Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Boywise,
Nguruvi3
anasema ati wewe mgeni katika mjadala huu.

Kaguswa na ukweli uliomueleza tena kwa utulivu.Kleist na wanawe watatu wote walishiriki katika siasa za uhuru wa Tanganyika na kuunda TANU
Mohamed Said ukweli hujidhiri, Boywise kajiunga 2017 March 20.
Mimi nawewe tumekuwa katika mjadala mzito kuanzia 2011
Boywise anachouliza hakinigusi ndiyo maana bandiko 170 nimemueleza kwa utulivu na kina

Utakumbuka wakati unaanza mjadala, niliwahi kukuuliza maswali.
Ikiwa leo hii simba wanakula wanadamu Rufiji, miaka ya nyuma Mshume aliwezaje kusalimika na hilo katika kueneza TANU?

Ikiwa baraza kuu la Tanu liliundwa na asilimia 98 Waislam, nini kilitokea asilimia 2 ikazidi nguvu 98?

Tulikuuliza, ikiwa Kleist Sykes alianzisha AA nafasi ya Mwalimu Cecil Matola ilikuwa wapi?

Tukauliza ikiwa Abdul Sykes alimpokea Nyerere alipoingia Dar kwa mara ya kwanza, ni ukweli kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza?

Orodha ya maswali ni ndefu ambayo hayakuwa na majibu.

Hii maana yake ni kuwa kuandika hakuaaminishi ni kukamilika kwa historia kwani wewe si alpha na Omega. Historia ya Uingereza inasomwa na inaandikwa seuse ya Abdul

Hakuna mtu aliyakataa kushiriki kwa familia ya Sykes au nyingine.

Tulichokataa ni kutaka kumtumia Mwalimu kwa kumlinganisha na Abdul.

Kwamba ukuu wa Abdul hautimii bila mwalimu. Kama utakumbuka tulikueleza watu hao ni tofauti kwa sifa zao, kuwalinganisha si kuwatendea haki na hasa Abdul

Tofauti inayokutia maudhi ni wewe kutaka hadhira ya 'hewalaa, ndiyoo'. Hilo hapana

Unakukumbuka elimu uliyopata hapa kwa hoja za mantiki na nzito
Nikupe mfano, elimu ya utafiti wa takwimu ambayo tunakushukuru umetuelewa
 
Mzee huyo yericko ana chuki binafsi na wewe ndio maana anajifanya mjuaji sana hata ukiona mtu hataki kukosolewa huyo anarudi kwenye kundi la wapumbavu sio wajinga
Hekima ya mjadala ni kuzungumza kwa stara
 
Xungura na Boywise,
Kuna mengi ya kusikitisha jinsi historia hii ilivyopigwa vita.
Angalia hapa chini mkasa uliomfika mama wa Kiingereza Paula Park.

Huyu mama aliandika makala, ''An Unsung Hero?’ Africa Events, London,
November 1986 p.48:

''Mwaka a 1986, miaka miwili kabla, baada ya takriban miaka ishirini na tano ya ukimya, Ally Sykes alikubali kufanya majadiliano na mwandishi wa Kiingereza kutoka Africa Events, Paula Park. Park akachapisha majadiliano aliyofanya na Ally Sykes kuhusu ukoo wa Sykes na mchango wao katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Makala ile iliposomwa Ally Sykes akawa anapata simu kutoka kwa marafiki zake na kwa wafanyabiashara wenzake wakitaka uhakika kama yale yaliyoandikwa katika gazeti lile kweli yeye ameyasema. Haukupita muda mrefu, maofisa wa Idara ya Uhamiaji walimtembeleaPark na kumuomba aondoke nchini.''
Kutoka kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''

Sasa hebu unganisha hii ilipate mtiririko anza na historia ilipotaka
kuandikwa na Abdul Sykes na Wilbert Klerruu, kisha njoo na kisa
cha Hassan Upeka alipolipa jopo la Kivukoni College ''notes'' za Abdul
Sykes
kuhusu TAA na TANU na huu mkasa wa Paula Park.

Hapa sijaweka makala yangu, ‘In Praise of Ancestors’ Africa Events, London,
March/April 1988, pp. 37-41, makala iliyosababisha toleo zima likusanywe
lisisomwe.

Kisa nini?
Jibu nawaachia Nguruvi3 na Yericko Nyerere.

Kuna mengine ingieni hapa:
Mohamed mimi sijaandika historia ya Kivukoni, TANU, Kicheba, Magoroto au Magila. Majibu niyatoe wapi?
 
Kwenye huu mjadala
Yeriko ni mdini na nguruvuvi pia maana hawajibu hasa kwa nini hostoria ya waislamu ilifichwa na sababu gani ilifanywa historia yao ificha
Kwanza, sikuandika historia yoyote, unaponitaka nikupe majibu unanionea.

Pamoja na hayo rejea bandiko 170 utapata majibu ya maswali yako kwa kina na ufasaha.
Lau kama hutaelewa au kuona majibu yako, sina namna ya kukusaidia kwa sasa

Ama kuhusu udini sikujua mjadala huu ni wa dini, kama ndivyo nitaomba nikae pembeni

Ninashiriki mijadala inayonifungua akili bila kujali asili yake bali mantiki na hoja zake

Kuna aina kadhaa za wasomaji
Wapo wanaosoma ili kuelewa. Wapo wanaosoma ili kuburudika

Kuna aina za wazungumzaji
Wapo wanaotaka kuzunguza unachotaka wewe kukisikia
Wapo wanaozungumza wanachotaka kukumabia wewe na si unachotaka kusikia

Katika makundi hayo, unaweza kujipima na kuchukua nafasi yako. Hiyo ni hiari yako

Kwa ushauri tu, elimu ni bahari, ukitaka kufaidika ni kusoma kutoka kwa wenzako, kudadisi , kuhoji na kutoa hoja. Ukisoma tu kama burudani utaburudika sana hutaelimika

Ungefuatulia mijadala na Mohamed Said ungenufaika na mengi kama tulivyonufaika na kama Mohamed alivyonufaika na hoja zetu. Hiyo ndiyo elimu

Historia ni mjumuiko wa matukio, dini iwe za asili au ziwazo ni sehemu yake.
Hivyo kujadili historia kwa muktadha wa matukio kama ya dini hakuna tatizo.

Tatizo ni kuangalia historia kwa jicho la dini na hapo ndipo utajikuta unakaa kitako kuhadithiwa kila siku. Utajenga uzio wa michongoma katika kichwa bila sababu
 
Nguruvi3 na Mtanganyika,
Tutakuwa tunakwenda na kurudi palepale.
Duara la ''merry go round.''

Kitabu sasa kipo mwaka wa 20 yaani miongo miwili na nakala ya Kiingereza
tuko toleo la pili na la Kiswahili toleo la tatu.

Kitabu kimeingia katika ''reviews,'' ndani ya Cambridge Journal of African
History.

Wote waliokipitia wamesema kitabu kimekuja na habari mpya na imeongeza
ufahamu wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kama nilivyosema, ''the untold story...'' hakika historia hii ilikuwa haijaandikwa.
Tena kitakuwepo hata baada yetu. Vipo vitabu vya mwaka 1300 miaka 20 si mingi

Kuingia katika review si kukamilika kwa historia, ni sehemu ya historia imeelezwa

Ni kweli kina habari mpya sijui nani anakataa hilo.
Nani alimjua Ayoub Kinyozi ? Nani alijua Nyerere alikwenda sokoni bila hela za mboga? n.k.

Yapo mengi umayaleta katika uso wa habari. Tunakushukuru sana

Ulikuwa karibu sana na familia ya Sykes ambayo umepata nyaraka za kutosha.
Je, hayo yanakamilisha historia?

