Mnabuduhe
JF-Expert Member
- May 8, 2015
- 352
- 592
Yericko,
Swali lako umelikosea kuuliza.
Ilitakiwa uulize hivi, ''Kwa nini hakwenda Abdul au Ally?''
Wala ndugu yangu hapana haja ya wewe kuuliza swali kisha
ukaweka na masharti ya kujibiwa kuwa iwe, ''kinagaubaga.''
Nitaanza na Abbas.
Abbas alikuwa mtoto mdogo wakati ule, mtoto wa kutumwa
na kaka zake fanya hili, kalete kile kiasi hata Nyerere alipokuja
kukaa kwao baada ya kuacha kazi ya ualimu, Abbas alitolewa
chumbani kwake kumpisha Nyerere na Nyerere akimtuma
Abbas kama mdogo wake sana.
Hata siku ile ya mkutano wa kuasisi TANU 1954 Abbas alikuwa
nje pale New Street akitumwa kazi ndogo ndogo na ni yeye
aliyeagizwa kumleta mpiga picha Gomes aliyepiga ile picha
mashuhuri ya waasisi wa TANU.
Kwa nini Abdul hakwenda yeye UNO?
Abdul hakwenda yeye UNO kwa kuwa aliyetakiwa kwenda ni
rais wa TANU, Julius Nyerere.
Sasa hili si swali ambalo mtu ungeuliza na umewachagua ndugu
hawa kuuliza kwa nini hawakwenda wao wakamwachia Nyerere.
Labda ningekufahamisha kitu kuwa mwaka wa 1954 ilipokuja
Kamati ya Udhamini ya UNO aliyetoa maoni ya Waafrika kuhusu
kujitawala hakuwa Nyerere bali alikuwa Said Chamwenyewe.
1953 Abdul Sykes alipata, ''admission,'' ya Princeton University,
New Jersey.
Earle Seaton alimwandikia barua Abdul akimwambia kuwa
akifika New Jersey awe anakwenda New York, UNO kusikiliza
majadiliano ya nchi zilizo chini ya udhamini wa Waingereza.
Kutoka New York kwenda New Jersey ni masafa ya Magomeni
Mapipa na Kariakoo.
Yericko,
Nataka nikupe kitu.
Hii safari ya UNO ilikuwa katika TAA siku nyingi hata kabla
Nyerere hajafika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi.
Huyu Seaton mtu wa Bermuda alikuwa rafiki ya Abdul na
yeye ndiye aliyemuomba kwanza awasaidie TAA Political
Subcommittee katika kuliendea suala la Mandate Territories
UNO mwaka wa 1950 na 1952 ni yeye Abdul akiwa Kaimu Rais
wa TAA ndiye aliyemuomba Seaton atengeneze, ''petition,''
ya Meru Citizens Union katika Meru Land Case chini ya uongozi
wa Japhet Kirilo kwenda UNO.
Kirilo alipokwena kuzungumza UNO mkalimani wake alikuwa
Seaton.
Nakueleza haya yote ili nikujulishe historia ya safari ya Baba
wa Taifa UNO.
Nahitimisha kwa kukueleza kuwa mratibu wa safari hii na
mkusanyaji wa fedha za safari alikuwa Idd Faiz Mafungo
mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia
mweka hazina wa TANU.
Hii historia ndiyo iliyomvuruga akili Prof. Haroub Othman.
Hakuwa amepatapo kuyasikia majina haya wala kuijua historia
hii.
Aliona lazima azungumze na Baba wa Taifa apate kauli yake.
Ndiyo hivi sasa kinaandikwa kitabu kueleza maisha ya Mwalimu
Nyerere na bila shaka watapita nilipowatangulia.
Nadhani nimejibu, ''kinagaubaga,'' kama ulivyoniamrisha.
Sijataka kueleza kuwa Seaton ndiye alisaidia sana kutengeneza
mapandekezo ya katiba yaliyopelekwa kwa Gavana Twining
1950 na ''document,'' hii ikajadiliwa katika mkutano wa kuasisi
TANU 1954 na mapendekezo yake yamo katika hotuba ya
Mwalimu Nyerere UNO.
Mimi ningeambiwa niongeze majina katika yale 17 ya waaisi
wa TANU ambayo hayapo lakini yalistahili yawepo ningemweka:
Hamza Mwapachu, Ali Migeyo na Earle Seaton.
Chembelecho Maalim Faiza: ''Elimu Bila Khiyana.''
![]()
Earle Seaton na Mwalimu Nyerere baada ya uhuru
Earle Seaton alikuwa mkalimani wa Kililo toka lugha ipi kwenda lugha ipi?