"boywise, post: 22685677, member: 423208"]Mkuu Nguruvi3
Kwani wewe bado ni mgeni na kazi za Mzee Mohamed Said katika Historia ya Uhuru wetu?
Kwanza nikupongeze kwa kukubali kwako kuwa nikweli upo mchango wa baadhi ya Waislamu katika uhuru wetu na bila shaka Mzee Mohamed Said amekusaidia sana katika hili.
Nadhani wewe ni mgeni katika majadiliano baina yetu na Mohamed.
Akitoa toleo la kwanza wengine tulishahoji kitambo sana kuhusu historia iliyokuwepo
2011 tulipoanza kujadili vitabu vyake, sikumbuki mtu aliyekataa mchango wa Waislam
Ni kutokana na ukweli mji mkuu ulikuwa Pwani wakazi wengi Waislam
Haina maana mapambano ya uhuru yalikuwa Pwani peke yake, la hasha.
Kwingine kulikuwa na vugu vugu la kukataa udhalimu.
Huko walipokuwepo bado walitoa mchango mkubwa
Mzee Mohamed Said ameeleza wazi kuwa alichukua jukumu la kuufahamisha umma kuhusu mchango wa Waislamu baada ya kuwa hapakua na popote katika Historia ya Tanu na Uhuru ulipotajwa sasa kwa hili ulitaka awataje na wasiokua Waislamu?
Historia haiandikwi kwa utashi wa mtu, maono au chaguo 'cherry-pick'
Huwezi kuandika historia ya dunia ukamweka Hitler pembeni kisa humpendi
Huwezi kuandika historia ya Tanganyika ukaondoa watu wengine kisa hawahusiki
Ni makosa yale yale uliyosema yaliwaondoa Waislam katika historia kwa kutotajwa ndiyo unapigia upatu wa kuondoa makundi mengine kama afanyavyo Mohamed. Umeona!
Historia ni mtiririko wa matukio kama yalivyotokea na kujidhihiri
Ukiandika historia na kumwacha John Rupia, Cecil Matola, Vedastus Kyaruzi na wengine kwasababu si Waislam historia haikamiliki. Haikamiliki kwasababu kutakuwa na matundu
Ni kwa mantiki hiyo, hakuna kitu kinaitwa historia ya Waislam kupigania uhuru ukiacha wahusika wasio waislam. Kuna Historia ya Tanzania ambayo ndani yapo makundi
Lakini pia itakua vema kama nawe utakuja na majibu ya kuwa kwanini mchango wa Waisamu umepuuzwa na hata baadhi yao kufikwa na madhila baada ya huo uhuru kupatikana.
Kuna vitu viwili unachanganya katika hili.
Kwanza, kuna kupigania uhuru na pili kuna yatakanayo baada ya kupata uhuru.
Uhuru ulipoiganiwa ilikuwa ni suala la kiutu na kibinadamu.
Mohamed Said amenukuu Aabdul Sykes akieleza kuhusu hili.
Hivyo jitihada za ''kujikomboa zililenga kurudisha utu na heshima ya Mwafrika''
Baada ya uhuru kukaja suala la kujitawala.
Hapa tukaondoka katika harakati za utu na ubinadamu tukaingia katika siasa.
Ilikuwa ni dhahiri Waislam walitaka kuchukua haki ya kupigania Uhuru na kuifanya haki ya kisiasa, rejea hotuba ya Rehan Bilal Waikela, moto wa Waislam ukiwaka
Kisiasa hakuna anaye vumilia matishio katika utawala, bila shaka Nyerere hakuwa tofauti.
Lakini pia utambue tulihitaji umoja wa Taifa kwani tulikuwa hatuna Utaifa kwa kuanzia.
Kundi moja linapochukua mapambano ya uhuru na kujimilikisha halikuwa jambo sahihi
Kuna nchi zilijaribu zimeishia katika matatizo makubwa heri yetu sisi tuliojaribu vinginevyo
Historia ni reflection ya yaliyotokea. Dunia ya sasa inazungumzia historia kama kumbu kumbu kwavile asilimia zaidi ya 90 hawakuwepo wakati huo na ni vizazi vya 3 au 4
Tatizo linaljitokeza katika maandishi ya Mohamed, ni kuhamasisha watu kuhusu 'umiliki' wa historia ili kujenga hoja katika msingi wa historia.
Inaweza kuonekana ni jambo jema kwa wakati huu, siku za mbeleni ni jambo lenye athari kubwa kwa jamii ile ile anayoizungumzia
Unapopandikiza fikra kuwa babu au bibi walipigania uhuru na hivyo unapaswa kubebwa na historia ni kujidumaza. Historia itumike katika reflection kwa mambo mazuri
Kwamba kama yupo aliyetoa mali zake kusaidia uhuru, kwanini wasiwepo wanaotoa mali zao kubadilisha hali za jamii kielemu, uchumi au utamaduni? Hiyo ndiyo kazi ya historia
Athari za mantiki iliyotafsiriwa na jamii ni kuwa wapo waliopigania uhuru wanaonewa
Mohamed kajenga historia kwanza, halafu katumbukiza mbegu hizo(rejea takwimu za elimu kuhusu mitihani) na nafasi za kazi kwa mujibu wa mijadala tuliyokuwa nayo
Jamii inaondoa focus kwenye 'real problem' na kudhani suluhisho ni historia.
Huwezi ku qualify kuwa mwandishi mzuri kama Mohamed kwasababu ya historia kama ambavyo huwezi kuwa Eng., Entrepreneur, Mhasibu, Daktari au professor kwa historia
Ikiwa wazee wetu waliji organize wakaondoa tofauti na kupigana na mkoloni, kwanini kiwepo kizazi kinachotaka kusimama katika mabega yao bila kizazi hicho kuweka miguu chini ili kingine kijacho kijifunze kutoka kwao?