Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mtanganyika ikiwa unaona napotosha njoo na historia unayoiamini tutaisoma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe Yericko Nyerere ni mpumbavu sana! Yaani nilikuwa nakuona kama mmoja ya vijana hazina ya taifa hili tukufu hapa jukwaani. Ila kupitia uzi huu umejivua nguo kabisa !Ungelitambua hilo usingetembea dunia nzima ukiwatukana... Hivi Kleist Sykes asingebadili dini yake ya ukristu kisa mwanamke akawa muislamu leo ungemlilia kila kona ya ulimwengu? Mbona Cecil Matola humsemi wala kumuenzi zaidi ya kumfifisha ilihali yeye ndie mwasisi wa vyama Tanganyika?
Ilikuwa mwaka 1927 ndipo chama cha AA kiliundwa kwa msaada wa Gavana wa Kiingereza nchini Tanganyika Sir Roland Davidl Cameron na Dr Agrey raia wa Ghana mwenye mtaa Kariakoo ya leo, huyu Mghana alikuwa mshauri wa kisheria na kimuundo tu, kikawa kinafanyia shughuli zake nyumbani kwa Rais wa kwanza wa AA bwana Cecil Matola kutoka kabila la wayao, na miaka mitatu baadae, yaani 1930 ndipo wakapata jengo toka kwa Gavana Donald Cameron, hapo ndipo picha hii ilipigwa,
Mwaka 1933 Cecil Matola alifariki dunia, na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa AA Bwana Kleist Sykies (ambae baba yake mzee Platanta alikuwa ni muhamiaji haramu toka Afrika Kusini aliyefika Tanga na kuanzisha makazi huko baada ya kuwa mateka wa wajerumani vita ya kwanza ya dunia), mpaka mwaka 1948 chama kilipobadilishwa jina nakuwa TAA chini ya Rais wake Daktari Vedasto Kyaruzi (Mhaya),
Hapo Rais wake wa kwanza wa TAA akawa Daktari Vedasto Kyaruzi, na katibu akawa Abdulwahid Klest Sykies, miaka miwili baadae, Dr Kyaruzi alihamishiwa Kingolwila hivyo nafasi ya urais wa AA ikakaimiwa na Abdulwahid Kleist Sykies hadi ilipofika uchaguzi wa 1953 ambao Julius Nyerere alimshinda Abdulwahid Kleist Sykies kwakishindo na kuwa Rais wa TAA, Mwaka mmoja baadae Julius Nyerere alibadilisha jina na mrengo wa TAA nakuwa TANU ya kupigania uhuru kutoka chama cha kuratibu shughuli za starehe za weusi (chama cha walevi)
................................................................ Yote kwa urefu yamo katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,
View attachment 544629
View attachment 544695
Kama hujui mjadala huu kaa kimya na sihitaji heshima yako kwangu...Wewe Yericko Nyerere ni mpumbavu sana! Yaani nilikuwa nakuona kama mmoja ya vijana hazina ya taifa hili tukufu hapa jukwaani. Ila kupitia uzi huu umejivua nguo kabisa !
Umeshindwa kihoja na mzee mohame said naona umekimbilia kwenye dini yake! Mtu mstarabu alitakiwa achukue yakujifunza nakuyafanyia kazi..! Ila wewe unayejifanya mjuvi wa mambo bado unaleta ubishani wa kitoto!
Pathetic!
Sent by Ubavu
Mtanganyika ikiwa unaona napotosha njoo na historia unayoiamini tutaisoma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Darsa ni kiswahili cha wapi? Hata kama neno lina asili ya kiarabu lakini baada ya kulikopa na kuliingiza kwenye matumizi lahaja yake imebadilika kuendana na lugha mpya ya kiswahili, hivyo tusione ni ufahari saaana kulitamka au kuandika kama waarabu walitamkavyo bali ni vyema tukalitumia kama watanzania wote tunavyolitumia neno hilo DARASA na sio DARSAChige,
Yericko hana kitabu wala nini...
Kkuandika hajui ataweza kuandika kitabu?