Absolutely historia yako haikuwahi kuandikwa vinginevyo tungesema umefanya plagiarism, hakuna anayesema hayo.

Umeleta mengi yaliyokuwa hayajulikani. Je, ndio utimilifu wa historia?

Ninaamini yapo mengi tusiyoyajua na kadri muda unavyosonga tutayajua.

Akitokea mwingine akadunduliza, ni heri kwani kizazi kinabaki na faida.

Kwa mtu mwenye weledi wa kutosha, mnyenyekevu na mwingi wa hekima, kupokea maoni mbadala kwakwe ni faraja.

Asiyetaka kukosolewa, kushauriwa au kupewa maoni mara nyingi huwa na inferiority complex hali inayojitokeza kwa kitu tunachoita kitaalam grandiosity ambayo ni intrinsic
 
Hongera mzee wetu Muhammad saidi kwa kazi unayo ifanya mungu atakulipa ingawa unaitwa mdini usihuzunike kwa kuwa history iko hivyo inaonyesha waislam ni asilimia kubwa ndio walianzisha vugu vugu la kudai uhuru sasa ukisema kweli baadhi ya wakristo wenzangu hawapendi wewe tuelimishe dini yako baki nayo wewe sisi tupe history ili watoto wetu tuje kuwafundisha history ya kweli ya tanganyika
Mohamed bandiko 170 nilikueleza hatari unayoijenga. Hii hapa ni moja ya hatari hizo

Kwamba, walioanzisha vuguvugu la kudai Uhuru ni Waislam kwasababu ya wingi wao!!!
Pili, kwamba historia uliyoandika ni ya Waislam si ya Tanganyika kama unavyodai

Rejea bandiko 170 unisome kwa utulivu kabisa halafu umsome isk kisha ukanushe kama nilichokueleza si hatari.
 
Ilikuwa mwaka 1927 ndipo chama cha AA kiliundwa kwa msaada wa Gavana wa Kiingereza nchini Tanganyika Sir Roland Davidl Cameron na Dr Agrey raia wa Ghana mwenye mtaa Kariakoo ya leo, huyu Mghana alikuwa mshauri wa kisheria na kimuundo tu, kikawa kinafanyia shughuli zake nyumbani kwa Rais wa kwanza wa AA bwana Cecil Matola kutoka kabila la wayao, na miaka mitatu baadae, yaani 1930 ndipo wakapata jengo toka kwa Gavana Donald Cameron, hapo ndipo picha hii ilipigwa,

Mwaka 1933 Cecil Matola alifariki dunia, na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa AA Bwana Kleist Sykies (ambae baba yake mzee Platanta alikuwa ni muhamiaji haramu toka Afrika Kusini aliyefika Tanga na kuanzisha makazi huko baada ya kuwa mateka wa wajerumani vita ya kwanza ya dunia), mpaka mwaka 1948 chama kilipobadilishwa jina nakuwa TAA chini ya Rais wake Daktari Vedasto Kyaruzi (Mhaya),

Hapo Rais wake wa kwanza wa TAA akawa Daktari Vedasto Kyaruzi, na katibu akawa Abdulwahid Klest Sykies, miaka miwili baadae, Dr Kyaruzi alihamishiwa Kingolwila hivyo nafasi ya urais wa AA ikakaimiwa na Abdulwahid Kleist Sykies hadi ilipofika uchaguzi wa 1953 ambao Julius Nyerere alimshinda Abdulwahid Kleist Sykies kwakishindo na kuwa Rais wa TAA, Mwaka mmoja baadae Julius Nyerere alibadilisha jina na mrengo wa TAA nakuwa TANU ya kupigania uhuru kutoka chama cha kuratibu shughuli za starehe za weusi (chama cha walevi)

................................................................ Yote kwa urefu yamo katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,

View attachment 544629

View attachment 544695

Unapotosha Historia sijui Kwa maslahi ya nani hebu jaribu kuzungumza ukweli rejea hotuba za Mwalimu jinsi alivyo pata kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa taa Leo unasema Baba yake sykies alikuwa muhamiaji haramu unamaanisha nini kusema alikuwa muhamiaji haramu??? Ukiwa na reference gani halafu hapo hapo unasema alitekwa na wajerumani na kupelekwa Pangani. Inaonyesha jinsi gani Mwandishi ulivyobias na huwezi ukawa Mwana history katafute forum nyingine ya kudanga sio humo na hata huyo publisher wa kitabu chako nadhani naye anajichafua Kwa kujaribu kupindisha history
 
Mohamed Said ukweli hujidhiri, Boywise kajiunga 2017 March 20.
Mimi nawewe tumekuwa katika mjadala mzito kuanzia 2011
Boywise anachouliza hakinigusi ndiyo maana bandiko 170 nimemueleza kwa utulivu na kina

Utakumbuka wakati unaanza mjadala, niliwahi kukuuliza maswali.
Ikiwa leo hii simba wanakula wanadamu Rufiji, miaka ya nyuma Mshume aliwezaje kusalimika na hilo katika kueneza TANU?

Ikiwa baraza kuu la Tanu liliundwa na asilimia 98 Waislam, nini kilitokea asilimia 2 ikazidi nguvu 98?

Tulikuuliza, ikiwa Kleist Sykes alianzisha AA nafasi ya Mwalimu Cecil Matola ilikuwa wapi?

Tukauliza ikiwa Abdul Sykes alimpokea Nyerere alipoingia Dar kwa mara ya kwanza, ni ukweli kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza?

Orodha ya maswali ni ndefu ambayo hayakuwa na majibu.

Hii maana yake ni kuwa kuandika hakuaaminishi ni kukamilika kwa historia kwani wewe si alpha na Omega. Historia ya Uingereza inasomwa na inaandikwa seuse ya Abdul

Hakuna mtu aliyakataa kushiriki kwa familia ya Sykes au nyingine.

Tulichokataa ni kutaka kumtumia Mwalimu kwa kumlinganisha na Abdul.

Kwamba ukuu wa Abdul hautimii bila mwalimu. Kama utakumbuka tulikueleza watu hao ni tofauti kwa sifa zao, kuwalinganisha si kuwatendea haki na hasa Abdul

Tofauti inayokutia maudhi ni wewe kutaka hadhira ya 'hewalaa, ndiyoo'. Hilo hapana

Unakukumbuka elimu uliyopata hapa kwa hoja za mantiki na nzito
Nikupe mfano, elimu ya utafiti wa takwimu ambayo tunakushukuru umetuelewa

Nguruvi3,
Cecila Matola
alikuwapo pamoja na wazalendo wengine kwenye kitabu
cha Abdul Sykes nimeorodhesha majina yote ya waasisi wa African
Association:

Kleist Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, brahim Hamis, Zibe
Kidasi, Ali Said Mpima Suleiman Majisu, Raikes Kusi, na Rawson
Watts.

Mshume Kiyate
si aliyeijenga TANU Rufiji bali ni Said Chamwenyewe
aliyekuwa akipanda baiskeli kutoka Dar es Salaam hadi hadi Rufiji.

Ikiwa unaamini kuwa wanaoliwa na simba ni wapanda baiskeli barabarani
mimi sina la kusema lakini hiyo ndiyo historia ya Said Chamwenyewe na
alikwenda Rufiji baada ya kuagizwa na Abdul Sykes nakuwekea mkasa wake:

''TANU ilipata tasjili yake tarehe 30 Novemba, 1954 baada ya kuzishinda hila nyingi na vizingiti vilivyowekwa na serikali za kupinga usajili wake. Bi Zainabu, mke wa Ally Sykes anakumbuka siku moja adhuhuri, jua lilikuwa kali, wakati Nyerere alipokwenda nyumbani kwao Mtaa wa Kipata (Siku hizi Mtaa wa Kleist) ambako Ally na kaka yake Abdulwahid walikuwa wakimsubiri atoke mjini alikokwenda kushughulikia tasjila ya TANU. Alipofika Nyerere alionekana amechoka taabani na mwenye wasiwasi. Alizama ndani ya sofa akaufunika uso wake kwa mikono yake na akakaa kimya kwa muda. Abdulwahid na Ally walikuwa wakimsubiri azungumze. Nyerere alikuwa na habari mbaya. Serikali ilikuwa imekataa kuisajili TANU. Nyerere aliwaambia kuwa serikali ilikataa kutoa usajili kwa sababu za kiufundi. Serikali ilidai kuwa TANU haikuwa na wanachama. Baada ya kufahamu kuwa serikali imekataa maombi ya TANU kwa kuwa ati haikuwa na wanachama wa kutosha, mithili ya onyesho la mchezo wa kuigiza unaokwenda haraka, Abdulwahid alitumia hekima na mara moja akamuomba Said Chamwenyewe aende nyumbani kwao Rufiji kusajili wanachama kwa ajili ya TANU. Rufiji ni sehemu ya Waislam watupu. Kwa ajili hii TANU haikuwa na tatizo la kuwapata wanachama. Kwa hakika wanachama wa mwanzo wa TANU walikuwa kutoka Gerezani na Rufiji.''

Hiyo Nyerere, ''mara ya kwanza,'' kupokelewa na Abdul Sykes sijui umeitoa wapi.
Angalia hapo chini Nyerere alivyoeleza vipi alikutana na Abdul Sykes:

''Katika hotuba ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, (wazee wa Kiislam waliomuunga mkono wakati wa kudai uhuru) aliyoitoa tarehe 5 Novemba, 1985 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Nyerere aliwaambia waliohudhuria kuwa Kasella Bantu ndiye aliyempeleka nyumbani kwa Abdulwahid na kumtambulisha. Hii ilikuwa mara ya kwanza Nyerere kuzungumza hadharani kuhusu kufika kwake Dar es Salaam na ilikuwa mara yake ya kwanza kuihusisha hadharani historia yake, ya TANU na jina la Abdulwahid.''

Hiyo orodha yako ya maswali sijapatapo kuiona tafadhali ilete na ikiwa ninayo majibu
In Shaa Allah nitajibu.

Umezungumza historia ya Uingereza sawa lakini kwa hii ya TANU hadi sasa hakuna
aliyeigusa tena baada ya mimi kuiandika kwa kutumia Nyaraka za Sykes ambazo
sasa baadhi zimetiwa katika Kavazi la Mwalimu Nyerere.

Wala mimi sijapatapo kumlinganisha Abdul na Nyerere hata siku moja nilichofanya
ni kusema tu kama ni historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika mbona jina la Abdul,
Sheikh Hassan bin Amir
na wazalendo wengine hayamo kwenye historia ya uhuru?

Sijapatapo, ''kuudhika,'' kwa kupingwa kitabu changu.
Sana, sana nafurahi kwani inanifanya mimi kuwa na nafasi ya kueleza mengi kwenu.

Sijaelwa unakusudia nini kuhusu elimu ya ''takwimu.''
Ingia hapo chini kuna ya ziada:

Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
 
Mohamed bandiko 170 nilikueleza hatari unayoijenga. Hii hapa ni moja ya hatari hizo

Kwamba, walioanzisha vuguvugu la kudai Uhuru ni Waislam kwasababu ya wingi wao!!!
Pili, kwamba historia uliyoandika ni ya Waislam si ya Tanganyika kama unavyodai

Rejea bandiko 170 unisome kwa utulivu kabisa halafu umsome isk kisha ukanushe kama nilichokueleza si hatari.
Nguruvi,
Hatari ipi?

Hebu fafanua.
 
