Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Ilikuwa mwaka 1927 ndipo chama cha AA kiliundwa kwa msaada wa Gavana wa Kiingereza nchini Tanganyika Sir Roland Davidl Cameron na Dr Agrey raia wa Ghana mwenye mtaa Kariakoo ya leo, huyu Mghana alikuwa mshauri wa kisheria na kimuundo tu, kikawa kinafanyia shughuli zake nyumbani kwa Rais wa kwanza wa AA bwana Cecil Matola kutoka kabila la wayao, na miaka mitatu baadae, yaani 1930 ndipo wakapata jengo toka kwa Gavana Donald Cameron, hapo ndipo picha hii ilipigwa,

Mwaka 1933 Cecil Matola alifariki dunia, na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa AA Bwana Kleist Sykies (ambae baba yake mzee Platanta alikuwa ni muhamiaji haramu toka Afrika Kusini aliyefika Tanga na kuanzisha makazi huko baada ya kuwa mateka wa wajerumani vita ya kwanza ya dunia), mpaka mwaka 1948 chama kilipobadilishwa jina nakuwa TAA chini ya Rais wake Daktari Vedasto Kyaruzi (Mhaya),

Hapo Rais wake wa kwanza wa TAA akawa Daktari Vedasto Kyaruzi, na katibu akawa Abdulwahid Klest Sykies, miaka miwili baadae, Dr Kyaruzi alihamishiwa Kingolwila hivyo nafasi ya urais wa AA ikakaimiwa na Abdulwahid Kleist Sykies hadi ilipofika uchaguzi wa 1953 ambao Julius Nyerere alimshinda Abdulwahid Kleist Sykies kwakishindo na kuwa Rais wa TAA, Mwaka mmoja baadae Julius Nyerere alibadilisha jina na mrengo wa TAA nakuwa TANU ya kupigania uhuru kutoka chama cha kuratibu shughuli za starehe za weusi (chama cha walevi)

.........Yote kwa urefu yamo katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,

FB_IMG_1500302327031.jpg

FB_IMG_1500311302294.jpg
 
M
Wewe Yericko sasa unataka kumtowa nyoka pangoni, yani waanzilishi ni makafir watupu na wazee wa Mohammed Said yupo mmoja tu mzee Sykes?

Hapo siondoki nawahi siti ya mbele kabisa namsubili mzee Mohammed Said, hapa patamu leo.

Mohamed Said ni mwalimu wangu, tatizo mi mdini tu
 
Maandiko yako kama haya wengi tunapenda. Yanajenga sana. Ila ya siasa achana nayo kamanda.
 
Nao waanzilishi 17 ambao 3 ni wakristo na the rest ni waislam vipi? Ebu dadavua nao ili tujue.
Assalam alleykhum;
Tumsifu Yesu Kristo;
 
Rais wa kwanza wa AA Bibi Sesilia Matola kutoka kabila la wayao,

Mwaka 1933 Sesilia Matola alifariki dunia, na
Mkuu Yeriko, kwanza hongera sana kuandika kitabu, maana kuandika kitabu sio mchezo haswa kwa kuuzingatia utamaduni wa Watanzania na moyo wa kujisomea vitabu, yataka moyo sana kuandika kitabu ambacho hakitaingizwa kwenye ithibati yoyote!

Umefanya kazi nzuri ila kwanza naomba uthibitisho, ni Bibi Sesilia Matola au ni Bw. Cecil Matola?. Nani aliyekudanganya Cecil Matola ni Bibi na jina lake ni Sesilia?!. Kama hiki ndicho ulichoandika kwenye kitabu chako hadi kutoa Hard Copy!, I wonder how many factual errors zitakuwepo kwenye the rest of kitabu hicho?

Kama jambo dogo kama hili umeshidwa to get the facts right, what about the credibility of the rest?

Paskali

Ref:
A Modern History of Tanganyika
Google Books › books
John Iliffe - 1979 - ‎History
Its first president was Mwalimu Cecil Matola, the aristocratic Yao teacher educated at Kiungani who ...
Kleist Sykes - Wikipedia
Wikipedia, the free encyclopedia › wiki › Kleist...
Kleist Sykes (1894–1949) was a Tanganyikan political activist. ... along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi.
Mohamed Said: CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YABOMOA ...
www.mohammedsaid.com › 2015/02 › c...
14 Feb 2015 - Historia ya CCM inaanza mwaka 1929 katika nyumba ya Cecil Matola (sasa mali ya marehemu ...
A Place in the World: New Local Historiographies from Africa and ...
Google Books › books
Axel Harneit-Sievers - 2002 - ‎History
Matola, Cecil 1929. Cecil Matola Anatuhadithi Habari za Maisha Yake [ Cecil Matola tells us from his life]. Illambo Leo ...
Generations Past: Youth in East African History
Google Books › books
Andrew Burton, ‎Andrew Ross Burton, ‎Helene Charton-Bigot - 2010 - ‎History
March 1930], Kisarawe District Book, TNA). 16. Cecil Matola to Chief Secretary (CS), 22 April 1930, TNA 61/ 207/I/12.
Nyerere: The Early Years - Ukurasa 245 - Matokeo ya Google Books
Google Books › books
Thomas Molony - 2014 - ‎Biography & Autobiography
... Ujuzi Educational Publishers, 2006, pp.47–8 on the role of Martin Kayamba, Cecil Matola, Ramadhani Ali and Kleist ...
Miaka 48 bado tunaficha ukweli, kwa nini? – Raia Mwema
www.raiamwema.co.tz › miaka-48-bado-...
19 Mei 2012 - AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes ...
 
Good history to start with, lakini Yericko wewe si nasikia huwa unaandika vitabu? Kama ndivyo, mbona una punctuation mbovu kiasi hiki?

In addition, for your own benefit, hukutakiwa kuweka link kavu ya Amazon bali link ya hicho kitabu! Na hicho kitabu chenyewe binafsi nimeshindwa kukiona kupitia hiyo Amazon main link!
 
Mkuu Yeriko, kwanza hongera sana kuandika kitabu, maana kuandika kitabu sio mchezo haswa kwa kuuzingatia utamaduni wa Watanzania na moyo wa kujisomea vitabu, yataka moyo sana kuandika kitabu ambacho hakitaingizwa kwenye ithibati yoyote!.

Umefanya kazi nzuri ila kwanza naomba uthibitisho, ni Bibi Sesilia Matola au ni Bw. Cecil Matola?. Nani aliyekudanganya Cecil Matola ni Bibi na jina lake ni Sesilia?!. Kama hiki ndicho ulichoandika kwenye kitabu chako hadi kutoa Hard Copy!, I wonder how many factual errors zitakuwepo kwenye the rest of kitabu hicho?!.

Kama jambo dogo kama hili umeshidwa to get the facts right, what about the credibility of the rest?.

Mkuu Pascal Mayalla

Kwanza nisamehe sana kwa kuchanganya baadhi ya dondoo katika andiko langu, nakiri nimejichanganya tu na tayari nimesharekebisha hasa jina la Cecil Matola,

Naomba nikujibu kwenye hizo baadhi rejea ulizoweka sawa na nilivyomjibu Mzee wangu Mohamed Said katika barza letu huko viunga vingine...

Nanukuu:

"Unasema tufanye rejea kwakusoma wapi???

Sasa ngoja tuwasaidie wasomajo kwamba hizo zako ni ngano za masika,

Kwasababu kuu hizi,

John Iliffe alikuwa ni mwalimu wa Daisy Sykes mtoto wa Abdul Sykes, mjukuu wa Kleist Sykes,

Hivyo John huyu kitabu chake kwa sehemu kubwa ni simulizi za familia ya akina Sykes yani familia zilezile zenye chuki na Mwalimu baada ya visa vile nilivyowasimulia kule mwanzo ambavyo vilizaa uhaini na kuwekwa kizuizini kwa mabwana hao wa ukombozi, hivyo msingi wa kitabu cha Modern Tanzanians ni chuki ile ile iliyomuandama Mohamed Said Salum leo.

Pili unasema tusome kitabu cha Kleist Sykes The Townsman kilichoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes yuleule na mnyororo ni ule ule,

Na mwisho unasema tukusome wewe, tyuuuuupu wacha niteme mate kwanza, wewe ambaye umejaza chuki kifuani kwako mpaka kitabuni? Unayepinga waziwazi kwamba Julius Nyerere hakuasisi Tanu kisha unakubaliana kuwa kadi namba moja ni ya Julius Nyerere? Kitabu chako nimekisomo chote sio niekewe bali nikupinge kwa jambo ninalolijua... Kwaujumla umeeneza chuki tu,

Hoja nyingine ni hii ya AA unaipotosha bila sababu za msingi, mimi nimeeleza kuwa iliasisiwa 1927 nyumbani kwa Rais wake Mwalimu Cesil Matola na vikao vyote vya mwanzo vikifanyika kwake, lakini wewe hapo unanilisha maneno kwamba nimesema iliasisiwa Lumumba(Stanley). Huo ni uongo wa kutupwa..."
 
Mkuu Yeriko, kwanza hongera sana kuandika kitabu, maana kuandika kitabu sio mchezo haswa kwa kuuzingatia utamaduni wa Watanzania na moyo wa kujisomea vitabu, yataka moyo sana kuandika kitabu ambacho hakitaingizwa kwenye ithibati yoyote!.

Umefanya kazi nzuri ila kwanza naomba uthibitisho, ni Bibi Sesilia Matola au ni Bw. Cecil Matola?. Nani aliyekudanganya Cecil Matola ni Bibi na jina lake ni Sesilia?!. Kama hiki ndicho ulichoandika kwenye kitabu chako hadi kutoa Hard Copy!, I wonder how many factual errors zitakuwepo kwenye the rest of kitabu hicho?!.

Kama jambo dogo kama hili umeshidwa to get the facts right, what about the credibility of the rest?.

Paskali

Ref:
A Modern History of Tanganyika
Google Books › books
John Iliffe - 1979 - ‎History
Its first president was Mwalimu Cecil Matola, the aristocratic Yao teacher educated at Kiungani who ...
Kleist Sykes - Wikipedia
Wikipedia, the free encyclopedia › wiki › Kleist...
Kleist Sykes (1894–1949) was a Tanganyikan political activist. ... along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi.
Mohamed Said: CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YABOMOA ...
www.mohammedsaid.com › 2015/02 › c...
14 Feb 2015 - Historia ya CCM inaanza mwaka 1929 katika nyumba ya Cecil Matola (sasa mali ya marehemu ...
A Place in the World: New Local Historiographies from Africa and ...
Google Books › books
Axel Harneit-Sievers - 2002 - ‎History
Matola, Cecil 1929. Cecil Matola Anatuhadithi Habari za Maisha Yake [ Cecil Matola tells us from his life]. Illambo Leo ...
Generations Past: Youth in East African History
Google Books › books
Andrew Burton, ‎Andrew Ross Burton, ‎Helene Charton-Bigot - 2010 - ‎History
March 1930], Kisarawe District Book, TNA). 16. Cecil Matola to Chief Secretary (CS), 22 April 1930, TNA 61/ 207/I/12.
Nyerere: The Early Years - Ukurasa 245 - Matokeo ya Google Books
Google Books › books
Thomas Molony - 2014 - ‎Biography & Autobiography
... Ujuzi Educational Publishers, 2006, pp.47–8 on the role of Martin Kayamba, Cecil Matola, Ramadhani Ali and Kleist ...
Miaka 48 bado tunaficha ukweli, kwa nini? – Raia Mwema
www.raiamwema.co.tz › miaka-48-bado-...
19 Mei 2012 - AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes ...
Msanii tu huyu jamaa, Pascal Mayalla
 
Good history to start with, lakini Yericko wewe si nasikia huwa unaandika vitabu? Kama ndivyo, mbona una punctuation mbovu kiasi hiki?

In addition, for your own benefit, hukutakiwa kuweka link kavu ya Amazon bali link ya hicho kitabu! Na hicho kitabu chenyewe binafsi nimeshindwa kukiona kupitia hiyo Amazon main link!
Mkuu nisamehe nimeitoa ili mjadala wa kumbukumbu uende vizuri
 
Kitabu hicho kinauzwa bei gani mkuu?? Tafadhari usiweke bei ambayo wengine tutashindwa kuimudu
 
Ilikuwa mwaka 1927 ndipo chama cha AA kiliundwa kwa msaada wa Gavana wa Kiingereza nchini Tanganyika Sir Roland Davidl Cameron na Dr Agrey raia wa Ghana mwenye mtaa Kariakoo ya leo, huyu Mghana alikuwa mshauri wa kisheria na kimuundo tu, kikawa kinafanyia shughuli zake nyumbani kwa Rais wa kwanza wa AA bwana Cecil Matola kutoka kabila la wayao, na miaka mitatu baadae, yaani 1930 ndipo wakapata jengo toka kwa Gavana Donald Cameron, hapo ndipo picha hii ilipigwa,

Mwaka 1933 Cecil Matola alifariki dunia, na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa AA Bwana Kleist Sykies (ambae baba yake mzee Platanta alikuwa ni muhamiaji haramu toka Afrika Kusini aliyefika Tanga na kuanzisha makazi huko baada ya kuwa mateka wa wajerumani vita ya kwanza ya dunia), mpaka mwaka 1948 chama kilipobadilishwa jina nakuwa TAA chini ya Rais wake Daktari Vedasto Kyaruzi (Mhaya),

Hapo Rais wake wa kwanza wa TAA akawa Daktari Vedasto Kyaruzi, na katibu akawa Abdulwahid Klest Sykies, miaka miwili baadae, Dr Kyaruzi alihamishiwa Kingolwila hivyo nafasi ya urais wa AA ikakaimiwa na Abdulwahid Kleist Sykies hadi ilipofika uchaguzi wa 1953 ambao Julius Nyerere alimshinda Abdulwahid Kleist Sykies kwakishindo na kuwa Rais wa TAA, Mwaka mmoja baadae Julius Nyerere alibadilisha jina na mrengo wa TAA nakuwa TANU ya kupigania uhuru kutoka chama cha kuratibu shughuli za starehe za weusi (chama cha walevi)

................................................................ Yote kwa urefu yamo katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,

View attachment 544629

View attachment 544695
Wafia dini wakiislamu wao historia ya TANU na harakati za kudai uhuru huzianzia kwa Abdul Sykeis tu

Habari za African Association (AA) baadae Tanganyika African Association (TAA) huwezi kukuta wakizizungumza
 
Good history to start with, lakini Yericko wewe si nasikia huwa unaandika vitabu? Kama ndivyo, mbona una punctuation mbovu kiasi hiki?

In addition, for your own benefit, hukutakiwa kuweka link kavu ya Amazon bali link ya hicho kitabu! Na hicho kitabu chenyewe binafsi nimeshindwa kukiona kupitia hiyo Amazon main link!
Chige,
Yericko hana kitabu wala nini...
Kuandika hajui ataweza kuandika kitabu?

Hebu soma hili darsa nililomzawadia huko FB:
''Bado niko na wewe Yericko. Nimekuwekea darsa zima kuhusu uandishi wa vitabu. Meza kibri chako na soma na zingatia. Umesema uko Amzon lakini ukweli ni kuwa hawakujui huko. Mimi nimeingia Amazon toka mwaka wa 1998 kwa hiyo nawajua vyema. Kuna kitu lazima ukijue pia. Amazon hujipeleki. Amazon unapelekwa na ''publishers,'' na ''booksellers'' yaani wauza vitabu. Kuna kitu kinaitwa ''blarb'' katika kitabu. Haya ni maelezo nyuma ya ''cover,'' ya kitabu. ''Blarb,'' inaandikwa na ''publisher,'' si wewe Yericko. Huu ni ushauri wa bure wenzako wanalipia fedha. Mimi nakupa bure ili ujitoe katika ujinga.''

