Ah Mohamed, kama utamaduni wako ni ule wa Nabii Ibrahimu hakuna shaka
Tatizo linajitokeza kwa ukweli kuwa LUGHA hubeba utamaduni wa jamii husika.
Ni ukweli usiopingika popote pale duniani
Sasa Arabic umesema huwezi kuzungumza, na hiyo ndiyo imebeba utamaduni. Huoni tatizo hapo?
Nguruvi3,
Hapana sijaliona tatizo.
Hakika lugha hubeba utamaduni nami ninalo tatizo hili nina mjukuu
hasemi Kiswahili na nawaambia wazazi wake kuwa Uislam unakwenda
na utamaduni wake kwenye lugha yetu nayo ni Kiswahili.
Wakifanya maskhara, nawaambia mtoto atasoma Qur'an na lafidhi ya
London.
Mimi lugha yangu ni Kiswahili na Uislam umejikita vizuri katika Kiswahili.
Nikisema, ''shahada,'' najua ni nini halikadhalika nikisema, ''sala.''
Hiki ni Kiarabu na kipo ndani ya Kiswahili.
Nikisoma Aya hii, ''Akimi salat liduluki shamsi ila ghasaki layli wa Qur'an
Fajr...''
Angalia hapo unayaona maneno mangapi ya Kiswahili katika Aya hiyo?
Wewe utatambua, ''sala,'' ''Qur'an,'' na ''Fajr.''
Aliyesoma Qur'an atajua maana ya maneno yote hayo ila labda machache.
Nadhani umeelewa.
Sasa turudi kwa yule mwalimu wangu wa Arab Maratime Transport Acedemy
Alexandria, Egypt.
Tuko katika msikiti wa Muntaza Palace, Alexandria.
Muntaza ilikuwa moja ya makasri ya Mfalme Faruq wa Misri na kuna msikiti
mzuri sana.
Tumemaliza kusali Ijumaa akaniuliza kama nimeelewa khutba nani nikamjibu
kuwa nimeielewa.
Akashangaa vipi nimeielewa khutba ya Kiarabu ilhali mimi Kiarabu sikijui?
Nadhani sasa nimekuelewesha na umefahamu.
Hii ni nyongeza.
Iko siku huyu mwalimu wangu akaniuliza kama namjua Um Kulthum.
Nikamwambia kuwa mama yangu akiimba nyimbo zake tena kwa Kiarabu.
Alichoka.