Tena kitakuwepo hata baada yetu. Vipo vitabu vya mwaka 1300 miaka 20 si mingi

Kuingia katika review si kukamilika kwa historia, ni sehemu ya historia imeelezwa

Ni kweli kina habari mpya sijui nani anakataa hilo.
Nani alimjua Ayoub Kinyozi ? Nani alijua Nyerere alikwenda sokoni bila hela za mboga? n.k.

Yapo mengi umayaleta katika uso wa habari. Tunakushukuru sana

Ulikuwa karibu sana na familia ya Sykes ambayo umepata nyaraka za kutosha.
Je, hayo yanakamilisha historia?

Absolutely historia yako haikuwahi kuandikwa vinginevyo tungesema umefanya plagiarism, hakuna anayesema hayo.

Umeleta mengi yaliyokuwa hayajulikani. Je, ndio utimilifu wa historia?inafsi

Ninaamini yapo mengi tusiyoyajua na kadri muda unavyosonga tutayajua.

Akitokea mwingine akadunduliza, ni heri kwani kizazi kinabaki na faida.

Kwa mtu mwenye weledi wa kutosha, mnyenyekevu na mwingi wa hekima, kupokea maoni mbadala kwakwe ni faraja.

Asiyetaka kukosolewa, kushauriwa au kupewa maoni mara nyingi huwa na inferiority complex hali inayojitokeza kwa kitu tunachoita kitaalam grandiosity ambayo ni intrinsic

Nguruvi3,
Sijasema imekamilika historia ya TANU.

Kwenye kitabu cha Abdul Sykes nimesema historia ya TANU inahitaji utafiti zaidi
na nyaraka zake nyingi zimo katika mikono ya watu binafsi.

Unaweza kufanya kejeli kwa Mzee Kinyozi na Mshume Kiyate lakini Mshume
Kiyate
ndiyo huyu hapo chini na Baba wa Taifa:

N0K7HwrXLn9yn-vuUI6CcDhAy_JxngLb32-lpGzC6ED8VsBAnTOAf5QblFdleHTHcegdAhjuCRQwms63fYIHXkoNe-5su2JIfo8SlFBkhgzq13_J38vjywAbVMp43w8kavLWb0RIgQtt_pAmKsjNF_B6v9I87vAsnoCybn0Z3PNYHLCi5JB38mjxUBHURbzH319O_uZHZWZ5-AYnor9G_OyVW0bX_dm-40L1ByAEVqgeHbdxYvNyBijXfjt6wuAASaDyEJLC42750iaxkgPusUVgtyJ3NgC845Ze_hfdl20CepaFzPM9F1bmIUIxpn8Q22ffJkJpp525sVaRme2bnYM1wY6M4gBRXFibk623qxtfdzc5NDOgajoV5eHst9YZDZE_Ye_HFlUSBKmcd53FSEAAassYipbDMiO6miGui4crZ65caceVHjSmHQQfuTlq6M6ltapInWYdm9u7RJShAE2f4Dux3ZnxMCfTpIWZQILaYFweh7W_6UIeEAadJLzk4Y9QYIscvpeenV29SevpM1HZuNnpLSIYwRn-5gLHOTAuImYT759bfj8eJhBdxuqkWuAGT-DeyNEEVENMUz0e5deslxVxPiSI-UX0Y7vDQAaKs0aZDVnlgVgv=w360-h480-no


''Baada ya maasi ya wanajeshi wa KAR tarehe 20 Januari, 1964, kuzimwa na Jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani. Mzee Mshume kwa niaba ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Nyerere kilemba kama ishara ya kumuunga mkono. Picha ya Mzee Mshume akimvisha Nyerere kilemba ilichapishwa katika magazeti mengi. Halikadhalika picha nyingine mashuhuri ya Mzee Mshume na Nyerere ni ile iliyopigwa Novemba 1962 wakati wa Uchaguzi Mkuu. Picha hiyo inamuonesha Mzee Mshume akiwa amevaa koti, kanzu na kofia amemshika Nyerere mkono akimsindikiza kupiga kura. Magazeti ya Chama na Serikali - Uhuru na Daily News yamekuwa yakiitumia picha hii kila baada ya miaka mitano katika uchaguzi wa rais kama njia ya kuwahamasisha watu kupiga kura na kumchagua Nyerere. Kwa bahati mbaya si chama wala magazeti hayo yamekuwa na ujasiri wa kuandika maneno chini ya hiyo picha kueleza lini picha hiyo ilipigwa na huyo aliyekuwa kwenye picha na Nyerere ni nani.''
 