5bDT5yK4WfHz0QFpqYKBzUNiSToufTEZZ5p4HUil4VnNM7AoRI2DPidbJp3SvJjB4tC74NS1Me9u6h_WzKik7hLuj6eQM6uKlb7jjgn-2OeZxEV7ZWVUt2N1lXfLGR3n-cjnsiif0fZH3_TyeEzV80edxUgStfIJs7gZrzdi4EFjDMRwjOYK2OnpI2ub0FdB9e1Q7-uC1uVcXDSohM3Orp2aQMp73JB023taZeWCz-M9WtJEVuxq_C7qjt68ahXqSlkX68knlzkxEapRn4dllWkiZaXT-9COMnzIqGI6jD8VWF-AY374i0m8NnAP8TU6mVRgMBc2jBLvDQypndbIEuDNrzBHId43uU07S35PFVz-iFP1h6ZTFGyA7dnVUAtPdGV_m94rgn3QyRJ8rWHWDpVF2ywH1qBSHGQH0e0vV7h2EtTUERqlkuvBxab22AHizpLrSFtxPgxBF_G57kU_4Uj35VLjlI7MPPGS0GnKsMVT1kDG0BOBNPDrvn_IFCKqi2k7SlcNVRfmO5CiOMQpAZpcHt7u9_KPzCdVMxtwkVYUvD1v2bYtDHeWGOs6J7Iu8rohqMAhLLgNhzySaThe6Yu0Z5dY_XoOBNVnqq_zNA_mf9F5au2JpQ=w335-h188-no

''Daisy baada ya kufariki baba yake mwaka wa 1968 alitaka kuandika kitabu cha maisha yake lakini mwalimu wake John Iliffe alimwambia somo hilo linataka muda haitakuwa vyema kwa yeye kufanya haraka. Daisy hakuandika kitabu kile na ikaja kuwa mimi ndiye Allah akanijaalia kukiandika kwa msaada mkubwa sana wa nyaraka za ukoo wake. Picha hiyo tumepiga April 2017 na Daisy ni huyo kashika kitabu cha maisha ya baba yake. Unaweza kumsoma Daisy katika hii, ''paper,'' yake: A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15). Inapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana.''

''Marafiki wa Mwalimu Nyerere na baadhi ya wasomi wameona ni bora baada ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes ambacho kwa namna moja au nyingine kimegusa maisha ya siasa ya Baba wa Taifa, na wao wafanye utafiti na iandikwe ''biography,'' ya Mwalimu Nyerere. Nimefanya mahojiano na wao nyumbani kwangu Magomeni Mapipa mara tatu na nimewapa nyaraka na picha nyingi sana kutoka kumbukumbu za akina Sykes. Mradi huu nadhani sasa uko mwaka wa nne. Wanaofanya utafiti huu ni Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman Yahya na Dr. Kamata.''

Chige,
Haya ndiyo yangu katika historia hii.
 
Wafia dini wakiislamu wao historia ya TANU na harakati za kudai uhuru huzianzia kwa Abdul Sykeis tu

Habari za African Association (AA) baadae Tanganyika African Association (TAA) huwezi kukuta wakizizungumza
Aotomata,
Hapana haja ya kuhamaki na kuja na lugha kali huu ni mjadala tu
hapana sababu ya kutukanana.

Ikiwa lipo jambo unaloona halikukaa vyema unaandika fikra zako
hapa na sote tunachangia.

Huu ndiyo uungwana na huu ndiyo ustaarabu.

Historia ya TANU ukipenda unaweza kuanza na Kleist baba yake
Abdul miaka ya 1920 na unaweza pia kuanza na Kleist mwenyewe
miaka ya 1940 mwishoni.

Lakini pia ukipenda unaweza kwenda nyuma zaidi katika Vita Vya
Maji Maji wananchi waliponyanyua silaha dhidi ya ukoloni wa
Wajerumani.

Hapa utakutana na Chief Abdul Rauf Songea Mbano.
 
Back
Top Bottom