Mohamed Said ukweli hujidhiri, Boywise kajiunga 2017 March 20.
Mimi nawewe tumekuwa katika mjadala mzito kuanzia 2011
Boywise anachouliza hakinigusi ndiyo maana bandiko 170 nimemueleza kwa utulivu na kina
Utakumbuka wakati unaanza mjadala, niliwahi kukuuliza maswali.
Ikiwa leo hii simba wanakula wanadamu Rufiji, miaka ya nyuma Mshume aliwezaje kusalimika na hilo katika kueneza TANU?
Ikiwa baraza kuu la Tanu liliundwa na asilimia 98 Waislam, nini kilitokea asilimia 2 ikazidi nguvu 98?
Tulikuuliza, ikiwa Kleist Sykes alianzisha AA nafasi ya Mwalimu Cecil Matola ilikuwa wapi?
Tukauliza ikiwa Abdul Sykes alimpokea Nyerere alipoingia Dar kwa mara ya kwanza, ni ukweli kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza?
Orodha ya maswali ni ndefu ambayo hayakuwa na majibu.
Hii maana yake ni kuwa kuandika hakuaaminishi ni kukamilika kwa historia kwani wewe si alpha na Omega. Historia ya Uingereza inasomwa na inaandikwa seuse ya Abdul
Hakuna mtu aliyakataa kushiriki kwa familia ya Sykes au nyingine.
Tulichokataa ni kutaka kumtumia Mwalimu kwa kumlinganisha na Abdul.
Kwamba ukuu wa Abdul hautimii bila mwalimu. Kama utakumbuka tulikueleza watu hao ni tofauti kwa sifa zao, kuwalinganisha si kuwatendea haki na hasa Abdul
Tofauti inayokutia maudhi ni wewe kutaka hadhira ya 'hewalaa, ndiyoo'. Hilo hapana
Unakukumbuka elimu uliyopata hapa kwa hoja za mantiki na nzito
Nikupe mfano, elimu ya utafiti wa takwimu ambayo tunakushukuru umetuelewa
Nguruvi3,
Cecila Matola alikuwapo pamoja na wazalendo wengine kwenye kitabu
cha
Abdul Sykes nimeorodhesha majina yote ya waasisi wa African
Association:
Kleist Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, brahim Hamis, Zibe
Kidasi, Ali Said Mpima Suleiman Majisu, Raikes Kusi, na Rawson
Watts.
Mshume Kiyate si aliyeijenga TANU Rufiji bali ni
Said Chamwenyewe
aliyekuwa akipanda baiskeli kutoka Dar es Salaam hadi hadi Rufiji.
Ikiwa unaamini kuwa wanaoliwa na simba ni wapanda baiskeli barabarani
mimi sina la kusema lakini hiyo ndiyo historia ya
Said Chamwenyewe na
alikwenda Rufiji baada ya kuagizwa na
Abdul Sykes nakuwekea mkasa wake:
''TANU ilipata tasjili yake tarehe 30 Novemba, 1954 baada ya kuzishinda hila nyingi na vizingiti vilivyowekwa na serikali za kupinga usajili wake. Bi Zainabu, mke wa Ally Sykes anakumbuka siku moja adhuhuri, jua lilikuwa kali, wakati Nyerere alipokwenda nyumbani kwao Mtaa wa Kipata (Siku hizi Mtaa wa Kleist) ambako Ally na kaka yake Abdulwahid walikuwa wakimsubiri atoke mjini alikokwenda kushughulikia tasjila ya TANU. Alipofika Nyerere alionekana amechoka taabani na mwenye wasiwasi. Alizama ndani ya sofa akaufunika uso wake kwa mikono yake na akakaa kimya kwa muda. Abdulwahid na Ally walikuwa wakimsubiri azungumze. Nyerere alikuwa na habari mbaya. Serikali ilikuwa imekataa kuisajili TANU. Nyerere aliwaambia kuwa serikali ilikataa kutoa usajili kwa sababu za kiufundi. Serikali ilidai kuwa TANU haikuwa na wanachama. Baada ya kufahamu kuwa serikali imekataa maombi ya TANU kwa kuwa ati haikuwa na wanachama wa kutosha, mithili ya onyesho la mchezo wa kuigiza unaokwenda haraka, Abdulwahid alitumia hekima na mara moja akamuomba Said Chamwenyewe aende nyumbani kwao Rufiji kusajili wanachama kwa ajili ya TANU. Rufiji ni sehemu ya Waislam watupu. Kwa ajili hii TANU haikuwa na tatizo la kuwapata wanachama. Kwa hakika wanachama wa mwanzo wa TANU walikuwa kutoka Gerezani na Rufiji.''
Hiyo
Nyerere, ''mara ya kwanza,'' kupokelewa na
Abdul Sykes sijui umeitoa wapi.
Angalia hapo chini Nyerere alivyoeleza vipi alikutana na
Abdul Sykes:
''Katika hotuba ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, (wazee wa Kiislam waliomuunga mkono wakati wa kudai uhuru) aliyoitoa tarehe 5 Novemba, 1985 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Nyerere aliwaambia waliohudhuria kuwa Kasella Bantu ndiye aliyempeleka nyumbani kwa Abdulwahid na kumtambulisha. Hii ilikuwa mara ya kwanza Nyerere kuzungumza hadharani kuhusu kufika kwake Dar es Salaam na ilikuwa mara yake ya kwanza kuihusisha hadharani historia yake, ya TANU na jina la Abdulwahid.''
Hiyo orodha yako ya maswali sijapatapo kuiona tafadhali ilete na ikiwa ninayo majibu
In Shaa Allah nitajibu.
Umezungumza historia ya Uingereza sawa lakini kwa hii ya TANU hadi sasa hakuna
aliyeigusa tena baada ya mimi kuiandika kwa kutumia
Nyaraka za Sykes ambazo
sasa baadhi zimetiwa katika Kavazi la
Mwalimu Nyerere.
Wala mimi sijapatapo kumlinganisha
Abdul na
Nyerere hata siku moja nilichofanya
ni kusema tu kama ni historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika mbona jina la
Abdul,
Sheikh Hassan bin Amir na wazalendo wengine hayamo kwenye historia ya uhuru?
Sijapatapo, ''kuudhika,'' kwa kupingwa kitabu changu.
Sana, sana nafurahi kwani inanifanya mimi kuwa na nafasi ya kueleza mengi kwenu.
Sijaelwa unakusudia nini kuhusu elimu ya ''takwimu.''
Ingia hapo chini kuna ya ziada:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE