Kumbukumbu ya kifo cha Munga Tehenan


Sasa kuna mpango gani wa kufufua gazeti mkuu??
Nakumbuka lilikuwa moto mno jamani!! Hadithi ile ya Timo....aliyekuwa anashughulikiwa na jamaa wa usalama......

Kwa kweli ntalikumbuka sana gazeti lile?
 
Kumbe Munga Tehnan alikuwa na dini?? Nakumbuka alinifundisha kuwa hakuna Mungu mwingine mbinguni na duniani isipokuwa mimi mwenyewe
Na wewe ulimuelewa vibaya...........alikuwa anamaanisha kwamba hatima yako iko mikononi mwako................
 
I wish ningekuwa hapo nihudhurie hii Misa itakuwa lini?
Alinisaidia sana huyu ndugu Tehenan

mwenyezi mungu aiweke mahali pema peponi roho yake


Amen.
 
Alisaidia pia kuyabadili maisha yangu! Daima nitamkumbuka, tukijaaliwa lazima tumchangie ili kufanikisha shughuli hiyo, shime ndugu zangu!
 
Munga was a genious..namkumbuka sana huyu jamaa,moja ya makala yake ambayo sitoisahau ni "UKITAKA KUFA MAPEMA FANYA HAYA" baadhi aliyolist ni......,,nitajitahidi nifike,ila Mr.Mtambuzi msife moyo,tujitahidi lirudi hili gazeti,tuokoe hiki kizazi
 

wengi wakianguka wanashindwa kunyanyuka..hongera kwa kujipangusa na kusonga mbele baada ya kuanguka.
 
nakumbuka makala yake moja ilisema kupenda sana ni ukichaa sitakaa niisahau ile makala ilinibadilisha sana
 
Npo mbali sijui nichange vipi..jamaa alinibadilishA sana mtazamo wa maisha
 
Mimi ningeomba wadau wwnye nakala za huyu bwana ama kiwanda alichokuwa anachapa magazeti tuzikusanye tufanye gharama ya kuzichapisha hapa jf kama special thread.amini nawaambia makala zile zitawasaidia wengi

Hata mie natamani hicho kitu kwani sikuwahi kutambua hilo zaidi nashukuru nilijatambua kupitia makala kwenye blogu ya jamaa anaitwa Ndesanjo Macha nayo siku hizi inasuasua sio kama kipindi kile makala motomoto zinaamsha fikra na kukupa uhuru wa kujitambua. MKUU Inkoskaz fanya jambo hapa kushirikiana na mods tuweze kupata nakala za marehemu Munga.
Mbarikiwe sana na mungu ampe wepesi marehemu Munga.
 
Tunahitaji reprinting ya zile nakala zote na pesa itakayopatikana imsaidie mama mjane
 
Mtambuzi kama unazo nakala za jitambue nazihitaji sana,nilikuwa na nakala za jitambue na mshauri wako nyingi sana karibia miaka 2 nilizikusanya,kuna mdogo wangu akili ya kiteja akaja kuzipitia akaenda kuuza dukani kwa kg yaani mpaka leo nasikitika sana,maana makala zake zilikuwa hazipitwi na wakati,Niliwahi kuhudhuria pale rombo mara kadhaa kwenye darasa zake pia,
 
mnatusaidieje sasa kwa sisi ambao hatumfahamu, alikuwa na mambo mazuri
 
Mkuu Mtambuzi hongera kwa kuwa mmoja wa watu waliofanya kazi kwa karibu na Bw. Munga. Swali langu ina maana nyie mliofanya nae kazi kwa karibu na pia wanafunzi wake wote hadi leo mmeshindwa "kujitambua" na kumuenzi huyu marehemu kwa kutumia kile mlichokuwa mnafundisha wengine au kufundishwa nae? Kwamba mlipoanguka na gazeti la Jitambue mkononi mmekubali kubaki hapo hapo badala ya kunyanyuka tena na kuanza mwendo upya hata kama ni kwa kutumia staili nyingine. Kama kuna staili nyingine mnayotumia kuwafanya watu wajitambue kwa kufuata falsafa ya Munga basi inaonekana hiyo staili haijulikani kwa wengi. Ila sina maana mbaya.
 
Mzee Mtambuzi yuko hai kweli kama kumbukumbu zangu ziko sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…