilimsukuma kwa hasira . Wakati yale yanatokea, nilikua siamini kile alichokua anakifanya. Lakini, Nilipokaa peke yangu kule kwenye vyumba vya kubadilishia nguo nilipata nafasi ya kutuliza hasira na kufikiria kwa umakini juu ya tukio lile.
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
“Nilijiweka ndani ya viatu vya Ronaldo kwa dakika kadhaa, kisha nilijiuliza maswali yafuatayo. Je ningefanya kama alivyofanya yeye? Bila shaka ingekua hivyo. Je ningemzonga refa ili kuhakikisha naye anatolewa nje kwa kadi? Kama alistahili kadi nyekundu, na endapo kama kadi hiyo ingetusaidia nasi tushinde — Ndio! , hamna tena swali.

Pia nikakumbuka kitu: ‘Alafu, Nilijaribu kumsabaabishia apate kadi ya njano kipindi cha kwanza kwa kujirusha’. Na kwa ukalimu (#Ronaldo) alinikonyeza tu! wakati ule natoka nje ya uwanja kwa hasira akinikumbusha kuwa kuwa ni moja ya mchezo, ingawa sikuona hayo yote yakitokea, hivyo nikawa mpole. Baadae nilimfuata ili kuzungumza nae kwenye 'tunnel' kabla hajaingia chumba cha kubadilishia nguo. Niliona ni vizuri kuzungumza nae wakati mambo bado yakiwa bado madogo (kabla ya propaganda za media) na ilikua vyema kufanya hivyo tukiwa tunaonana uso kwa uso na si kwa njia ya simu. Ronaldo alinitazama kwa jicho la hisia ya kuomba msamaha, na wakati huo mawazo yangu kichwani yametawala juu ya ukaribu wetu ndani ya kikosi cha (Manchester United). Nikamwambia sina tatizo nawewe. Endelea kufurahia mashindano na kila lakheri.Tutaonana baada ya wiki chache — na uje tupambane ili tushinde ligi kuu (EPL) .” [emoji1022]

#KUMBUKUMBU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Rooney ndiye aliyemng'arisha Ronaldo pale Man U ila ni kama hilo huwa halionekani hivi!
Man u ile hakuna mchezaji aliyeng'arisha mwingine.kuanzia 1-11 .wote walikuwa na viwango vya juu na teamwork nzuri wakiongozwa na kocha mzuri.kila mchezaji alikuwa bora kwa nafasi yake.ronaldo alikuwa na uwezo wa kusukuma attack kuanzia nusu yao mpaka 18 ya wapinzani.free kick za kibabe.tuwe wakweli.nimeangalia 80% ya mechi za man u kipindi kile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Man u ile hakuna mchezaji aliyeng'arisha mwingine.kuanzia 1-11 .wote walikuwa na viwango vya juu na teamwork nzuri wakiongozwa na kocha mzuri.kila mchezaji alikuwa bora kwa nafasi yake.ronaldo alikuwa na uwezo wa kusukuma attack kuanzia nusu yao mpaka 18 ya wapinzani.free kick za kibabe.tuwe wakweli.nimeangalia 80% ya mechi za man u kipindi kile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Rooney alikuwa na work rate ya ajabu asee, alifanya kazi kama mtumwa au mnyama, alirudi kusaidia beki,alikaba kama kiungo, alishambulia kwa kaunta ataki za hatari. Sijasema Ronaldo hakuwa na kitu,alionyesha kipaji chake hasa ila kwa namna Man U walivyokuwa wanacheza Rooney aliplay part kubwa sana ktk ufanisi wa Ronaldo.
 
Rooney alikuwa na work rate ya ajabu asee, alifanya kazi kama mtumwa au mnyama, alirudi kusaidia beki,alikaba kama kiungo, alishambulia kwa kaunta ataki za hatari. Sijasema Ronaldo hakuwa na kitu,alionyesha kipaji chake hasa ila kwa namna Man U walivyokuwa wanacheza Rooney aliplay part kubwa sana ktk ufanisi wa Ronaldo.
Hakuna kitu kama hicho.hakukuwa na mchezaji ambae alikuwa favor kwa mwingine.kwenye kukaba timu nzima ilikaba ndio maana nakwambia utapigaje counter bila ronaldo.ndiye aliyekuwa na spidi kuliko wote.tuseme tu kwa pamoja walicheza vizuri.futa hiyo kauli ya rooney kumsaidia kumng'arisha ronaldo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu nzima ilifaidika na upambanaji wa rooney.but ronaldo alikuwa wa kipekee sana.kutwaa ile tuzo ya ballon kwa mchezaji wa EPL...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom