Bwana Mohamed,Yericko,
Paskali...hapana hawezi.
Kitabu changu kimefurtu ada.
Mwaka wa ngapi nimesimama na nyie hapa?
Nyie mnauliza maswali na mie ndiye msomeshaji.
Mliyajua haya kabla ya mimi kuandika? Ila inanishangaza hii chuki katika uandishi wenu. Hii historia imewauma sana. Mngependelea tubakie na historia ya Chuo Cha Kivukoni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kifyatu ahsante kwa hayo yote. Ikhtikafu ni jambo la kawaida katika fikra. Kubwa nililotaka kufanya ni kusahihisha historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni.Bwana Mohamed,
Kwanza nikupe pongezi kwa maandishi yako yote yakijumuisha vitabu, scholarly papers kwenye majarida, na mabandiko yako humu JF katika kuweka vema historia ya unaowaita wazee wako, ambao pia ni wazee wetu sote.
Nimeyafuatilia kwa ukaribu sana malumbano kati ya fikra zako na zile fikra tofauti hapa JF kitambo sasa. Kwa maoni yangu nadhani huu ukakasi unaowafanya watu wapinge maandishi yako ni kwa sababu ya ulivyoumba (frame) hoja zako katika maandiko haya. Kuna tofauti kati ya maumbo haya mawili yafuatayo na yanatoa mafunzo mawili tofauti:
1. WAISLAMU waliopigania uhuru wa Tanganyika na kusahauliwa katika historia ya nchi.
2. WATANGANYIKA waliopigania uhuru wa Tanganyika na kusahauliwa katika historia ya nchi (wengi wao wakiwa Waislam).
Hizi framing mbili zitawazungumzia watu hao hao lakini kila framing inaleta somo tofauti na nyingine.
1. Framing ya kwanza inaleta hisia kana kwamba kulikuwa na Islamic Movement iliyopigania uhuru na baada ya uhuru wakatoswa. Hii inawagusa wengi zaidi ya ukoo wa Mohamed Said, Sykes, na wengine. Hii inaugusa Umma wote wa Waislam kijiuliza kulikoni.
Wanazuoni wanaposoma historia inayosema Waislamu ndio chanzo cha uhuru wa Tanganyika wanakuwa na maswali mengi. Kwa nini sasa Tanganyika siyo Caliphate? Iweje Sharia isiwe law of the land? .........n.k. kufikia kusema hatukubali nchi ya Waislam iendeshwe kikafir.......
Hapa ndipo panapowafanya wengi waseme maandiko yako yanaweza kuwa chimbuko la chuki za kidini.
2. Framing ya pili itakuwa inaweka wazi Watanganyika waliokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru na ambao wameachwa kuingizwa katika historia ya hii nchi. Na kwa kuwa wengi wao walikuwa wenyeji wa pwani mwa Tanganyika, hawa wazee walikuwa waumini wa dini ya KIISLAM.
Framing hii ingewaweka wazee wako (wetu) kwenye limelight na kwenye nafasi zao stahiki katika upiganiaji uhuru wa nchi hii bila kujenga hisia za dhulma za kidini.
Pengine wengine walikwishayasema haya na pengine mengi ulikwishayajibu. Kumradhi kama ni hivyo. Nimeona namimi nichangie pesa mbili zangu.
Historia inawafunza watu kilichotokea na kuwatayarisha leo na siku za usoni.
Ni funzo gani unalotaka kuwapa Watanzania wa leo na wa kesho kutokana na historia ulioandika?
Jukumu kubwa sana hilo kaka!
Sent using Jamii Forums mobile app
Unasahihisha kwa kufanya kosa zaidi? Huo sio usahihi maalimKifyatu ahsante kwa hayo yote. Ikhtikafu ni jambo la kawaida katika fikra. Kubwa nililotaka kufanya ni kusahihisha historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kituko,
Unatakiwa kunipongeza kwa kuandika historia hii.
Kituko siwezi kukuzuia kuamini unavyopenda. Kwangu muhimu ni kuwa nimeingiza katika historia ya TANU na Tanganyika mengi ambayo wengi hawakuyajua.Kaka kuna kitu umeandika, Kitu kizuri sana japo kina mapungufu makubwa pia, kuna mambo ya vijiweni na kuna vitu halisia, hao wote uliowaandika ni kweli walikuwepo, lakini kuna ukweli unaoukataa na kujaribu kulazimisha baadhi ya mambo, lakini bahati mbaya facts zinakataa, TABIA KUBWA YA UKWELI NI KUJISIMAMIA WENYEWE, maana kila unapoandika mwisho unajikuta unajitia kitanzi mwenyewe miguuni na unaanguka
Kituko,
Bahati mbaya umechelewa sana katika mjadala huu.
