Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kwabahati mbaya mzee wangu haujakisoma kitabu chsngu, ingekuwa busara ukisome kisha uulize maswali... Kwa waliokisoma wameona vema mwishoni mwa kitabu nimeweka nyaraka na rejea zote, swali la chanzo lingejibiwa hivyo...

AA iliasisiwa 1927 na gavana wa kiingereza kama chama cha kushughulika na mambo ya starehe za watu weusi waliokuwa wamezuiwa kwenda kwenye maendeo ya starehe za wazungu huko mjini hasa katika ukumbi wa starehe wa Karijee leo NBC Garden ....

Matola amefariki 1933 wakati AA imeshazawadiwa jengo mtaa wa Stanley, leo Lumumba na leo ni makao ya TANU/ccm... Hoja ya kuwa ukoo wa Sykes ndio uliotoa jengo hilo ni uongo, labda tuseme waliteka umiliki baada ya Matola kufariki...kumbuka tangu afariki matola 1933 hadi achukue Nyerere madaraka 1953 chama hicho kilikuwa kama kikundi cha kahawa tu kisicho na dira... Baadae ndio chama kikaanza kuwa cha Siasa...
 
Yericko,
Hayo uliyoandika hapo juu tulishajadili huko nyuma na naamini mjadala
ule tuliumaliza lakini ukiwa unataka turejee upya katika huu mjadala si
vibaya ila mada iliyopo mezani kwa sasa ni mimi kukuomba, ''source,''
ya hayo unayosema umeandika kuhusu Cecil Matola.

Nakusihi toa jibu katika hili kisha tutasonga mbele Insha Allah kwa hayo
ambayo utapenda tujadili.

Huenda labda hujui unachotakiwa kufanya.

Mimi hapo chini nakuwekea moja ya ''source,'' ya historia niandikayo kuhusu
African Association:



Yericko,
Hiyo hapo juu ni tarifa za siri za Special Branch walizokuwa wakitoa mara kwa mara
kufanya tathmini ya harakati za siasa zilivyokuwa zikienda wakati wa ukoloni.

Nakusihi tuwekee mfano wa haya kuhusu Cecil Matola kuthibitisha unayosema.
Ikiwa huna hapana neno mimi nitaelewa.
 

Ndugu zanguni,
Mie sitii langu...

Cecil Matola
kapewa jina la kike - Sesilia...

Niliyoshuhudia hapa yamenitosha mzigo mzito.
Kusoma kitabu naweza kuvunjika mgongo.

Stanley Street ikawa Aggrey baada ya uhuru kisha Makisi Mbwana
katika kuwaenzi wapigania uhuru kiasi miaka 20 iliyopita.


Kushoto: Mwinjuma Mwinyikambi, Makisi Mbwana Julius Nyerere na Mshume Kiyate, 1962

Lumumba Avenue ilikuwa New Street wakati wa ukoloni na baada ya
uhuru 1961 ndiyo ikawa Lumumba.

Hii yote ni mitaa yangu niliyokulia naijua vyema.
Ukumbi wa Karimjee haukupata hata siku moja kuwa wa starehe.

Waafrika walikuwa wanakutana ukumbi wa Alexander na Tanga Club
kisha George Arnautoglo akawajengea Waafrika ukumbi maarufu kwa
jina la Arnautoglo Hall.
 
... is just an average diplomat, tofauti anavyotaka kukuzwa; Yericko is more security conscious kuliko yeye.
Mkuu Kilatha , nimekuona ukimponda mtu kule na kumsifu huyu jamaa. Kama mwandishi wa history anasoma jina la Cecil Matola, ni mwanaume, anamuandika Bibi Cecilia Matola, na hiyo ni hard copy!, what do you expect?.
P
 
... is just an average diplomat, tofauti anavyotaka kukuzwa; Yericko is more security conscious kuliko yeye.
Mkuu Kilatha , nimekuona ukimponda mtu kule na kumsifu huyu jamaa. Kama mwandishi wa history anasoma jina la Cecil Matola, ni mwanaume, anamuandika Bibi Cecilia Matola, na hiyo ni hard copy!, what do you expect?.
P
 
Wewe mzee unatapa tapa sana kulazimisha historia yako
 
Wewe mzee unatapa tapa sana kulazimisha historia yako
Yoga,
Nipo katika Cambridge Journal of African History.

Hawa sijawalazimisha kunitia katika jarida lao maarufu dunia nzima.

Halikadhalika niko katika Dictionary of African Biography.

Hawa ni Oxford University Press.

Haiwezekani ikawa mimi nimewalazimisha kutambua kazi zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…