Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

M2...
Soma hapo chini ni bandiko langu la ziku za nyuma hapa Majlis:

Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
grey10.gif
By Mohamed Said
Pondamali,
Hilo usemalo wala halina wasiwasi umesema kweli.

Abdul Sykes alikuwa katibu na kaimu rais wa TAA toka Dk. Kyaruzi alipopewa
uhamisho.

Wala sina haja ya kuweka sawa ninayoandika hilo mie nikilijua siku zote.
Kwani pamezuka nini?

Vipi kuhusu habari za Mzee Kasella Bantu.

Ungependa nikuwekee hapa habari zake zaidi au umetosheka basi na zile za
mwanzo?

Pondamali,
Historia Abdul Sykes inakuhangaisha wewe kama ilivyowahangaisha
wengi kabla yako.

Kwa mara ya kwanza nilipoandika habari zake katika gazeti la Africa
Events lililokuwa linachapwa London, toleo zima lilikusanywa likapigwa
moto.

Jiulize amri ya kuyakusanya magazeti yale ilitoka wapi na nini sababu
yake?

Huenda usiamini lakini ndivyo ilivyokuwa.

Kwa yale machache ambayo yaliwafikia watu habari ile ilikuwa gumzo
kubwa.

Watu wengi walivurugikiwa akili kama wewe hii leo akili yako
inavyovurugika.

Unajiuliza,''Hii kweli au ni uongo na porojo za Mohamed Said?''

Watu wengi hapa jamvini husema naandika porojo.
Wengi walikuwa hawajamsikia Abdul Sykes kuwa ndiye aliyeunda
TANU.

Sasa gazeti lile lilikuwa na makala,‘'In Praise of Ancestors’' Africa
Events,
London, March/April 1988, (uk. 37-41) nilitaja mchango wa
Waislam na nikamtaja Abdul Sykes.

Kwa wengi historia hii ilikuwa ngeni kabisa.

Pondamali sasa nakurudisha kwa Dk. Kyaruzi na dhana kuwa yeye
ndiye aliyemwachia chama Nyerere.

Nakuambia kwa kinywa kipana kabisa.
Huo ni uongo.

Haya ninayoweka hapo chini nimetoa katika kitabu changu:

''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold
Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998.

''In June, TAA headquarters announced its executive committee
with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias
and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were
Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z.
James, Dome Okochi, C. Ongalo
and Patrick Aoko.[1] The composition
of the TAA leadership showed East African solidarity that existed
during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected
as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it
was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid
talked to Nyerere seriously about forming an open political party to
replace TAA.''



[1]Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

Pondamali,

Nimekuwekea hapa juu uongozi wa TAA wa 1953 na gazeti ambalo
lilitaarifu habari hiyo.

Umeomuona Mzee Kasella Bantu katika mabadiliko hayo ya kihistoria?

Uongozi huu mpya ulitokea baasa ya uchaguzi wa tarehe 17 Aprili
katika Ukumbi wa Arnautoglo ambako Nyerere alichaguliwa kuwa rais
wa TAA na Abdul Sykes makamu wake.

Katika hali kama hii vipi Dr. Kyaruzi iwe kamuachia chama Nyerere?

Achilia mbali kuwa yeye alipata uhamisho kwenda Kingolwira na kisha
Nzega mwaka 1951.

Mimi nawapeni sana pole kwa kuwa kwa kweli mnaziviza akili zenu
pasi na sababu ya maana.

Hakuna mwanahistoria ambae ataweza kuandika historia ya TANU
au ya Nyerere bila ya kwenda kwenye Nyaraka za Sykes.

Hii ni hazina ya kipekee kabisa.
Ukiwa hujaridhika rejea tena na maswali mengine.

Insha Allah utanikuta mie bado nabariz hapa jamvini nakusubiri.

Tuagane kwa swali hili langu moja.

Pondamali,
Mzee Kasella Bantu
hakupata kukuhadithia ile ''drama,'' siku ile
ya uchaguzi kati ya mwalimu wa shule Nyerere ambae hakuna
aliyekuwa anamfahamu na Abdul Sykes kijana maarufu wa mjini?

