Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Yericko hujui kitu katika historia hii wewe unajisemea tu.

Sykes Mbuwane kaingia Tanganyika akiwa Muislam na alikuwa na nduguye kipofu wamekuja pamoja anaitwa Ali Katini.

Ramadhani Mashado Plantan kaingia Tangnayika 1905 akiwa na umri wa miaka 5 akiwa Muislam.

Hakika nahadhiri kwingi duniani na nashirikishwa katika miradi ya historia ya Afrika kwa kupewa mialiko.

Ningekuwa natukana hakuna chuo wala taasisi kingenipa heshima wala wasingechapa vitabu vyangu.

Bado nakusisitizia usome.

Sent using Jamii Forums mobile app
MZEE SAID MOHAMED NI MSOMI MZURI! HILO HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED NI MFUATILIAJI MZURI WA MAMBO! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED NI MDINI MKUU! ANAYETAKA KUSILIMISHA HISTORIA YA NCHI YETU NZURI! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED NI KIPOFU WA KUDHANI NI YEYE PEKEE ANAJUA HISTORIA YA NCHI HII ! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID ATABAKIA KUWA MBISHI NA MZEE ASIYETAKA KUJIFUNZA TENA KUTOKA KWA VIJANA CHIPUKIZI KAMA KINA YERICKO NYERERE! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED HANA UWEZO WA KUANDIKA KITABU HURU BILA KUUTAJA NENO UISLAM/MUISLAM!HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED MUNGU AMJALIE AIJUE KWELI YOTE! ILI AWEKWE HURU! HILI TUNASEMA INSHALLAH!
 
Ungelitambua hilo usingetembea dunia nzima ukiwatukana... Hivi Kleist Sykes asingebadili dini yake ya ukristu kisa mwanamke akawa muislamu leo ungemlilia kila kona ya ulimwengu? Mbona Cecil Matola humsemi wala kumuenzi zaidi ya kumfifisha ilihali yeye ndie mwasisi wa vyama Tanganyika?
BRAZA UNAWEZA! UTAKUWA BORA ZAIDI! KWA SABABU KATIKA KUFUATILIA MAANDIKO YAKO! HUMU NA FACEBOOK! NAONA 'DOUBT' NDANI YAKO! KATIKA MAENEO MENGI UNAHOJI NA KUONESHA WAZI KUWA HUKUBALIANI MOJA KWA MOJA MAMBO MENGI ! YOU HAVE A GREAT CURIOSITY! ANDIKA ANDIKA!ANDIKA!MENGINEUTAKUWA UNAJIFUNZA MBELE KWA MBELE!
 
MZEE SAID MOHAMED NI MSOMI MZURI! HILO HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED NI MFUATILIAJI MZURI WA MAMBO! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED NI MDINI MKUU! ANAYETAKA KUSILIMISHA HISTORIA YA NCHI YETU NZURI! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED NI KIPOFU WA KUDHANI NI YEYE PEKEE ANAJUA HISTORIA YA NCHI HII ! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID ATABAKIA KUWA MBISHI NA MZEE ASIYETAKA KUJIFUNZA TENA KUTOKA KWA VIJANA CHIPUKIZI KAMA KINA YERICKO NYERERE! HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED HANA UWEZO WA KUANDIKA KITABU HURU BILA KUUTAJA NENO UISLAM/MUISLAM!HILI PIA HALINA SHAKA!
MZEE SAID MOHAMED MUNGU AMJALIE AIJUE KWELI YOTE! ILI AWEKWE HURU! HILI TUNASEMA INSHALLAH!
Mnabuduhe,
Umetumia herufi kubwa tupu.
Katika uandishi ukifanya hivyo maana yake unapiga kelele yaani unabwata.

Nadhani hili unalijua.

Mimi nimeandika historia ya uhuru na kuonyesha nchango wa Waislam,
mchango ambao wanahistoria hawakuugusa popote kwa bahati mbaya
au kwa kudhamiria.

Kitabu changu kilipotoka kikawa kimekuja na taarifa mpya ambazo kabla
hazikuwa zinafahamika.

