Shukran kwa kunisahihisha mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukran kwa kunisahihisha mkuu
Mimi ningeomba wadau wwnye nakala za huyu bwana ama kiwanda alichokuwa anachapa magazeti tuzikusanye tufanye gharama ya kuzichapisha hapa jf kama special thread.amini nawaambia makala zile zitawasaidia wengi
Mkuu nimekuelewa Sana.... Mimi Ni Mmoja wa Watu waliopenda Kazi zenu.. Nitakutafuta Binafsi ili nipate Angalau vitabu vyenuNaweza kushangaa leo nikisikia maneno kama yako................. Labda kwa wale wasiojua, ukweli ni kwamba mimi ni mmoja wa waliokuwa waandishi wa gazeti lile na kusema kweli katika jambo ambalo lilimsumbua kichwa sana Hayati Munga mpaka anaenda kaburini ni kitendo cha gazeti lile kukosa soko la kuridhisha. Ingawa wengi leo wanalisifu sana hapa, lakini lile gazeti lilikuwa haliuzi ukilinganisha na magazeti ya udaku. Ilifikia mahali hata lilikuwa halirudishi hela iliyotumika kulichapa....! Kama mnakumbuka TK Media ilikuwa na magazeti mawili, Mshauri Wako ambalo lilikuwa likiandika habari za wanawake zaidi na hilo la Jitambue ambalo lilikuwa linaandika habari mbalimbali za kisaikolojia na utambuzi kwa ujumla. Ilibidi tuyaunganishe yote mawili ili kampuni imudu kujiendesha maana ilifikia mahali magazeti hayo yanaendeshwa kwa fedha za mifukoni. Leo hii nikisikia watu wanadai Gazeti la Jitambue lirudi.............inanishangaza kwa kweli.
Kuna ushahidi hapa hapa JF. Nimekuwa nikirejea baadhi ya makala za Jitambue hapa, lakini watu wanadai ni ndefu na hawawezi kusoma...............Awali nilitaka kuacha, lakini hao baadhi wanaosoma wamekuwa wakinipa moyo.
Mhusika anayeshikilia Gazeti hilo anataka kuliuza lakini kila mtu anaogopa kulinunua kwa sababu falsafa ya gazeti hilo haiuzi, nani angependa kuhatarisha mtaji wake? Inahitaji utambuzi wa hali ya juu kuliendesha gazeti la Jitambue la sivyo hakuna atakaye weza.
Hayati Munga aliwahi kuniambia kwamba anashindwa kuelewa kwa nini Gazeti la Jitambue haliuzi ingawa lina maarifa mazuri yanayoelimisha. Aliwahi kuandika katika mojawapo ya tahariri zake katika gazeti hilo kwamba Watanzania ni wavivu wa kusoma na hasa vitabu au magazeti yaliyosheheni maarifa na elimu. Wengi tunapenda kusoma habari za udaku, kitu ambacho yeye haikuwa ni falsafa yake. Ilibidi tuanzishe mradi wa Vitabu ili kama vikiuza basi vichangie kuliendesha gazeti hilo, lakini pia hilo lilishindikana.............Vitabu navyo havikuuza kama ilivyotarajiwa.
Kuna watu wenye ujuzi wa aina nyingi humu na wana uwezo mkubwa wa kuelimisha wengine, lakini wadau wengi humu hawako tayari kupokea maarifa hayo, sana sana utawasikia .... oooh ni ndefu sana... au Chapa Gazeti..........na maneno mengi ya kukatisha tamaa. kama mtu huna muda wa kusoma basi kaa kimya au print ukasome nyumbani.
Siamini kama Gazeti hilo litauza hata akipatikana mtu wa kuliendesha...................................