Kabla ya kandika haya yote ungepitia kwanza kitabu cha "Life and times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)"
Kina Matola, na wenzake ambao siyo Waislam wametajwa sana mpaka wale madaktari watano.
Hoja yako ya msingi sijui ni ipi.
Ritz,
Ilianza na email kutoka kwa profesa mmoja akaniambia kuwa Sauti ya
Ujerumani (DW) imemwomba ashiriki katika kipindi cha kuadhimisha
Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 yeye akawataka radhi na walipomwomba
awatafutie mtu badala yake akataja jina langu.
Niliridhia na tukafanya kipindi, ''Meza ya Duara,'' washiriki wakiwa
Ahmed
Rajab akiwa (London),
Dr. Harith Ghassany (Washington),
Saleh Feruzi
(Zanzibar) na mimi nikiwa Tanga, mwenyekiti
Othman Miraj akiwa Bonn.
Hii ilikuwa mwaka wa 2011.
Mjadala ulikuwa mkali sana.
Ahmed Rajab alichiana sana na
Dr. Ghasany kwa yale aliyokuwa amesema
katika kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' kilichotoka 2010.
Katika mjadala ule nilishangazwa na
Saleh Feruzi nadhani alikuwa Deputy
Secretary General CCM jinsi alivyokuwa anajifanya hajui, ''facts,'' katika
historia ya Tanzania na nilifika nikamwambia kuwa naelewa tatizo lake
anaujua ukweli lakini anaogopa kuusema.
Feruzi hivi sasa ni marehemu alipata tabu sana na mimi siku ile na hiki
ndicho kilichowavutia wasikilizaji wengi katika kipindi kile.
Kipindi kiliporushwa hewani,
Othman Miraj ananiambia kuwa watu wengi
wakawa wanapiga simu DW kutaka kupata ''profile,'' ya
Mohamed Said.
Hivi ndivyo niliavyoalikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin kufanya
mhadhara na kuandika chochote nipendacho kibaki katika maktaba yao.
Baada ya kumaliza mhadhara wangu wakati niko mgahawani wakati wa
chakula cha machana nimekaa peke yangu, akanifuata mtu akanambia
kuwa nimewanyongesha sana wenyeji wangu kwa kuwa nimewapa historia
ambayo hata siku moja hawakupatapo kuisikia lau kama wahadhiri kadhaa
kutoka Tanzania wamefika pale na kuzungumza.
Ikawa sasa zamu yangu mimi kunyongea.
Nilijisikia vibaya kuwa wenyeji wangu walionialika kwao na kunikirimu
nimewafadhaisha kwa yale aniliyosema.
Lakini baada ya mazungumzo na wengi katika wataalamu pale ZMO
niligundua kuwa kama ilivyo historia hii tunayoizungumza hapa kwa miaka
na wao walipata mshtuko kujua kuwa walichokuwa wanaamini siku zote
sicho.
Prof. Ali Mazrui aliniandikia email ya kunipongeza nilipompelekea kitabu
cha
Abdul Sykes, Prof. Haroub Othman akanitafuta na kunihoji na
kutokana na yeye ndipo ilipoamuliwa historia hii ya TANU na uhuru wa
Tanganyika iandikwe kupitia maisha ya Baba wa Taifa, mradi ambao yeye
mwenyewe
Mwalimu Nyerere aliridhia atashiriki lakini akafariki.
Hivi niandikapo kitabu kinaandikwa.
Kwa kuhitimisha hii ndiyo moja ya ibra ya kitabu cha
Abdul Sykes, kila
akisomae kwa kutumia lugha ya kisasa, ''hakimuachi salama.''
ZMO wakati tunaagana waliniambia kuwa watafuatilia utafiti wangu kwa
wao kutuma wasomi wao kuja kufanya utafiti kwa yale niliyoandika katika
kitabu changu na wakaniomba niwape ushirikiano.
Hadi miaka mitatu hivi iliyopita watafiti wawili walishafika kutoka Ujerumani
kufanya utafiti na wamenihoji.
Hapa JF wapinzani wangu wao wanakuja na kejeli na wanaingia katika mjadala
wameghadhibika na wanaleta matusi na lugha zisizokuwa za kiungwana.