Sidhani kama kuna ubaya katika hilo.

Ikiwa iko kweli nyingine zaidi ya hiyo historia iliyodumu kuanzia 1961 hadi
1998 kilipochapwa kitabu cha Abdul Sykes, na iandikwe watu wasome na
kufaidika kama walivyofaidika na kitabu changu.

Hilo la kuwa sitaki kujifunza kutoka kwa vijana chipukizi si kweli napenda
elimu sana na popote nitakapoikuta ni kama kitu changu kilichonipotea,
nitakichukua.

Hili la kuwa mimi naijua historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika hili
sikatai sidhani kama nina mpinzani katika hili.

Kwa ajili ya ujuzi huu nimeshiriki katika miradi mikubwa miwili ya Harvard
na Oxford na wamechapa kazi zangu na hivi sasa zinasomwa kwenye vyuo
vyote duniani vinavyosomesha African History.

Si hilo tu wamenialika hata kuzungumza katika vyuo vyao Marekani, Ujerumani
na sehemu mbalimbali Afrika.

Kuhusu udini ikiwa wewe unaniona hivyo siwezi kukuzuia lakini ukweli ni kuwa
nauthamini Uislam kama watu wengine wanavyothamini imani zao.
 
Historia inaonyesha asili ya kiswahili ni Pwani. Wamanyema wametoka Kongo kama sijakosea

Hili ningeomba mwenye ufahamu atueleweshe, hivi ni kweli hakuna lugha ya Kimanyema?
Na je ni kweli kuwa lugha ya kimanyema ni kiswahili!

Nikirudi kwa Mohamed, uwepo wa Kilungwana tu unatosha kuonyesha kitu tofauti na kiswahili

Hii ni orodha ya makabila (125) ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani.

1. Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
2. Waakiek
3. Waarusha
4. Waassa
5. Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang'ati)
6. Wabembe
7. Wabena
8. Wabende
9. Wabondei
10. Wabungu (au Wawungu)
11. Waburunge
12. Wachagga
13. Wadatoga
14. Wadhaiso
15. Wadigo
16. Wadoe
17. Wafipa
18. Wagogo
19. Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
20. Wagweno
21. Waha
22. Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na Watindiga)
23. Wahangaza
24. Wahaya
25. Wahehe
26. Waikizu
27. Waikoma
28. Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
29. Waisanzu
30. Wajiji
31. Wajita
32. Wakabwa
33. Wakaguru
34. Wakahe
35. Wakami
36. Wakara (pia wanaitwa Waregi)
37. Wakerewe
38. Wakimbu
39. Wakinga
40. Wakisankasa
41. Wakisi
42. Wakonongo
43. Wakuria
44. Wakutu
45. Wakw'adza
46. Wakwavi
47. Wakwaya
48. Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
49. Wakwifa
50. Walambya
51. Waluguru
52. Waluo
53. Wamaasai
54. Wamachinga
55. Wamagoma
56. Wamakonde
57. Wamakua (au Wamakhuwa)
58. Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
59. Wamalila
60. Wamambwe
61. Wamanda
62. Wamatengo
63. Wamatumbi
64. Wamaviha
65. Wambugwe
66. Wambunga
67. Wamosiro
68. Wampoto
69. Wamwanga
70. Wamwera
71. Wandali
72. Wandamba
73. Wandendeule
74. Wandengereko
75. Wandonde
76. Wangasa
77. Wangindo
78. Wangoni
79. Wangulu
80. Wangurimi (au Wangoreme)
81. Wanilamba (au Wanyiramba)
82. Wanindi
83. Wanyakyusa
84. Wanyambo
85. Wanyamwanga
86. Wanyamwezi
87. Wanyanyembe
88. Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
89. Wanyiha
90. Wapangwa
91. Wapare (pia wanaitwa Wasu)
92. Wapimbwe
93. Wapogolo
94. Warangi (au Walangi)
95. Warufiji
96. Warungi
97. Warungu (au Walungu)
98. Warungwa
99. Warwa
100. Wasafwa
101. Wasagara
102. Wasandawe
103. Wasangu (Tanzania)
104. Wasegeju
105. Washambaa
106. Washubi
107. Wasizaki
108. Wasuba
109. Wasukuma
110. Wasumbwa
111. Waswahili
112. Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
113. Watongwe
114. Watumbuka
115. Wavidunda
116. Wavinza
117. Wawanda
118. Wawanji
119. Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
120. Wayao
121. Wazanaki
122. Wazaramo
123. Wazigula
124. Wazinza
125. Wazyoba
 
U
Mnabuduhe,
Umetumia herufi kubwa tupu.
Katika uandishi ukifanya hivyo maana yake unapiga kelele yaani unabwata.

Nadhani hili unalijua.

Mimi nimeandika historia ya uhuru na kuonyesha nchango wa Waislam,
mchango ambao wanahistoria hawakuugusa popote kwa bahati mbaya
au kwa kudhamiria.

Kitabu changu kilipotoka kikawa kimekuja na taarifa mpya ambazo kabla
hazikuwa zinafahamika.

Sidhani kama kuna ubaya katika hilo.

Ikiwa iko kweli nyingine zaidi ya hiyo historia iliyodumu kuanzia 1961 hadi
1998 kilipochapwa kitabu cha Abdul Sykes, na iandikwe watu wasome na
kufaidika kama walivyofaidika na kitabu changu.

Hilo la kuwa sitaki kujifunza kutoka kwa vijana chipukizi si kweli napenda
elimu sana na popote nitakapoikuta ni kama kitu changu kilichonipotea,
nitakichukua.

Hili la kuwa mimi naijua historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika hili
sikatai sidhani kama nina mpinzani katika hili.

Kwa ajili ya ujuzi huu nimeshiriki katika miradi mikubwa miwili ya Harvard
na Oxford na wamechapa kazi zangu na hivi sasa zinasomwa kwenye vyuo
vyote duniani vinavyosomesha African History.

Si hilo tu wamenialika hata kuzungumza katika vyuo vyao Marekani, Ujerumani
na sehemu mbalimbali Afrika.

Kuhusu udini ikiwa wewe unaniona hivyo siwezi kukuzuia lakini ukweli ni kuwa
nauthamini Uislam kama watu wengine wanavyothamini imani zao.

Uniwie radhi kwa kubwata!
lakini Ukisoma kitabu kilichohaririwa na John Illife cha Modern Tanzanians - Utaona mchango mkuu wa watanzania wengi bila kujali imani zao walivyopigania kuundwa kwa taifa letu! Uwe unawataja wote. Godfrey Kayamba,Mwl. Steven Mhando.n.k
Soma pia kitabu cha Mzee Erasto Mbwana Mang'enya - Discipline and Tears. Chukua jumla yao uje na historia ya wapigania Uhuru isiyo na picha ya Udini.Kuna Unsung Heroes wengi tu! Kuwatukuza waislam na Kuwashusha wengine sio sawa!
Hata ukisoma kitabu chako cha Uamuzi wa Busara wa Tabora,Ukifuatilia Interview yako na Mr. Gunze wa Radio Butiama marekanI ! mimi naona unapelea unapoanza kujisabisha na udini katika historia isiyo na udini!
Kwa hakika kabisa wazee hawa wangalikuwa na fikra kama zako tungechelewa sana kupata uhuru.
Walishikamana pamoja bila kujali imani zao!
Wasaalam.
 
Yericko Nyerere, ni kweli sikuwa nimeuona huu mnakasha wala kuufuatilia na hivyo asante sana kwa kunishtua! Ngoja nisome taratibu yaliyojiri na kama nitakuwa na chochote cha kuongezea nitachangia.

Kawaida yangu ni kwamba kabla sijasoma michango yote ya awali sitakuwa nimeitendea nafsi yangu haki nikivamia tu bila kujua mnakasha ulipoanzia, ulipo na unakoelekea...siko hivyo. Hongera kwa kuandika kitabu.
 
Umemkusudia Martin Kayamba.
Unajitisha bure pasi na sababu.

Vitabu vyote hivyo vipo katika, ''bibliography,'' ya kitabu cha Abdul Sykes.
Hao, ''unsung heroes,'' ndiyo mimi nimewafufua katika kitabu changu.