Mimi ''movie'' nzima ninayo kanihadithia Dossa Aziz nyumbani kwake
Mlandizi.

Mzee Kasella Bantu hakupata kukuhadithia kwa nini yeye na
Nyerere walikuwa maadui wakubwa kufikia Kasella Bantu kutoroka
nchi kwenda Ujerumani hali kapitishwa uwanja wa ndege kavaa
mavazi ya kipadri?
Kasella Bantu ndio huyo?
dear-priest-look-away.jpeg
 
Porojo jazz band zimeanza cha uzuri huyo Sykes alikuwa mkristo aliingia Uislam sababu ya Mwanamke tu na si vingine..
 
Porojo jazz band zimeanza cha uzuri huyo Sykes alikuwa mkristo aliingia Uislam sababu ya Mwanamke tu na si vingine..[/Qkitabu chaUOTE]
Duduwasha,
Ikiwa unaona kitabu cha Abdul Sykes ni, ''porojo,'' Dictionary of African
Biography, Oxford University Press New York, 2011 wamechapa maisha
ya Kleist Sykes:

DSCN1132.JPG
 
Kasella Bantu ndio huyo?View attachment 553050
Duduwasha,
Kasella Bantu ni huyu hapa chini kama nilivyomwandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Kasella Bantu, yeye alisoma Afrika Kusini kwa hivyo alishuhudia utawala wa mabavu wa weupe na ubaguzi wa rangi. Kasella Bantu alikuwa akiwasema sana Waingereza. Alipokuwa Afrika ya Kusini alizozana na Mzungu mmoja, Hugh Tracey. Tracey aliandika ripoti ya siri kwa utawala wa kikoloni dhidi ya Bantu. Alipokuwa akifanya kazi Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) Shirika la Utangazaji Tanganyika, Bantu kwa mara nyingine tena alizozana na ofisa mmoja Mzungu. Kisa cha ugomvi ni kuwa yule Mzungu aliwaita Waafrika ‘’wapumbavu.’’ TBC ilikuwa chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii. Kesi ya Bantu ilipoletwa mbele ya Kamishna wa Maendeleo ya Jamii, Kamishna alirejelea ripoti ya awali kuhusu tabia ya Bantu iliyoandikwa na Tracey nchini Afrika ya Kusini. Kamishina yule alifikia uamuzi kuwa Bantu alikuwa mkorofi na akamfuta kazi.''
 
kwann us na sio saudia iran kuwait yemen syria nk
Mtanganyika...
Nakuwekea hapo chini nchi ambazo nimefika na nimejifunza mengi katika nchi hizo:

Zambia, Ethiopia, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey, Abu Dhabi, Uingereza, Afrika ya Kusini, Ujerumani, Nigeria na United States of America.
 
I thought hiyo dictionary imechapishwa miaka ya sitini kumbe 2011 means wanaweza kuwa wamelishwa na ukanjanja wako zaidi ya fact...
 
I thought hiyo dictionary imechapishwa miaka ya sitini kumbe 2011 means wanaweza kuwa wamelishwa na ukanjanja wako zaidi ya fact...
Duduwasha,
Dictionary of African Biography (DAB) ulikuwa mradi wa Oxford University Press,
New York na Harvard University chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong.

Uliwajumuisha wanahistoria zaidi ya 500 ulimwenguni.

Lakini kabla ya mimi kuwa katika mradi huu nilikuwa katika mradi mwingine wa
Qxford University Press, Nairobi na walichapa kitabu changu kimoja, ''The Torch
on Kilimanjaro.''

the%20torch%20on%20kilimomanjaro.jpg
 
Duduwasha,
Dictionary of African Biography (DAB) ulikuwa mradi wa Oxford University Press,
New York na Harvard University chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong.

Uliwajumuisha wanahistoria zaidi ya 500 ulimwenguni.

Lakini kabla ya mimi kuwa katika mradi huu nilikuwa katika mradi mwingine wa
Qxford University Press, Nairobi na walichapa kitabu changu kimoja, ''The Torch
on Kilimanjaro.''

the%20torch%20on%20kilimomanjaro.jpg
Hongera sana ndugu
 
Duduwasha,
Dictionary of African Biography (DAB) ulikuwa mradi wa Oxford University Press,
New York na Harvard University chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong.

Uliwajumuisha wanahistoria zaidi ya 500 ulimwenguni.

Lakini kabla ya mimi kuwa katika mradi huu nilikuwa katika mradi mwingine wa
Qxford University Press, Nairobi na walichapa kitabu changu kimoja, ''The Torch
on Kilimanjaro.''

the%20torch%20on%20kilimomanjaro.jpg
Mkuu Mohamed Said
Humu vijana wengi na mbao za kuwasomeshea wengine endelea kuwatumia kwa hekma na busara mara dufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko,
Wewe huna kisomo cha kupambana na mimi.

Nakupa changamoto nyingine.
Kitabu cha Abdul Sykes kimefanyiwa review na John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Review ya Iliffe na Glassman zimechapwa katika Cambridge Journal of African History.

Sasa fanya utafiti uone hapa Tanzania ni wangapi wamepata kuandika na vitabu vyao vikapata review katika hii journal.

Yawezekana kabisa kwa kuwa huna ulijualo katika utafiti na uandishi ikawa huoni kabisa uzito wa jambo hili.

Lakini kukusaidia hebu nenda British Council Library katizame mna nini katika hii journal na usiishie kutazama muulize mkutubi hadhi ya hiyo journal.

Ati utaamka na mimi.
Uamke na mimi ndiyo iwe nini.

Amka kamwagie dawa bamia zako utakuwa umefanya kazi ya maana sana kuliko kutaka kuweka mjadala na Mohamed Said.

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi mzee Mohamed Said msamehe mtoto mdogo sana huyu..!

Sent by Ubavu
 
Allah amewakataza Waislam kuwatukania watu miungu yao
wasije wakamtukana mungu wa kweli.
Ungelitambua hilo usingetembea dunia nzima ukiwatukana... Hivi Kleist Sykes asingebadili dini yake ya ukristu kisa mwanamke akawa muislamu leo ungemlilia kila kona ya ulimwengu? Mbona Cecil Matola humsemi wala kumuenzi zaidi ya kumfifisha ilihali yeye ndie mwasisi wa vyama Tanganyika?
 
Yericko hujui kitu katika historia hii wewe unajisemea tu.

Sykes Mbuwane kaingia Tanganyika akiwa Muislam na alikuwa na nduguye kipofu wamekuja pamoja anaitwa Ali Katini.

Ramadhani Mashado Plantan kaingia Tangnayika 1905 akiwa na umri wa miaka 5 akiwa Muislam.

Hakika nahadhiri kwingi duniani na nashirikishwa katika miradi ya historia ya Afrika kwa kupewa mialiko.

Ningekuwa natukana hakuna chuo wala taasisi kingenipa heshima wala wasingechapa vitabu vyangu.

Bado nakusisitizia usome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko hujui kitu katika historia hii wewe unajisemea tu.

Sykes Mbuwane kaingia Tanganyika akiwa Muislam na alikuwa na nduguye kipogu wamekuja pamoja anaitwa Ali Katini.

Ramadhani Mashado Plantan kaingia Tangnayika 1905 akiwa na umri wa miaka 5 akiwa Muislam.

Hakika nahadhiri kwingi duniani na nashirikishwa katika miradi ya historia ya Afrika kwa kupewa mialiko.

Ningekuwa natukana hakuna chuo wala taasisi kingenipa heshima wala wasingechapa vitabu vyangu.

Bado nakusisitizia usome.

Sent using Jamii Forums mobile app
historia unaipotosha kwa ufia dini wako!
ww mwanazuon wa madrasa dini itakuua kihoro,wacha porojo za vijiweni kwenye kahawa wacha "usomi mwanasesere"
 
Back
Top Bottom