Yericko,
Swali lako umelikosea kuuliza.
Ilitakiwa uulize hivi, ''Kwa nini hakwenda
Abdul au
Ally?''
Wala ndugu yangu hapana haja ya wewe kuuliza swali kisha ukaweka
na masharti ya kujibiwa kuwa iwe, ''kinagaubaga.''
Nitaanza na
Abbas.
Abbas alikuwa mtoto mdogo wakati ule, mtoto wa kutumwa na kaka
zake fanya hili, kalete kile kiasi hata
Nyerere alipokuja kukaa kwao,
Abbas alitolewa chumbani kwake kumpisha
Nyerere na
Nyerere
akimtuma
Abbas kama mdogo wake sana.
Hata siku ile ya mkutano wa kuasisi TANU 1954
Abbas alikuwa nje
pale New Street akitumwa kazi ndogo ndogo na ni yeye aliyeagizwa
kumleta mpiga picha
Gomes aliyepiga ile picha mashuhuri ya waasisi
wa TANU.
Kwa nini
Abdul hakwenda yeye UNO?
Abdul hakwenda yeye UNO kwa kuwa aliyetakiwa kwenda ni rais wa
TANU,
Julius Nyerere.
Sasa hili si swali ambalo mtu ungeuliza na umewachagua ndugu hawa
kuuliza kwa nini hawakwenda wao wakamwachia
Nyerere.
Labda ningekufahamisha kitu kuwa mwaka wa 1954 ilipokuja Kamati
ya Udhamini ya UNO aliyetoa maoni ya Waafrika kuhusu kujitawala
hakuwa
Nyerere bali alikuwa
Said Chamwenyewe.
1953
Abdul Sykes alipata, ''admission,'' ya Princeton University,New
Jersey.
Earle Seaton alimwandikia barua
Abdul akimwambia kuwa akifika
New Jersey awe anakwenda New York, UNO kusikiliza majadiliano ya
nchi zilizo chini ya udhamini wa Waingereza.
Kutoka New York kwenda New Jersey na masafa ya Magomeni Mapipa
na Kariakoo.
Yericko,
Nataka nikupe kitu.
Hii safari ya UNO ilikuwa katika TAA siku nyingi hata kabla
Nyerere
hajafika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi.
Huyu
Seaton alikuwa rafiki ya
Abdul na yeye ndiye aliyemuomba
kwanza awasaidie TAA Political Subcommittee katika kuliendea suala la
Mandate Territories UNO mwaka wa 1950 na 1952 ni yeye
Abdul ndiye
aliyemuomba
Seaton atengeneze, ''petition,'' ya Meru Citizens Union
katika Meru Land Case chini ya uongozi wa
Japhet Kirilo kwenda UNO.
Kirilo alipokwena kuzungumza UNO mkalimani wake alikuwa
Seaton.
Nakueleza haya yote ili nikujulishe historia ya safari ya
Baba wa Taifa
UNO.
Nahitimisha kwa kukueleza kuwa mratibu wa safari hii na mkusanyaji wa
fedha za safari alikuwa
Idd Faiz Mafungo mweka hazina wa Al Jamiatul
Islamiyya fi Tanganyika na pia mweka hazina wa TANU.
Hii historia ndiyo iliyomvuruga akili
Prof. Haroub Othman.
Hakuwa amepatapo kuyasikia majina haya wala kuijua historia hii.
Aliona lazima azungumze na
Baba wa Taifa apate kauli yake.
Ndiyo hivi sasa kinaandikwa kitabu kueleza maisha ya
Mwalimu Nyerere
na bila shaka watapita nilipowatangulia.
Nadhani nimejibu, ''kinagaubaga,'' kama ulivyoniamrisha.
Chembelecho
Maalim Faiza: ''Elimu Bila Khiyana.''
Earle Seaton na Mwalimu Nyerere baada ya uhuru