"Mohamed Said, post: 22738039, member: 12431"]Nguruvi3,
Cecila Matola
alikuwapo pamoja na wazalendo wengine kwenye kitabu
cha Abdul Sykes nimeorodhesha majina yote ya waasisi wa African
Association:

Kleist Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, brahim Hamis, Zibe
Kidasi, Ali Said Mpima Suleiman Majisu, Raikes Kusi, na Rawson
Watts.
Hatari niliyosema kwa kijana irks ni kuaminisha watu kuwa umeandika historia ya Waislam. Kumbe basi historia ilikuwa na wengine wengi tu kuendelea

Kijana amesahau unazungumzia historia, yeye anazungumzia wingi wa Waislam tena kwa madai ya kwamba ndio walioanzisha vugu vugu la Uhuru.

Unless uniambie Uhuru una maana tofauti na kujikomboa kutoka katika ukoloni na kujitawala kijana wako utakuwa umempotosha Yarabi.
Uhuru ulianza kupiganiwa sehemu nyingi kwa namna nyingi

Ipo hatari nyingine, naiweka kiporo.
Hiyo Nyerere, ''mara ya kwanza,'' kupokelewa na Abdul Sykes sijui umeitoa wapi.Angalia hapo chini Nyerere alivyoeleza vipi alikutana na Abdul Sykes:
Wanakumbuka mjadala waje wakanushe kama si kweli Mohamed alisema Abdul ndiye aliyempokea Dar mwaka 1950. Tulikanusha hili kwa hoja
Hiyo orodha yako ya maswali sijapatapo kuiona tafadhali ilete na ikiwa ninayo majibu
In Shaa Allah nitajibu.
Swali la ilikuwaje Halmashauri ya TANU ilikuwa na wajumbe Waislam asilimia 98 na bado inaonekana walishindwa nguvu na asilimia 2 aliuliza Mzee Mwanakijiji , namuomba aje hapa anithibitishe au anikanushe.
Wala mimi sijapatapo kumlinganisha Abdul na Nyerere
Mohamed hivi hukumbuki hata maudhui ya kitabu chako mwenyewe? Tuvute kurasa ?

Siku zote unataka kumfanya Abdul na Familia ya Sykes kama ndio vinara wa Uhuru

Ni kweli walishiriki na ni kweli walikuwa na mchango kwasababu ya uenyeji wao

Hata hivyo huwezi kumweka Abdul na Nyerere katika mizani, ni watu wawili tofauti kabisa wenye sifa tofauti na hutamtendea haki Abdul
Sijapatapo, ''kuudhika,'' kwa kupingwa kitabu changu.
Maandiko yako yanaonyesha hasira, ukijinasibisha na kitabu kufanyiwa review Cambridge n.k. kama ishara ya kutuambia neno.

Tunasema hivi ya Cambridge yaache huko tuongee ya Tanganyika maana mimi na wewe tunakijua kisamvu, mlenda na ng'onda.

Tunajua nini maana ya mboga hivyo kujua Nyerere alivyokwazikaje kupata vitoga hadi akasaidiwa na Mshume Kiyate
Sijaelwa unakusudia nini kuhusu elimu ya ''takwimu.''
I mean ulitumia historia kujenga hoja ya uonevu katika elimu kwa kile ulichokiita utafiti wa MSAUDI ambaye basically ulikuwa wewe na pengine wenzako

Ukabumba data za matokeo ukaleta jamvini.
Tukakuonyesha matundu yote na shukran hazijarudi jamvini labda huko Cambridge.

