Kumbukumbu ya Halila Tongolanga

Kumbukumbu ya Halila Tongolanga

Ntinje

Senior Member
Joined
Feb 2, 2019
Posts
127
Reaction score
113
Juni 5-7/2017 majonzi makubwa yalitawala kwa kuondokewa na mwanamziki ambaye hakika alitoa mchango mkubwa katika sanaa.

Huyu ni Halila Tongolanga. Nadhani wengi wetu mtakumbuka kibao chake ambacho kilivuma sana "Kila mtu ave na kwao".

Hakika kibao hicho hata leo kikipigwa wengi wetu hutulia na kupata burudani yake. Wimbo ule una ujumbe kuntu ambao hasa kizazi cha leo ni vyema wakaupata ujumbe ule.

.Mungu azidi kumupumzisha Halila Tongolanga mahali pema peponi. Daima tutaendelea kumkumbuka ndugu yetu huyu.
 
Ninakushukuru mkuu kwa kutukumbusha hili na kutunza hizi rekodi muhimu za watanzania wenzetu walioitangaza nchi yetu katika fani hii ya muziki ,ninategemea mwana JF mwingine atakuja na kumbukumbu kuhusiana na wale wote waliotangulia mbele ya haki,maana walituelimisha na kutuburudisha mfano Mbaraka M.;Shaaban Dede;Maalim Ngurumo,TX,na wapiga magitaa maarufu kipindi hicho kama Mulenga etc etc,yeah tumeishi maisha yetu.
 
Mwenye wimbo wake wa Sanura afanye kuu-appload humu
Kweli Duniani tunapita!
 
Field Marshal Halila Tongolanga mwanalichewe wa kukaya kumchichiraa kooo
 
Mr ebo kuna mahali anamtaja huyu jamaa kwenye wimbo wa machinga anasema halila tongolanga langa ngoma ya tanga halafu anaenndelea kamongo umemfanya nini pigi...........
 
Back
Top Bottom