Kumbukumbu ya kifo cha Munga Tehenan

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Posts
268
Reaction score
124

Kwa wadau wote wa FAJI na waliokuwa wapenzi wa Gazeti la JITAMBUE. Mke wa Hayati Munga Tehenan na wana FAJI, watafanya kumbukumbu ya kifo cha MUNGA TEHENAN. Shughuli hiyo itafanyika katika msikiti wa Kimara na sadaka ya chakula itatolewa katika ofisi za Faji Kimara Rombo.

Bajeti kwa wageni wanaotarajiwa kufikia idadi ya 120 ni Tsh. 631,000. Tunahitaji michango ya wadau kwa hali na mali ili kufanikisha shughuli hiyo. Mtu yeyote mwenye nia ya kuchangia, tunaomba atume mchango kwa M-PESA 0764 461366 au awasiliane na Dr. John wa Tabata Dispensary kwa namba hii 0713 250701.

Atakayesoma taarifa hii amjulishe mwenzie……………
 
tunashukuru sana kwa taarifa, nipo Mwanza ila nitatuma mchango wangu.
 
tunashukuru sana kwa taarifa, nipo Mwanza ila nitatuma mchango wangu.
Nakushukuru sana kwa mwitikio wako na kuunga mkono shughuli hii...............Tutashukuru pia iwapo utawafahamisha na wengine
 
Jambo la maana sana!

Nina magazeti ya Mshauri na Jitambue ambayo nimeyatunza na huwa nayapitia mara kwa mara.. Yanaelimisha sana juu ya kuona mambo kwa macho tofauti..

Kifupi naendelea kumpongeza sana marehemu.. Alichangia kubadili maisha ya watu wengi sana!
 
Alikuwa mweredi wa kweli na alichangia watu wengi kujitambua,..anyway r.i.p Munga
 
Nipo hapa mjini na inshallah ntachaangia'huyu bwana alichangia kiasi kikubwa sana kunibadili maisha yangu'mpaka sasa naamini kwa tz hajawahi kutokea mtambuzi kama Marehem Munga Said Tehenan'mungu amlaze mahali pema,
 
Kuna wakati nadhani kuna haja ya kufufua Majarida yale..
 
Kuna wakati nadhani kuna haja ya kufufua Majarida yale..
Nilifanya nae kazi katika hayo magazeti yao...
Nakumbuka kampuni iliitwa TK media. Ni muunganiko wa majina mawili...huyo K ndie aliebaki na amana zote...ukilihitaji muone huyo aliebaki.
Mungu amweke Marhuum Munga panapostahiki. Aamiin.
 
Ah kumbe jamaa ni marehemu mi sikuwa taarifa kabisa, alifariki lini wakuu?
 
Nilifanya nae kazi katika hayo magazeti yao...
Nakumbuka kampuni iliitwa TK media. Ni muunganiko wa majina mawili...huyo K ndie aliebaki na amana zote...ukilihitaji muone huyo aliebaki.
Mungu amweke Marhuum Munga panapostahiki. Aamiin.
Mkuu habari za siku....................
Naomba tuwasiliane kuna habari njema kuhusu gazeti hilo la JITAMBUE..............................
 
Mkuu habari za siku....................
Naomba tuwasiliane kuna habari njema kuhusu gazeti hilo la JITAMBUE..............................

Nilifahamu gazeti hili baada ya kuokota kipande cha gazeti hilo jalalani, wakati huo nilikuwa nimefukuzwa chuo fulani cha uuguzi kwa kosa la kijinga sana. Sikuwa na mbele wala nyuma...hebu jiulize 'mtoto wa mtaani' anayefadhiliwa na NGO kusoma akifukuzwa shule marejeo ni wapi?...mtaani huwezi kwenda tena...

Ni jitambue iliyonionyesha njia, ninalo furushi kubwa la nakala za magazeti hayo, sijuhi kama kitakuja kupatikana chanzo cha FIKRA HURU hapa Tanzania kama Jitambue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…