Historia ilikuwa ishakamilika na hapakuwa na tegemeo kuwa itaandikwa
historia nyingine nje ya hiyo historia rasmi.

Mchango wa Waislam katika historia ya Tanganyika ni somo lililostahili utafiti
maalum na hicho ndicho nilichofanya.

Bahati mbaya kwa watu kama wewe kuwa nilipomleta Abdul Sykes katika
historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika mengi yamebadilika.

Nakuunga mkono kuwa kweli wazee wangu walishikamana na wakajenga umoja
lakini unajua yaiyowakuta baada ya uhuru?

Unaijua historia ya Sheikh Hasan bin Amir au Sheikh Suleiman Takadir?
Unajua kwa nini jwa nini historia ya wazalendo hawa iliwaogopesha wengi
walioingia katika uongozi wa TANU baada ya uhuru?

Mimi sijamshusha yeyote.

Waliowashusha wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika ni hao waliandika
historia nzima wakayafuta majina ya Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman
Takadir, Tatu bint Mzee, Bilali Waikela, Idd Faiz Mafungo
kwa kuwataja
wachache.

Sasa sijui udini unaingiaje hapa kwa mtafiti kufanya masahihisho ya historia ya TANU
iliyochakachuliwa.

Hivi ushajiuliza kwa nini imechukua zaidi ya miaka 50 Abdul Sykes na mdogo wake
Ally kupewa medali kama mashujaa waliounda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika?

Hebu ingia hapo chini:
Mohamed Said: UTATANISHI KATIKA HISTORIA YA TANU
 
Yericko Nyerere, ni kweli sikuwa nimeuona huu mnakasha wala kuufuatilia na hivyo asante sana kwa kunishtua! Ngoja nisome taratibu yaliyojiri na kama nitakuwa na chochote cha kuongezea nitachangia.

Kawaida yangu ni kwamba kabla sijasoma michango yote ya awali sitakuwa nimeitendea nafsi yangu haki nikivamia tu bila kujua mnakasha ulipoanzia, ulipo na unakoelekea...siko hivyo. Hongera kwa kuandika kitabu.
Nakushukuru sana mzee wangu kwakuitika na kuja, kwahakika umeongeza nguvu ya baraza letu...

Nashukuru pia kwa pongezi yako juu ya kitabu hiki, kwa sehemu kubwa wewe na Nguruvi3 ndio mlionisukuma nikachukua hatua za kuandika kitabu hiki ili kuweka sawa upotoshaji wa mzee wetu Mohamed Said, nashukuru kwa kiwango fulani nimeweka sawa sehemu alizojaribu kupotosha na sehemu alizonifunza nimemtendea haki kwa kumshukuru..
 
Yericko,
Unasema kitabu hiki cha ''Ujasusi...'' ndicho kitasahihisha kitabu cha Abdulwahid
Sykes
?

Kwani kitabu chako ni kitabu cha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika au ni
kitabu kuhusu ujasusi?

Naomba nikurudishe siyo kwangu bali kwa Ally Sykes ambae kadi yake ya TANU
ni no. 2 kadi ya Julius Nyerere ikiwa no. 1 na Abdul Sykes no.3.

Msikilize Ally Sykes anasema nini kuhusu historia ya Tanganyika katika utangulizi
wa mswada wake, ''Under the Shadow of British Colonialism in Tanganyika.'':

''...Kleist preserved this history through his own pen. And it is from that pen that many years after his demise we now have an accurate account of those long passed days. Before he died on 23 May 1949 my father left behind his memoirs in his long flowing German handwriting picked from a Germany school he attended in Dar es Salaam as a child in early 1900s. These memoirs [1] were later revisited by Abdulwahid, my elder brother, with his daughter Aisha Daisy Sykes, then an undergraduate student at Dar es Salaam University under the tutelage of John Iliffe, the renowned Cambridge -educated historian. A month before he died on 12 October 1968 Abdulwahid had already assisted Daisy to complete her research assignment of prominent Africans in Tanganyika for a history seminar on the life of her grandfather. The aim of this project was to document the life history of our father, Kleist Sykes, and his achievement in politics, education and business.