Haya maswali yako yote nimeyajibu hapa siku za nyuma na katika
kitabu nimeeleza sifa za Nyerere kuenea katika uongozi wa juu
katika TAA kisha TANU.
Ikiwa kweli unataka kujua jiepushe na lugha za kejeli mfano wa hii
''kumfundisha Kiswahili.''
Mimi naona tabu sana mambo kama haya.
Kituko siwezi kukuzuia kuamini unavyopenda. Kwangu muhimu ni kuwa nimeingiza katika historia ya TANU na Tanganyika mengi ambayo wengi hawakuyajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kituko hayo unayosema hivi sasa kuniambia mimi huko tulishapita ni bahati mbaya kuwa wewe umeyajua hayo hivi sasa.Kaka hivyo vitu vichache vya maana uliyoyaandika kuhusu AA, TA, TAA na TANU ni kama punje moja ya mchanga wa Baharini, kila mtu akiandika anachokitaka itakuwa ni fujo tu, na ndio maana uandishi wa Historia unakuwa na Historia rasmi na hii inapatikana baada ya kufanyika research ya kuangalia mambo gani ya msingi yanayopaswa kuwemo ndani ya hiyo historia inayoandikwa, Kama Nyerere kusaidiwa kitoweo na Mzee Kiyate ina uzito kweli wa kuwekwa kwenye historia? Nyerere kasaidiwa vingapi kila alipokuwa anapita?
Kituko nimesema hivyo kwa kuwa unauliza yale ambayo nilishajibu siku zilizopita. Sikutambua kama nina wasomaji wengi kiasi hiki. Alhamdulillah.Wala sijachelewa kaka, labda useme nimechelewa kuandika humu, lakini nipo tangu mnakasha unaanza na huu sio mnakasha wa kwanza kukusoma, kuna mnakasha ulikiwa mrefu sana humu JF ulianzishwa pia na huyuhuyu Yericko Nyerere
Mnabaduhe,
Umesema kweli lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa Uislam ulitumika sana.
Mkutano wa Kura Tatu ulifanyika Parish Hall lakini hiyo ni 1958 TANU ina
nguvu kila mtu anaifata sasa kwani walijua uhuru uko njiani.
Uliza ilikuwaje kabla ya hapo nikuwekee historia nzima kama nilivyoieleza
katika kitabu cha Abdul Sykes.
Yericko kazi yoyote ya mikono ya binadamu haikosi makosa na tutayarejea tena na tena na tena. Ukiliona kosa nifahamishe wala hapana sababu ya wewe kuandika kwa kisirani.Unasahihisha kwa kufanya kosa zaidi? Huo sio usahihi maalim
Kituko nimesema hivyo kwa kuwa unauliza yale ambayo nilishajibu siku zilizopita. Sikutambua kama nina wasomaji wengi kiasi hiki. Alhamdulillah.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kituko kila kona ya dunia katika vyuo.Kaka hiyo kauli ya "Sikutambua nina wasomaji wengi kiasi hiki" ni ya dhati ama maskhara?, maana kila siku unasema unasomwa kila kona ya Dunia iweje leo ushangae kuwa na wasomaji wengi?
Mzee MohamedWatu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking
Kuna hoja mbili kuhusu hili
1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam
Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali
2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir
Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.
Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.
Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole
3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.
Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki
1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.
Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10
Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine
Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii
Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.
Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?
Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!
Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.
Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia
Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
Boywise...ndugu zetu wamechomwa sana na kitabu hiki kwani kimebadili historia yote ya TANU na harakati za kudai uhuru.Mzee Mohamed
Ni sawa kusema kuwa hao waliofanya review kitabu chako hawajui 'critical thinking'?
Sent using Jamii Forums mobile app
Boywise...ndugu zetu wamechomwa sana na kitabu hiki kwani kimebadili historia yote ya TANU na harakati za kudai uhuru.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesahihisha kwakukuletea kitabu hiki kinachotambua na kusisitiza kuwa mwasisi wa AA ni Cecil Matola badala ya historia yako isemayo ni Kleist Sykes.Yericko kazi yoyote ya mikono ya binadamu haikosi makosa na tutayarejea tena na tena na tena. Ukiliona kosa nifahamishe wala hapana sababu ya wewe kuandika kwa kisirani.
Sent using Jamii Forums mobile app