Kama unadhani sikutendei haki zirudishe tena tujadili, nikiwa nimekosea nitakuomba radhi, ukiwa umekosea tumeshakusameh kuanzia siku hizo.
 
Nguruvi 3,
Nacheka peke yangu kama mwehu.

Nilipokuwa naandika kitabu hiki sikudhani hata kwa mbali kama kitachoma nyoyo za watu kiasi hiki.

Kitabu sasa kina miaka 20 tunakwenda toleo la nne Kiswahili na Kiingereza toleo la tatu sasa mbona hamuandiki hiyo historia ya wazee wenu walivyopigania uhuru na kuanzisha TANU huko makwenu?

Kinakushindeni nini kuja na nyaraka za wazee wenu na mapicha ya wakati wa kudai uhuru?

Nyie si ndiyo mmejaa History Department Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mbona hamna lolote la kuonyesha kuhusu historia mnayodai ndiyo ya kweli kama unavyoeleza?

Naitaja sana Cambridge Journal of African History kwa kuwa najua nini maana ya kitabu kuingizwa humo.

Ikiwa wewe hujui waulize waalimu wa historia katika vyuo vyetu.

Wengi hadi wanastaafu hawakuweza kuwa na "publication" humo.

Nakukumbusha umesahau kuitaja mihadhara yangu University of Iowa, Northwestern University, Chicago, Zentrum Moderner Orient, Berlin, University of Ibadan na Johannesburg na kwengineko.

Umeghafilika kutaja miradi niliyoshirikishwa na Oxford University Press New York na Nairobi na kazi zangu walizochapa na zinasomwa kote ulimwenguni.

Unakijua nilichokiandika humo?

Jitulize waache niliowalaumu kwa dhulma hii wanijibu.

Wao wamekuwa kimya miaka mingi lakini sasa kuna mradi wa kitabu na wamefanya mahojiano nami na nimewapa picha na nyaraka nyingine wameziweka katika Kavazi la Mwalimu Nyerere na wamenitaja na kunishukuru.

Pilipili iko shamba wewe unawashwa na nini mjini?

Mmejaa hasad na wivu katika nyoyo zenu mnataka hata kile kisicho chenu kiwe chenu.

Kama una uwezo na wewe andika acha kunibughudhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pilipili iko shamba wewe unawashwa na nini mjini?
Mmejaa hasad na wivu katika nyoyo zenu mnataka hata kile kisicho chenu kiwe chenu.

Kama una uwezo na wewe andika acha kunibughudhi.
Tutasoma na kama watu wenye upeo wa kuelewa tutaleta fikra katika maandishi yako. Hakuna bughudha isipokuwa rekodi sawa

Mohamed unajua kurudia jambo mara nyingi kwa lugh yetu sisi wataalam ni obsessions.

Hivyo ukiulizwa swali unajibu swali siyo kutuleta makala za kitabu ambacho kipo twaweza kusoma
Kila siku unaulizwa maswali simple unaleta hadithi ndeefu unnecessarily, please usiturudishe mduara.

Kauli ya kujibizana na mtu ukahisi unajibizana na watu 100 kwa lugha yetu ya kitaalam tunaita 'paranoia'.
Yaani unahisi kuna watu wanakufuata au ''kukushambulia'' na umesema hili hata kama huna ushahidi

Swali: Ikiwa Halmashauri kuu ya TANU ilikuwa na 98% Waislam, nini kuandikana kuweka mambo mengine sawa ?
 
Kama una uwezo na wewe andika acha kunibughudhi.
Hakuna bughudha Sheikh, lete zile takwimu za shule za Dar na chuo kikuu tuzijadili

Zile ndizo bughudha haswa, takwimu ndizo zinakubudhi si mimi

Tuendelee na mnakasha

Swali, tuonyeshe katiba ya chama chochote cha siasa kabla ya ile aliyotoa Mwalimu Nyerere!
 
Back
Top Bottom