It was from his diaries, personal papers and with the assistance of Daisy that Iliffe was able to write accurately on African Association and early colonial politics.[2] Daisy’s work was submitted to the History Department of University of Dar es Salaam in September 1968. It was later published in 1973 in a book edited by Illife.[3] It is a pity that Abdulwahid, who was the main informant on the biography, did not live to see the published work. Prior to the publication of my father’s biography little was known about the founding fathers of the Tanganyika African Association.''

Ally Sykes
Dar es Salaam
24 March 1997

[1] A.D. Sykes “The Life of Kleist Sykes,” University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15.
[2] See John Illife: A Modern History of Tanganyika, Cambridge University Press, London, 1977; Also “The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Consciousness in Tanzania.” Mimeo, University of East Africa Social Sciences Conference 1968.
[3] Illife Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973.
 
Mzee Said Mohamed Shikamoo!
Godfrey H. Kayamba Ni Mjukuu wa Hugh Peter Kayamba,mtoto wa Martin Kayamba,Alibahatika kusoma enzi hizo za Ukoloni London School of Economics,Huyu ni mmoja wapo yawaliounda Tanga Discussion Group!( 1950s) Chini ya Katibu wao Peter Mhando.Godfrey Kayamba akishirikiana na member wenzake aliandika memorandum ya hatari sana iliyomtisha gavana wa Tanganyika wakati huo Twinning akafunga safari mpaka umoja wa mataifa kukanusha memorandum hiyo! Sehemu ya Memeorandum hiyo ilisomeka hivi "It is a sin to God on the part of the Colonialists to treat people as human guinea pigs...'' Historia ya Tanganyika haijakamilika na ninakubaliana na wewe kuwa kuna mashujaa wengi wameachwa aidha kwa makusudi ya watawala,au kwa bahati mbaya,au kwa kuwa wa Tanzania hatuna utaratibu wa kusoma ndio maana hatujaweza kuyaona yote! Ila MZEE unapotoka unapowakumbuka hawa Mashujaa wetu kwa kuwaita Waislamu!
Kimsingi mimi siuoni huo Uislam wa hao wazee mashujaa hata kidogo ( In Islamic teachings) kwa sababu waliwahi kumfanyia Julius Nyerere matambiko ya Kiswahili(Pwani) ambayo ni kinyume cha mafundisho ya Uislamu( Ni kosa kumshirikisha Allah na matambiko).
Ninancho acknowledge ni kuwa Wazee hao ni Mashujaa na Wazalendo wa kweli Watanganyika halisi ambao historia rasmi ya Tanganyika imewapita bila kutambua mchango wao.
Naomba kuwasilisha.
 
Mnabuduhe sijamsikia Godfrey Kayamba katika historia ya Tanganyika.

Mnabudehe,
Marahaba.
Tuanze na hili la Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sidhani kama huo mchango wa Godfrey Kayamba unaweza kufuta mchango mkubwa
wa akina Hamisi Heri, Mohamed Kajembe, Mmaka Omari, Sheikh Rashid Sembe
kwa kuwataja wachache.

Hii mosi.
Pili nimepitia katika utafiti wangu wa kitabu cha Abdul Sykes yale yaliyotokea katika
hiyo, ''memorandum,'' uliyoitaja hapo juu na nakuwekea kitu hapo chini ukiangalie:

''Britain was administering Tanganyika under articles 76 and 77 of the Charter of the United Nations. As the administering authority, Britain was expected to establish and promote political, economic and social advancement of Tanganyika until such time as its people were ready for self-rule. In spite of this international commitment, the British were more interested in safeguarding their own colonial interests and those of other minorities but-not those of the indigenous African majority. [1] In order to pre-empt African reaction to this injustice, in 1949 Governor Twining invited proposals from prominent individuals, welfare societies and from Native Authorities,[2] as to how Tanganyika should be governed. The TAA political committee submitted a memorandum to the Constitutional Development Committee which was signed by the entire executive: Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando and Said Chaurembo. [3] In his annual report for 1950, Abdulwahid was to write:

