Juvenile, usipoteze bundle yako, hicho kitabu hakipo Amazon!Hahaa hadi niende Amazon ndipo ntatoa conclusion
Mkuu Yericko Nyerere, pasipo kung'ata meno wala kumung'unya, Mzee Mohamed Said ametamka wazi kwamba hauna kitabu Amazon! Nami naweza kushuhudia hilo ili kumpunguzia mzigo juvenile davis kwenda huko kujitafutia conclusion yake!
Ya nini basi kusema hicho kitabu kinapatikana Amazon wakati hakipo? Na kwa kuangalia hiyo picha ya kitabu uliyoweka hapo juu haielekei kwamba kina ISBN (International Standard Book Number), haidhuru hata kama kinaonekana upande wa mbele peke yake!!
Hivyo basi, nami nakubaliana na maelezo ya Mohamed Said kwamba hicho kitabu hakina ISBN na kwahiyo hakipo Amazon.
Nami katika shughuli zangu za ugangaji njaa nilishawahi kupata project ya kufanya products listing kwenye e-commerce library moja. Moja ya source kuu niliyokuwa natumia kupata hizo products ni Amazon na zingine alizotaja Mohamed Said kwenye post moja wapo bila kusahau eBay!!!
Kote huko, katu huwezi kukuta kitabu ambacho hakina ISBN... never, ever!
Hapana, nisiapize! Labda niseme mimi binafsi sikuwahi kuona kitabu ambacho hakina ISBN ingawaje nilifanya outsourcing ya maelfu ya bidhaa... books and other multimedia products kv DVDs, Blu Rays, Video Games n.k! Zote hizo, lazima ziwe na identification numbers.
Sina shaka, kitabu huenda unacho lakini usichotaka ni kuonesha kwamba kinapatikana kwenye maduka ya mchangani peke yake! Ili watu wakipate popote walipo duniani, basi fuata ushauri wa Mohamed Said wa namna gani unaweza kupata ISBN.
Nyongeza yangu kwa yale aliyoshauri Mohamed Said ni hii! Kama alivyosema Mzee wetu, anaefanya ISBN application ni Publisher. However, an Author anaweza ku-act as a Publisher as well kwa case ya ISBN application. Hii hutokea pale publication costs zinapokuwa fully borne (from bear) na Author mwenyewe.
Wasiliana na ISBN National Agency kwa sababu ndie atakaehusika. Kama humfahamu, huyu hapa:
Organization: National Bibliographic Agency
Address: Director General
Tanzania Library Services Board
P.O. Box 9283
Dar es Salaam
Phone 1: (+255 22) 21500 48
Phone 2: (+255 22) 21500 49
Fax 1: (+255 22) 21511 07
Email: tlsb@africaonline.co.tz
Web: Tanzania Library Services Board - TLSB
Kama hakuna mabadiliko, contact person ni: Ms. Emily Emmanuel Meshack
Bila ISBN huwezi kuuza kitabu Amazon, Full Stop!
NOTE: Kama cost bearer ni wewe mwenyewe unaweza ku-apply ISBN wewe mwenyewe kwa sababu, usefulness ya ISBN haitakuwa na umuhimu wowote kwa publisher but to yourself!!!
Natoa hiyo tip kwa sababu Kibongo bongo watu tunakuwa nyuma kidogo na mambo jinsi yanavyoendeshwa duniani. Kutokana na hilo, unaweza kufika pale Agency na wakakukomalia kwamba ni LAZIMA Publisher (Publishing Company) ndie afanye application for ISBN.
Hata hivyo, International ISBN Agency wanatoa exceptions, na kimsingi wanaeleza ni nani hasa anayepaswa ku-apply.