Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Ni kweli huwa siliwezi "somo" la wafia dini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ligema,
Dini iko wapi hapo?

Kusahihisha historia ndiyo imekuwa dini?

Au unataka kunambia kuwa Chuo Cha Kivukoni kwa kuwakwepa akina Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Amir kuwataja wachache walifanya hivyo kwa kutimiza malengo ya dini?

Ukweli umedhihiri leo wale wote walioachwa kuandikwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika nimewarejesha katika nafasi zao wanazostahili.

Ikiwa wewe hili limekughadhibisha na kukukera hii ni bahati mbaya.

Wala kwangu mie haikuwa nia yangu kuwaudhi ndugu zangu.

La unayo historia nyingine nje ya hii, uwanja uko wazi unakusubiri uandike.

Jopo la Prof. Shivji na wasomi wenzie wako kazini kuandika historia hii.

Tusubiri kitabu chao tukisome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mohamed Said, kumradhi, nitatoka kidogo nje ya mada. Katika mabandiko yako hapo nyuma ulizungumzia kuhusu chuo kikuu cha DSM na jumuia ya Waislam pale (MSAUDI).

Katika kipindi unachokizungumzia nilikuwa na swahiba wangu wa karibu sana ambae ametutangulia mbele ya haki (radhi-allah-anhu) kwa jina akiitwa inginia ULEDI KAYENVYA.

Ulimfahamu huyu ustadhi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ligema,
Dini iko wapi hapo?

Kusahihisha historia ndiyo imekuwa dini?

Au unataka kunambia kuwa Chuo Cha Kivukoni kwa kuwakwepa akina Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Amir kuwataja wachache walifanya hivyo kwa kutimiza malengo ya dini?

Ukweli umedhihiri leo wale wote walioachwa kuandikwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika nimewarejesha katika nafasi zao wanazostahili.

Ikiwa wewe hili limekughadhibisha na kukukera hii ni bahati mbaya.

Wala kwangu mie haikuwa nia yangu kuwaudhi ndugu zangu.

La unayo historia nyingine nje ya hii, uwanja uko wazi unakusubiri uandike.

Jopo la Prof. Shivji na wasomi wenzie wako kazini kuandika historia hii.

Tusubiri kitabu chao tukisome.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu weka vizuri hili, ulisahihisha historia ipi?

Maana katika maelezo yako maranyingi umekuwa ukisema wewe umeandika historia ya Tanganyika, ukibanwa unasema ni historia ya Wazee wako, napo tukikubana unahamisha magoli kwakusema ni historia ya uislamu, hapo ndipo hujificha mzee wewe...

Sasa waeleze makutano ulichoandikia kusahihisha ni nini?
 
Yericko,
Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ni historia ya wazee wangu.

Sijaelewa hiyo kunibana una maana gani.
Nimesahihisha historia ya Chuo Cha Kivukoni.

Kuhusu Waislam kitabu kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Sina tatizo ya wewe utapenda kuipa jina lipi historia hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
Kabla ya kandika haya yote ungepitia kwanza kitabu cha "Life and times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)"

Kina Matola, na wenzake ambao siyo Waislam wametajwa sana mpaka wale madaktari watano.

Hoja yako ya msingi sijui ni ipi.
 
mzee wako wa ngano mpaka sasa hajajibu hata hoja moja,na wewe unazurura tu!
njia ya muongo fupi!
 
Kabla ya kandika haya yote ungepitia kwanza kitabu cha "Life and times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)"

Kina Matola, na wenzake ambao siyo Waislam wametajwa sana mpaka wale madaktari watano.

Hoja yako ya msingi sijui ni ipi.
Ritz,
Ilianza na email kutoka kwa profesa mmoja akaniambia kuwa Sauti ya
Ujerumani (DW) imemwomba ashiriki katika kipindi cha kuadhimisha
Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 yeye akawataka radhi na walipomwomba
awatafutie mtu badala yake akataja jina langu.

Niliridhia na tukafanya kipindi, ''Meza ya Duara,'' washiriki wakiwa Ahmed
Rajab
akiwa (London), Dr. Harith Ghassany (Washington), Saleh Feruzi
(Zanzibar) na mimi nikiwa Tanga, mwenyekiti Othman Miraj akiwa Bonn.

Hii ilikuwa mwaka wa 2011.
Mjadala ulikuwa mkali sana.

Ahmed Rajab alichiana sana na Dr. Ghasany kwa yale aliyokuwa amesema
katika kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' kilichotoka 2010.

Katika mjadala ule nilishangazwa na Saleh Feruzi nadhani alikuwa Deputy
Secretary General CCM jinsi alivyokuwa anajifanya hajui, ''facts,'' katika
historia ya Tanzania na nilifika nikamwambia kuwa naelewa tatizo lake
anaujua ukweli lakini anaogopa kuusema.

Feruzi hivi sasa ni marehemu alipata tabu sana na mimi siku ile na hiki
ndicho kilichowavutia wasikilizaji wengi katika kipindi kile.