For the welfare of the Africans and to safeguard the interests of this Association and those of the African community as a whole, this Association has arranged for an advocate to stand by and to advise the Association on the technical side of the law. This advocate is Mr. E.E. Seaton of Moshi. He has from time to time written to the Association on various political subjects, and helped a great deal with his advices when this Association was compiling its memorandum on constitutional development. [4]

Abdulwahid realised that many of the problems in respect of the rights of Africans in the territory were legal issues which required the advice of legal experts. For the first time, with the help of Seaton, TAA was able to confront the colonial authority with facts and figures illustrating injustices in the colonial system which were contrary to the United Nations Charter.

In his analysis of the TAA memorandum to the Constitutional Development Committee, Pratt reported:

The most detailed African submission came from the Dar es Salaam branch of the Tanganyika African Association. It asked that the distribution of seats (i.e. an official majority and one-half of the unofficial to be African) should be held constant for the next twelve years and that in the thirteenth year a common electoral roll should be introduced with a majority of the council then being elected.[5]

Governor Edward Twining’s committee ignored TAA’s recommendations. The government continued with its long-term plans of strengthening the positions of minority Europeans and Asians in the political development of the territory while pushing aside the indigenous Africans contrary to the United Nations Charter. Many learned Africans were of the opinion that the TAA submission should have rightly formed the basis of the future constitution of the territory as a multi-racial society. But the spirit of that document did not die. It surfaced at the TANU founding conference on 7 th July, 1954 and was to form the basis of Julius Nyerere’s speech before the Trusteeship Council of the United Nations in New York in March, 1955. [6]

[1]For a detailed discussion on the subject see Cranford Pratt, The Critical Phase in Tanzania 1945-1968, Cambridge University Press, London, 1976, pp. 29-31.
[2]Ibid p. 30.
[3]The author was for the first time informed of the existence of this document by one of Mwapachu's children, Juma Volter Mwapachu. He was informed that Mwapachu took great pride in having participated in the drafting of this document. In her book Listowel mentioned this document and its historical significance to the political history of Tanganyika. But it was Pratt who analysed the document in detail. The document was first consulted by Pratt in 1959 in a file of the Committee on ‘Constitutional Development Report/and Despatches to the Secretary of State’ no. 1146-6, Dar es Salaam Secretariat Library. Although this file is available at the Tanzania National Archives, the document is missing. The author was informed that a microfilm of the document was available but that too could not be traced. For more information on loss of historical documents see M. Said, ‘In Praise of Ancestors Revisited’ in Africa Events, London March, 1989, pp. 50-51.
[4] Annual Report of the secretary of TAA, ibid.
[5] Pratt op. cit. p. 30.
[6] There are old men, TANU veterans, who believe to this day that the March 1955 speech by Julius Nyerere before the Trusteeship Council was written by Abdulwahid, and so was the constitution of Tanganyika. The author has come across this story several times in his interviews with early members of TANU. The reason for this belief is that the document was drafted by the TAA Political Subcommittee in 1950.

Mnabudehe,
Tuje katika nukta yangu ya tatu.

Umemsoma Pratt hapo juu na maelezo yake kuhusu hii memorandum.

Hajamtaja Godfrey Kayamba popote lakini inawezekana taarifa za Godfrey
Kayamba
zilimpita.

Sasa ili kuthibitisha nukuu hiyi ya Kayamba uliyoiweka hapa itakuwa bora
kama utaweka, ''citation,'' yake.

Mwisho ningependa kueleza kuhusu matambiko na Uislam.

Naamini wewe umefanya nukuu ya hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusu dua
aliyofanyiwa nyumbani kwa Jumbe Tambaza, Upanga.

Nyerere hawezi kupambanua kati ya dua na tambiko hana ujuzi huo.
Tujaalie kuwa walifanya dua na tambiko hii haiwatoi katika Uislam.

Nyerere mwaka wa 1958 alipata kushiriki katika dua nyingine kubwa kushinda
ile ya kumlani Edward Twining na dua hii ilifanyika Mnyanjani, Tanga na
ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur'an iliyosomwa na Sheikh Kombora.

Haya niliyokuwekea hapa na mengi mfano wa haya ndiyo yaliyofanya kitabu cha
Abdul Sykes kishinde historia zote zilizoandikwa kuhusu TANU na uhuru wa
Tanganyika.

Katika mhadhara niliofanya Northwestern University, Evanston Chicago kuhusu
mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni, msemaji mmoja alisema
kuwa walimjua kiongozi wa uhuru wa Tanganyika, Julius Nyerere kuwa ni Mkristo
lakini hawakujua kuwa nyuma yake kulikuwa na ''a strong Muslim Movement.''
 
Nguruvi3,
Kwanza napenda nikufahamishe kuwa mimi sina sababu yoyote ya kuwa na ''complex,''
kwa hiyo siwezi kuwa na sababu ya kudharau lugha ya Kimanyema.

Lakini ningependa kukueleza kuwa Kimanyema hakijapatapo kusemwa katika ardhi ya
Tanganyika..
Hili ni kosa kwasababu Wamanyema waliofika Tanganyika waliongea kilungwana kama lugha ya uungwana ambayo ni kiswahili ambacho ndani yake kuna kiarabu

Kudhani kuwa Umanyema si ustaarabu ni dhalili.
Ustaarab wa mtu upo katika lugha yake na si lazima lugha ya kuazima.

Tatizo la kupotea kimanyema linajieleza vema pale unaposema wewe ni Mswahili.
Unasema wazazi wako ni wana asili ya Kimanyema lakini wewe una asili ya 'Sahel'

Kama unaelewa Quran bila kuelewa kiarabu , unaweza kuwa mwislam bila kuwa mswahili.
Bado sijaona mantiki ya kukwepa Umanyema usio na athari kwa mila ya Ibrahim
 
Sitoweza kuwa utakavyo wewe.
 
Nguruvi3,
Sitoweza kuwa utakavyo wewe.
Wala nisingependa uwe tofauti na unavyojitambua

Nina uhakika wanaotusoma kuna kitu kinawashangaza hasa wakiona hoja za 'umanyema'
Kinachowaduwaza ni mahusiano ya Umanyema, Uislam, Uhuru na mada iliyopo

Ipo mantiki ya mambo hayo. Kwanza, Mohamed siku zote anaeleza mchango wa Waislam katika kupigania Uhuru.

Ni kweli mchango huo haupaswi kubezwa au kufutwa katika historia
Hata hivyo Mohamed anakuwa na ''jicho pembe'' kwa kutotambua michango ya wengine

Mohamed ana link Quran , Uislam na Kiswahili kwa makusudi kabisa.
Na hapa asiulize mtu tofauti ya Quran na Uislam, ieleweke ipo dhahiri

Mohamed 'anaukana' Umanyema kwasababu kujinasibisha nao kutaondoa ' uhalali' ;
1. Kwamba ni Wageni tu kama alivyokuwa Nyerere
2. Kwamba Umanyema ukiingia, basi kutakuwa na Udengereko, Uzaramo n.k.

Ukitaka kuandika historia kwa jicho la Udengereko, Uzaramo , Uluguru au Umanyema utakuwa umepunguza nguvu ya hoja ya 'Uislam na Uhuru'.

Ili kujenga hoja hiyo ni lazima 'kuua' hoja za makabila, kwa upande wake Umanyema

Hapo ndipo Mohamed anapata hoja ya kabila la Waswahili lenye mahusiano na lugha ya kiarabu iliyobeba Quran inayotumiwa na ''Waislam'' na iliyofanikisha Uhuru

Ndiyo maana lugha anyoijua ni Kiswahili na Kiarabu

Ni kwa ufupi tu
 
Nguruvi3,
Wamanyema sisi ni "Wakuja," na hili nimelieleza katika kitabu cha Abdul Sykes katika magomvi yaliyokuwa yakitokea kati ya babu zetu na wenyeji katika African Association.

Sijapatapo kuukana Umanyema.
Mimi ni Muyukwa Samitungo Mwekapopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom