Kumbukumbu: The Diko Affair

KALABASH

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
498
Reaction score
210
Hili ni tukio lilitokea mwaka 1984 Uingereza. Lilikuwa jaribio la kumteka nyara na kumrudisha Nigeria Umaru Diko aliyekuwa waziri katika serikali ya Nigeria na ambaye alikuwa amekimbilia uhamishioni Uingereza.

Ubalozi wa Nigeria kwa kushirikiana na majasusi wa Israel walimteka nyara Umaru Diko na kumpakia kwenye box kubwa kwa madhumuni ya kumsafirisha kwa ndege ndani ya hilo sanduku kubwa likiwa na hadhi ya "Diplomatic Bag"

Kwa wale wanzangu wenye kuimanya lugha ya "Malkia" jaribu Google "THE DIKO AFFAIR." Ni kisa cha kusisimua sana.
 
Kalabash umenikumbusha mkuu! ilikuwa enzi za analogia gazeti moja tu lilipatikana hapa TZ lilikuwa na habari za kimataifa likiitwa Africa Now. Habari hii iliandikwa kwa kwa kina jinsi waisrael wa Mosad walivyosaidia kumteka OMARU DIKKO arudishwa Nigeria kujibu tuhuma za wizi wa mafuta. Aliwekwa ndani ya Sanduku pamoja na watekaji wake huku akidungwa Sindano ya usingizi ili asiamke. Mzigo ulikuwa labelled DIPLOMATIC BAGGAGE kuashiria hautakiwa kukaguliwa Airport. Ilikuwa story ya kusisimua laiti tungekuwa na TV enzi hiyo au Youtube tulione tukio!
 

Mkuu mbona unaandika uongo sikweli kuwa walifanikiwa, na ukweli ni kuwa mpango ulibuma ?
angalia kideo hapo juu!
 
Mkuu mbona unaandika uongo sikweli kuwa walifanikiwa, na ukweli ni kuwa mpango ulibuma ?
angalia kideo hapo juu!
Bila hata kuangalia video mkuu Gazeti liliandika kuwa hawakufanikiwa kumtorosha walikamatwa Airport huko Uingereza, huo mzigo ulipofunguliwa baada ya kutiliwa shaka japo ni wa Kibalozi, ndio walimkuta Diko ndani na Mosad aliekuwa ameshika sindano ya usingizi kumchoma Diko asiamke mpango wao ubumbulike! Aliokolewa na kurudishwa ukimbizini UK. Sijakusudia kuandika Uongo mpango wao ulibuma according to Africa Now magazine ya enzi hizo! wee ndio leo uaniona kwenye video?
 
Mkuu INAMAMBO. Kwanza nimefarijika kuona kuna mwana JF kama wewe ambaye una interest na mambo muhimu kama haya. Pili kukusaidia kumjibu huyu amayesema umeandika uongo. Nimuthibitishie kuwa mpango wa kumsafirisha Umaru Dikko kama cargo ulifeli na mimi mwenyewe nilikuwa huko wiki hiyo. Tukio liliripotiwa sana kwenye vyombo vya habari vya Uingereza.
 

Mkuu labda kiswahili changu kibaya, ila mimi nilielewa unamaanisha ulifanikiwa.
 
Mkuu labda kiswahili changu kibaya, ila mimi nilielewa unamaanisha ulifanikiwa.
Kibanga Ampiga Mkoloni! Jina lako linanikumbusha nyimbo za kitoto enzi ya TANU na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Basi mkuu ilikuwa ni Spelling mistake sikukusudia kuandika walifanikiwa kumrudisha Nigeria! Hawakufanikiwa. Pia tukio hilo nililisikia kwenye Radio Sauti ya Injili iliyokuwa inatangaza kutoka Adis Ababa nchini Ethiopia. Ilikuwa ikifika wakati wa taarifa ya Habari Baba alikuwa anatunyamazisha nyumba nzima ili apate kusikia matangazo.
 
Kwa kweli mimi huwa nina interest ya mambo mengi ya siasa, technology, space exploration, na mengineyo. Nilikua kipindi kile hakuna taarifa kama siku hizi ila nilikuwa napenda kusoma magazeti hadi ya nje ya nchi niliyokuwa nayaona kwa kaka yangu. Nakumbuka hata kipindi tz kulikuwa kuna shida ya nguo na viatu, Africa Now wakatoa makala kuhusu Tz wakamuonesha Paulo Sozigwa amevaa soksi zilizochanika! Nilipenda kusoma habari za KGB,MOSAD,FBI zilzokuwa zimeandikwa kwenye riwaya ya Carlos the Jackal,Escape from Sorbibo na nyinginezo. Waisrael kuvamia Entebe Airport na kuwatoa mateka wao na story nyinginezo za enzi hizo za Cold War. MOSAD niliwapenda ili niliumia mpango wao huo wa kumsafirisha Dikko kubuma.
 
Very interesting. Keep up the spirit. Topic za aina hii hutawakuta akina Barbarosa,Jingalao msemakweli,wakudadavua et al ambao wamejikita zaidi kwenye ccm/Chadema bashing and vice versa na hiyo inaligeuza JF kuwa jukwaa la mediocrity
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…