Kipindi kiliporushwa hewani, Othman Miraj ananiambia kuwa watu wengi
wakawa wanapiga simu DW kutaka kupata ''profile,'' ya Mohamed Said.

Hivi ndivyo niliavyoalikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin kufanya
mhadhara na kuandika chochote nipendacho kibaki katika maktaba yao.

Baada ya kumaliza mhadhara wangu wakati niko mgahawani wakati wa
chakula cha machana nimekaa peke yangu, akanifuata mtu akanambia
kuwa nimewanyongesha sana wenyeji wangu kwa kuwa nimewapa historia
ambayo hata siku moja hawakupatapo kuisikia lau kama wahadhiri kadhaa
kutoka Tanzania wamefika pale na kuzungumza.

Ikawa sasa zamu yangu mimi kunyongea.

Nilijisikia vibaya kuwa wenyeji wangu walionialika kwao na kunikirimu
nimewafadhaisha kwa yale aniliyosema.

Lakini baada ya mazungumzo na wengi katika wataalamu pale ZMO
niligundua kuwa kama ilivyo historia hii tunayoizungumza hapa kwa miaka
na wao walipata mshtuko kujua kuwa walichokuwa wanaamini siku zote
sicho.

Prof. Ali Mazrui aliniandikia email ya kunipongeza nilipompelekea kitabu
cha Abdul Sykes, Prof. Haroub Othman akanitafuta na kunihoji na
kutokana na yeye ndipo ilipoamuliwa historia hii ya TANU na uhuru wa
Tanganyika iandikwe kupitia maisha ya Baba wa Taifa, mradi ambao yeye
mwenyewe Mwalimu Nyerere aliridhia atashiriki lakini akafariki.

Hivi niandikapo kitabu kinaandikwa.

Kwa kuhitimisha hii ndiyo moja ya ibra ya kitabu cha Abdul Sykes, kila
akisomae kwa kutumia lugha ya kisasa, ''hakimuachi salama.''

ZMO wakati tunaagana waliniambia kuwa watafuatilia utafiti wangu kwa
wao kutuma wasomi wao kuja kufanya utafiti kwa yale niliyoandika katika
kitabu changu na wakaniomba niwape ushirikiano.

Hadi miaka mitatu hivi iliyopita watafiti wawili walishafika kutoka Ujerumani
kufanya utafiti na wamenihoji.

Hapa JF wapinzani wangu wao wanakuja na kejeli na wanaingia katika mjadala
wameghadhibika na wanaleta matusi na lugha zisizokuwa za kiungwana.
 
Yericko,
Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ni historia ya wazee wangu.

Sijaelewa hiyo kunibana una maana gani.
Nimesahihisha historia ya Chuo Cha Kivukoni.

Kuhusu Waislam kitabu kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Sina tatizo ya wewe utapenda kuipa jina lipi historia hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwaje utafifishe akina Matola ambao ndio waasisi wa AA? Ilikuwaje uwafifishe akina Kyaruzi ambao ndio waasisi wa TAA? iweje uwafifishe kina Nyerere ambao ndio waasisi wa TANU?

Hapo ndipo utata ulipo
 
Ritz,
Ilianza na email kutoka kwa profesa mmoja akaniambia kuwa Sauti ya
Ujerumani (DW) imemwomba ashiriki katika kipindi cha kuadhimisha
Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 yeye akawataka radhi na walipomwomba
awatafutie mtu badala yake akataja jina langu.

Niliridhia na tukafanya kipindi, ''Meza ya Duara,'' washiriki wakiwa Ahmed
Rajab
akiwa (London), Dr. Harith Ghassany (Washington), Saleh Feruzi
(Zanzibar) na mimi nikiwa Tanga, mwenyekiti Othman Miraj akiwa Bonn.

Hii ilikuwa mwaka wa 2011.
Mjadala ulikuwa mkali sana.

Ahmed Rajab alichiana sana na Dr. Ghasany kwa yale aliyokuwa amesema
katika kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' kilichotoka 2010.

Katika mjadala ule nilishangazwa na Saleh Feruzi nadhani alikuwa Deputy
Secretary General CCM jinsi alivyokuwa anajifanya hajui, ''facts,'' katika
historia ya Tanzania na nilifika nikamwambia kuwa naelewa tatizo lake
anaujua ukweli lakini anaogopa kuusema.

Feruzi hivi sasa ni marehemu alipata tabu sana na mimi siku ile na hiki
ndicho kilichowavutia wasikilizaji wengi katika kipindi kile.

Kipindi kiliporushwa hewani, Othman Miraj ananiambia kuwa watu wengi
wakawa wanapiga simu DW kutaka kupata ''profile,'' ya Mohamed Said.

Hivi ndivyo niliavyoalikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin kufanya
mhadhara na kuandika chochote nipendacho kibaki katika maktaba yao.

Baada ya kumaliza mhadhara wangu wakati niko mgahawani wakati wa
chakula cha machana nimekaa peke yangu, akanifuata mtu akanambia
kuwa nimewanyongesha sana wenyeji wangu kwa kuwa nimewapa historia
ambayo hata siku moja hawakupatapo kuisikia lau kama wahadhiri kadhaa
kutoka Tanzania wamefika pale na kuzungumza.

Ikawa sasa zamu yangu mimi kunyongea.

Nilijisikia vibaya kuwa wenyeji wangu walionialika kwao na kunikirimu
nimewafadhaisha kwa yale aniliyosema.

Lakini baada ya mazungumzo na wengi katika wataalamu pale ZMO
niligundua kuwa kama ilivyo historia hii tunayoizungumza hapa kwa miaka
na wao walipata mshtuko kujua kuwa walichokuwa wanaamini siku zote
sicho.

Prof. Ali Mazrui aliniandikia email ya kunipongeza nilipompelekea kitabu
cha Abdul Sykes, Prof. Haroub Othman akanitafuta na kunihoji na
kutokana na yeye ndipo ilipoamuliwa historia hii ya TANU na uhuru wa
Tanganyika iandikwe kupitia maisha ya Baba wa Taifa, mradi ambao yeye
mwenyewe Mwalimu Nyerere aliridhia atashiriki lakini akafariki.

Hivi niandikapo kitabu kinaandikwa.

Kwa kuhitimisha hii ndiyo moja ya ibra ya kitabu cha Abdul Sykes, kila
akisomae kwa kutumia lugha ya kisasa, ''hakimuachio salama.''

ZMO wakati tunaagana waliniambia kuwa watafuatilia utafiti wangu kwa
wao kutuma wasomi wao kuja kufanya utafiti kwa yale niliyoandika katika
kitabu changu na wakaniomba niwape ushirikinao.

Hadi miaka mitatu hivi iliyopita watafiti wawili walishafika kutoka Ujerumani
kufanya utafiti na wamenihoji.

Hapa JF wapinzani wangu wao wanakuja na kejeli na wanaingia katika mjadala
wameghadhibika na wanaleta matusi na lugha za zisizokuwa za kiungwana.
Unapenda sana ngano na unapenda sana kusikilizwa... Haya tunakusikiliza...
 
Yericko,
Ukiwa mwandishi unapenda kusomwa na mie hakika hufurahi kama hivi mnavyonisoma na kuuliza maswali.

Kwani wewe hupendi watu wakisome Majasusi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwaje utafifishe akina Matola ambao ndio waasisi wa AA? Ilikuwaje uwafifishe akina Kyaruzi ambao ndio waasisi wa TAA? iweje uwafifishe kina Nyerere ambao ndio waasisi wa TANU?

Hapo ndipo utata ulipo
Yericko,
Ikiwa wewe unaamini kuwa Matola ndiye nguzo ya AA mimi sina tatizo aliyesema kuwa yeye ndiye muasisi ni Kleist Sykes katika mswada wa maisha yake na nakala ya mswada huu upo Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na katika kitabu cha Iliffe, Modern Tanzanians.

Walichofanya Harvard na Oxford University Press ni kumweka katika Dictionary of African Biography.

Sijiu kwa nini Matola hakutiwa humo.

Pia ukiwa unaamini Nyerere ndiye aliyekuja na TANU Dar es Salaam na kuiasisi pia mimi sina tatizo na hilo.

Marehemu Mzee Lameck Bugohe ni kati ya waasisi 17 wa TANU yeye anasema alikuwa pia na fikra ya kuunda TANU.

Sisi nani tumpinge?

Kwahiyo kwakuwa Kleist kasema basi hukuwa na sababu za kuusaka ukweli zaidi?
 
Ukweli gani nitafute mie wakati Kleist alikuwa katika uongozi wa African Association umri wake wote na wanae wakaja kuwa pia viongozi katika TAA?

Nyaraka na picha za wakati wake zipo na nimeziweka hapa.

Juu ya haya John Iliffe katumia nyaraka hizi za Kleist katika utafiti wake wa historia ya Tanganyika.

Lakini kama nilivyokwisha kusema hakuna ulazima wa kukubaliana na Iliffe au hata Kleist mwenyewe.

Tumekuwa na historia iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni kwa miaka mingi sana na haikuwa tatizo.

Hii ni nchi huru na wananchi wake wana uhuru wa kuamini wanachokitaka.

Mzee Kyaruzi alikuwepo uliwahi kumhoji ikizingatiwa yeye ndie alikuwa rais mwasisi wa TAA?
 
Yericko,
Sikuwahi kumuhoji Dr. Kyaruzi.
Ama kuwa yeye ni muasisi wa TAA nilishakueleza kuwa TAA ni mwendelezo wa African Association jina tu lilibadilika mwaka wa 1948 na Kyaruzi aliingia katika uongozi kama rais mwaka wa 1950 Abdul Sykes akiwa katibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom