Kumbukumbu : Uso kwa Uso na Simba.

Kumbukumbu : Uso kwa Uso na Simba.

Mleta uzi cjui ni shabiki wa yanga..cjapenda kabisa jinz simba alivyouwawa[emoji16] [emoji16] [emoji16]
Hahahaha, hapana Mkuu. Mimi ni Simba damu. Hapo ni jinsi nilivyomshughulikia mnyama huyu wa mwituni.
 
IMENIFANYA NIKUMBUKE HII
Mwalimu: *Alex, simba akianza kukufukuza utafanya nini?*
Alex: *nitapanda juu ya mti.*
Mwalimu: *je na simba nae akipanda juu ya mti?*
Alex: *nitakimbilia mtoni niogelee.*
Mwalimu: *je simba nae akikufuata mtoni?*
Alex: *mwalimu uko upande wangu au wa simba? Maana* *sikuelewi kabisa, kila ninavyojaribu kumkwepa* *simba we unamwelekeza niliko, kama hunipendi sema tu.*
 
Hahahaha, hapaja Mkuu. Mimi ni Simba damu. Hapo ni jinsi nilivyomshughulikia mnyama huyu wa mwituni.
Hahahaa ongera mkuu nmekuelewa ila nlikua najaribu kukutoa porini baada ya shughuli nzito
 
Kumbe kaka yangu una kipaji kikubwa namna hii cha simulizi?
Nakosa namna ya kukuelezea nilivyokuwa na hofu wakati nasoma hii kumbukumbu yako mujarab.

Nimetetemeka haswaaaaa. Uwiiiiiiiiii bora tu sikuwa mwanaume maana naona ningeliwa tu.
Siwezi kabisa hata kumsogelea Simba nini kupambana nae?
Sehemu ya 3 kidogo initoe roho!
 
Shemeji kwa ujasiri huu na experience hii inafaa sana nikupe sanduku la posta la wale jamaa zetu wale!!

What an experience... Haya ndio matukio ukizeeka wajukuu hawabanduki kibarazani kwako kusika ujana wako ulikuwaje!!
 
Dada, inatisha sana. Heri yako wewe unasoma kama simulizi. Mimi niitekeleza kabisa. Hofu niliyokuwa nayo iliniisha punde tu baada ya Simba Kumrukia mwenzangu.

Simba ni mnyama mkali sana. Katika kupiga story, nilihadithiwa kisa kimoja. Simba aliua karibia watu watatu kwenye tukio moja. Wote waliliwa lakini hiyo haiwakurudisha Morani nyuma, walihakikisha wanafanikisha kile walichokilenga.

Nilipokuwa naikumbuka kisa hiki cha Simba kutafuna watu watatu, niliona kabisa na mimi ni mmoja kati ya wanaoenda kufanywa kitoweo. Nilijaa hofu lakini hofu hiyo haikunirudisha nyuma.

Songa mbele, Okoa Jamii yako. Nilisonga mbele.

Acha kabisa. Macho ya simba pamoja na zile nywele zake zinatisha dada. Huwa nikikumbuka nasisimka sana.
 
Uwiiiiiiiiii ningekuwepo jamani naona ningeliwa tu! Maana ningetupa ngao na kukimbia!
Hongera sana,wewe ni zaidi ya shujaa [emoji122] [emoji122]
 
SEHEMU YA 3
Wakati kila mmoja akiendelea kujitafakari kurusha Mkuki awe wa Kwanza, ghafla bin Haraka Simba alimrukia mwenzangu. Bahati nzuri au mbaya alikuwa na ngao. Lakini, kuna utaratibu pia. Ukiona Simba anakurukia Sogea hatua moja mbele au rudi hatua moja nyuma. Hii inakusaidia ili kum-push au kutokukuangukia kama zigo. Hii ni kumkosesha Simba balance. Ile incident sitaki kuikumbuka kabisa wakuu. Jamaa kwa ujasiri kabisa alipoona Simba anaruka, na yeye akapiga hatua moja mbele hivyo simba akasukumwa nyuma kidogo.

Sijui nilipata wapi ujasiri. Wakati Simba anaruka, nami ndipo niliporusha Mkuki wangu kwa nguvu ya ajabu. Nilijua hapa nimekwisha. Nilirusha Mkuki nikimkusudia shingoni lakini bahati mbaya kutokana na kujirusha kwake ilimpata tumboni. Ilimuingia haswa. Wenzangu nao walifatia. Simba alipigwa mikuki yote Sita.

Simba ana nguvu bhanah! Pamoja mikuki yote lakini bado alikuwa na nguvu. Alinyanyuka tena kumfata mwenzetu. Tukachomoa sime zetu zilizokuwa ndani ya ngao na kuanza kumkatakata maeneo mbalimbali. Inashauriwa sana kumkata miguu kwanza hasa kwenye catilages zinazounganisha unyayo (kwato) na mguu ili kumkosesha nguvu ya kutembea na kunyanyuka.

Simba alipomfata mwenzetu aligongwa na ngao na kusukumwa chini, sasa mkuki mmoja uligota chini kabisa. Simba alishindwa kunyanyuka. Ndipo akaanza kukatwa karibia kila pembe huku akinguruma kwa hasira na mhemuko.

Tulimuweza Simba. Hakuwa amekata roho lakini alipata maumivu yasiyomwezesha kumjeruhi mtu. Ningelikuwa na smart phone miaka hiyo, ningeliweza kuchukua selfie kabisa kabla hajalikata roho.

Nitaendelea.
Mngemng`oa meno aisee pia mngemkata kucha
 
Shemeji kwa ujasiri huu na experience hii inafaa sana nikupe sanduku la posta la wale jamaa zetu wale!!

What an experience... Haya ndio matukio ukizeeka wajukuu hawabanduki kibarazani kwako kusika ujana wako ulikuwaje!!
Hahaha, shemeji ninyi si mna ule utaratibu wenu? One Brings One.

Sasa nichukue mimi sasa nikawe mmoja wenu. Hahahaha. Au umeshampata wa kumchukua? Hahaha, ngoja nijidai sitaki kwa sababu ukionyesha tu interest then umeshadisqualify.

Anyway,hizi visa zinaacha sana Kumbukumbu kubwa sana katika maisha yetu. Wajukuu wangelifurahia sana. Bahati mbaya sana, kizazi chetu cha Digitali, hawana muda wa kukaa kibarazani kusikiliza matukio. Wao wapo busy na kideo pamoja na michezo yao ya komputa.
Lakini tutasonga tu mbele.
 
Duh, hongera Sana mkuu, kweli wewe ndie haswa mwanaume Wa mkoani, sio Hawa wasukuma wanaojisifia kula sato.
 
Hofu tupu Mkuu. Inaogopesha sana. Acha tu Mkuu. Yakheri ufumaniwe kuliko kumfata Simba live live ukiwa na nia ya Kumuua. Yale macho yake yakikuangalia unaweza kudondoka kwa hofu.
Mwenzako ata huyo simba nimemuonea kwenye maonesho!!! Alikua ndani ya uzio ila alipounguruma nilitimua mbio hizo... Usain Bolt haingii ndani.
Sasa ningekutana nae ana kwa ana nadhanu matobo yote kwenye mwili wangu yangekua kwenye work mode!!!
 
nilisikiaga kwamba ukikutana nae usikimbie una tulia kama hujamuona ni kwel
Hahaha! Juzi kati nilipita kijiwe fulani wakaka wakawa wanajadili hili jambo... Yaani unaniambia kabisaaaa utakumbuka nini uliambiwa mda huo??? Hapo huwezi tumia akili ata kidogo... Adrenaline ndo inakupa muongozo, usimame au ukimbie!

Kjna siku tuliku darasani na usista duu wote kuna mtu akapiga kelele kengeee!!! Daah, sekunde moja mbona nyingi mno!!! Nilijikuta nipo juu kabisa ya dirisha nimejikunyata. Sikumbuki hadi leo nilipandaje kule juu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
IMENIFANYA NIKUMBUKE HII
Mwalimu: *Alex, simba akianza kukufukuza utafanya nini?*
Alex: *nitapanda juu ya mti.*
Mwalimu: *je na simba nae akipanda juu ya mti?*
Alex: *nitakimbilia mtoni niogelee.*
Mwalimu: *je simba nae akikufuata mtoni?*
Alex: *mwalimu uko upande wangu au wa simba? Maana* *sikuelewi kabisa, kila ninavyojaribu kumkwepa* *simba we unamwelekeza niliko, kama hunipendi sema tu.*
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kumbe kaka yangu una kipaji kikubwa namna hii cha simulizi?
Nakosa namna ya kukuelezea nilivyokuwa na hofu wakati nasoma hii kumbukumbu yako mujarab.

Nimetetemeka haswaaaaa. Uwiiiiiiiiii bora tu sikuwa mwanaume maana naona ningeliwa tu.
Siwezi kabisa hata kumsogelea Simba nini kupambana nae?
Sehemu ya 3 kidogo initoe roho!
Kuna watu jasiri kweli!!!
 
Back
Top Bottom