Hebu soma hili darsa nililomzawadia huko FB:
''Bado niko na wewe Yericko. Nimekuwekea darsa zima kuhusu uandishi wa vitabu. Meza kibri chako na soma na zingatia. Umesema uko Amzon lakini ukweli ni kuwa hawakujui huko. Mimi nimeingia Amazon toka mwaka wa 1998 kwa hiyo nawajua vyema. Kuna kitu lazima ukijue pia. Amazon hujipeleki. Amazon unapelekwa na ''publishers,'' na ''booksellers'' yaani wauza vitabu. Kuna kitu kinaitwa ''blarb'' katika kitabu. Haya ni maelezo nyuma ya ''cover,'' ya kitabu. ''Blarb,'' inaandikwa na ''publisher,'' si wewe Yericko. Huu ni ushauri wa bure wenzako wanalipia fedha. Mimi nakupa bure ili ujitoe katika ujinga.''
![]()
''Daisy baada ya kufariki baba yake mwaka wa 1968 alitaka kuandika kitabu cha maisha yake lakini mwalimu wake John Iliffe alimwambia somo hilo linataka muda haitakuwa vyema kwa yeye kufanya haraka. Daisy hakuandika kitabu kile na ikaja kuwa mimi ndiye Allah akanijaalia kukiandika kwa msaada mkubwa sana wa nyaraka za ukoo wake. Picha hiyo tumepiga April 2017 na Daisy ni huyo kashika kitabu cha maisha ya baba yake. Unaweza kumsoma Daisy katika hii, ''paper,'' yake: A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15). Inapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana.''
''Marafiki wa Mwalimu Nyerere na baadhi ya wasomi wameona ni bora baada ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes ambacho kwa namna moja au nyingine kimegusa maisha ya siasa ya Baba wa Taifa, na wao wafanye utafiti na iandikwe ''biography,'' ya Mwalimu Nyerere. Nimefanya mahojiano na wao nyumbani kwangu Magomeni Mapipa mara tatu na nimewapa nyaraka na picha nyingi sana kutoka kumbukumbu za akina Sykes. Mradi huu nadhani sasa uko mwaka wa nne. Wanaofanya utafiti huu ni Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman Yahya na Dr. Kamata.''
Chige,
Haya ndiyo yangu katika historia hii.
Mohamed kwani wewe unaweza kuzungumza lugha ngapi?Okaoni mimi nimezaliwa Dar es Salaam na kukulia Dar es Salaam sijapatapo kuzungumza lugha nyingine yeyote ila Kiswahili na nakisema kwa lafidh ya Pwani. Darsa ni mfano wa "lecture," hii ni tofauti na "darasa," yaani "class room."
Nguruvi,Mohamed kwani wewe unaweza kuzungumza lugha ngapi?
Sawa, kauli ya kwamba 'hujapato kuzungumza lugha nyingine zaidi ya kiswahili ilinishtua, kuna vitabu umeandika kwa kiingereza na huko unakokwenda sikuwahi kusikia una mkalimaniNguruvi,
Nazungumza lugha mbili Kiswahili na Kiingereza.
Nguruvi,Sawa, kauli ya kwamba 'hujapato kuzungumza lugha nyingine zaidi ya kiswahili ilinishtua, kuna vitabu umeandika kwa kiingereza na huko unakokwenda sikuwahi kusikia una mkalimani
Uliwahi pia kusema kama sitakosea kuwa asili yako ni Umanyema!
Kama ndivyo, wamanyema hawana lugha!
Pili, unafahamu kidogo wa lugha ya kiarabu?
Kwani walipotoka Umanyema walikuja na kiswahili?Nguruvi,
Nilikusudia kusema lugha nyingine hapa nyumbani kama ''dialect.''
Wamanyema wa Tanzania hawana lugha yao.
Sifahamu Kiarabu.
Umewahi kusoma Holy Quran ?Sifahamu Kiarabu.
Kwahiyo unataka kutuambia kuwa Wamanyema hawana lugha isipokuwa kilungwana? I mean hakuna lugha ya Kimanyema?Nguruvi waliingia Tanganyika wakizungumza, "Kilungwana," yaani Kiswahili.
Kuongea lugha kwa matamshi tofauti kunategemea asili zetu kuna watu hawawezi kutofautisha kati ya "r," na "l."
Historia inaonyesha asili ya kiswahili ni Pwani. Wamanyema wametoka Kongo kama sijakoseaNguruvi3,
Wamanyema wanasema Kiswahili ndiyo lugha yao. Hicho Kilungwana ni Kiswahili na hilo neno lilitumika zaidi ya karne mbili sasa wakati wanaingia Tanganyika
Na hapa naomba msaada nini tofauti ya Quran na ArabicNguruvi nasoma Qur'an.