Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Ukiweka vielelezo na vyanzo hayo yote yanakufa, unabaki usomi usio na mawaa, Tatizo mzee wako anatumia utafiti wa mnyororo mmoja tu,

Deisy Sykes mtoto wa Abdul Sykes mjukuu wa Kleist Sykes ndie aliyempa nyaraka Mwalimu wake wa chuo aitwaye John Ilife, na kitabu cha Mohamed chanzo cha historia nzima ni Daesy na John I,

Sasa tumia akili kujua kuwa kumbe historia ya Mohamed chanzo ni Sykes to Sykes, je unataraji jini hapo?

Yericko,
Hakuna neno kwa wewe kuzikataa Nyaraka za Sykes katika historia ya
African Association na TANU.

Hili nawaachia wasomaji waamue.

Lakini fahamu kuwa wako maelfu wamezikubali na katika hao ni John
Iliffe
na mabingwa wengine katika Historia ya Afrika.

Lakini hili lisituzuie kueleza historia ya TANU na watu walioshirika katika
kuiunda.

Katika historia ya TANU Chief Kidaha Makwaia hajatajwa popote lakini
mimi najua habari zake na napenda nikueleze kuwa ni vitu kama hivi
ndivyo vilivyoninyanyua mimi katika utafiti wa historia hii.

Soma hapo chini historia ya Chief Kidaha katika siasa za kuunda TANU:

toW0HLKw0_eZRKHUURD38LIxZWcW5RXD7goNoYJWFVWEj8kMEyL1bPXqHWB5CmfrXmD1mA=w329-h566-no

Kushoto: Mama Daisy, mbele ni Bi. Titi Mohamed
na kushoto yake ni Bi. Zainab mkewe Tewa Said Tewa
katika maandamano siku za mwanzo za uhuru

Mama Daisy iina lake ni Mwamvua biti Masha.
Mimi ni mama yangu kwa kuwa alikuwa shoga ya marehemu mama yangu.

Lakini kwa watu wa Dar es Salaam akivuma kwa jina la binti yake Daisy
kwa hiyo akijulikana kama Mama Daisy.

Ingekuwa si huu uhusiano wa kindugu Mama Daisy asingenieleza chochote
katika historia ya mumewe marehemu Abdulwahid Sykes na Chief Kidaha
kwa kuwa wakati ule watu walikuwa wengi wakiogopa sana kusema lolote lililo
kinyume na historia ambayo watu walikuwa wameaminishwa.

Jina la Abdul na Ally na wazalendo wengine kama Sheikh Hassan bin Amir,
Sheikh Suleiman Takadir, Bi, Tatu bint Mzee, Iddi Faizi Mafongo, Oscar
Kambona
kuwataja wachache yote yalikuwa yamefutwa kabisa katika historia
ya uhuru.

Siku ile Mwalimu Nyerere ambayo aliwahutubia Wazee wa Mzizima yaani Dar
es Salaam kuwaaga ambayo kwa bahati mbaya sana ndiyo siku aliyosema kuwa
hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika yeye alipoingia TAA.

Siku ile Mama Maria Nyerere alikuwa na kikao kifupi na akina Mama wa Dar
es Salaam hapo hapo Diamond Jubilee Hall.

Mmojawapo katika hao akina mama alikuwa Mama Daisy.

Mama Maria aliwaeleza akina mama wale kuwa yeye na mumewe walipokelewa
Dar es Salaam na Mama Daisy na mumewe Abdul Sykes.

Mama Daisy
hakuwa na wasiwasi na mimi akinieleza kila kitu na kubwa ambalo
lilinishtua sana ni siku aliponiambia kuwa Allah ndiye atoae ufalme, ''Baba yako
yeye akimtaka sana Chief David Kidaha Makwaia ndiyo aingie TAA wamchague
president kisha waunde TANU lakini Chief Kidaha hakutaka.''

IMG-20160406-WA0111%2B%25281%2529.jpg

Chief David Kidaha Makwaia wa Siha

''Kila Chief Kidaha akija Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Legico tukimualika
nyumbani kwa chakula cha jioni na mimi nilikuwa pale nikiwaandalia na nikisikiliza
mazungumzo yao yote Bwana Abdul akimwambia Chief Kidaha, ''David hebu
achana na hao Waingereza bwana njoo huku tudai nchi yetu.''

Mama Daisy alikuwa na mengi na akizungumza alikuwa hana uchungu kwa yale
yaliyopita akizungumza huku ametulia kabisa.

Hali ya siasa katika TAA ilikuwa hivi katika miaka ya mwanzoni ya 1950 kabla TANU
haijaasisiwa 1954.

Sasa sisi tusifungwe na hili jambo la nani achukue sifa ya kuasisi TANU.
Muhimu ni kuangalia nini kiliptika kabla ya TANU kuja kuasisiwa 1954.

Anaetaka taarifa zaidi za Chief Kidaha Makwaia aingie hapo chini:
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007
 
TAA aliikuta ikiwa na adiology gani?
Yericko,
Umeuliza TAA ilikuwa na ideology gani?

Nakuomba usome hii taarifa ya TAA iliyoandikwa na Abdul Sykes ambayo
nimeiweka katika kitabu chake ukimaliza naamini swali lako litakuwa labda
limepata jibu:

''Tarehe 7 Januari, 1951 mkutano muhimu sana ulifanyika katika Ukumbi wa Arnatouglo Dar es Salaam. Baada ya mwaka mmoja ofisini kama katibu, Abdulwahid aliwasilisha taarifa yake kwa mkutano mkuu. Hii ilikuwa tofauti ukilinganisha na uongozi uliopita wa wazee.

Akiangalia nyuma mwaka wa 1950, Abdulwahid aliwataarifu wanachama kuwa mwaka huo ulikuwa mgumu kwa TAA vile vile. Wanachama walijulishwa kuhusu mwanasheria kutoka Bermuda, Earle Seaton kama mshauri wa TAA wa sheria na mchango wake katika kutayarisha mapendekezo iliyowasilishwa kwa Gavana Twining.

Wanachama walijulishwa kuhusu kufufuliwa kwa matawi ya TAA, mawasiliano yake na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na uhusiano ulioanzishwa na TAA na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria. Abdulwahid aliwaeleza wanachama juu ya ziara yake ya Nairobi aliyofanya mwezi Oktoba, 1950, na kukutana kwake na Balozi wa India katika Afrika ya Mashariki.

Vilevile aliwaeleza kuhusu mshikamano ulioanzishwa kati ya TAA na KAU; na kutolewa nafasi za kusoma katika vyuo vikuu vya India na serikali ya nchi hiyo kwa Waafrika wa Tanganyika kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya India. Abdulwahid alieleza kwa ufupi juu ya kuundwa kwa African Parents Association kwa msaada wa Dr Raymond na European Parents Association.

Mwaka wa 1950 utaingia katika historia ya Tanganyika kama wakati wasomi wa Makerere, waliingia TAA kwa wingi sana. Wote walikuwa vijana na walitaka kufanya mambo mengi kwa haraka na kutimiza kila kitu mara moja. Migongano katika mawazo na mbinu za siasa hayakuwa mambo mageni. Lakini migongano hii ndiyo hasa ilikuwa kichocheo cha kuendesha utawala mzuri katika chama.

Taarifa ya Abdulwahid ilieleza mafanikio na matatizo ya TAA. Ofisi ya TAA haikuwa na umeme na aliwaeleza wanachama mipango ya kuingiza umeme, kufungua maktaba ndogo na kuanzisha masomo ya usiku kwa watu wazima. Hatimaye alizungumza juu ya ukomunisti na uhusiano kati ya watu wa rangi mbalimbali. Alitahadharisha dhidi ya taathira za ukomunisti katika siasa za Tanganyika na alihimiza ushirikiano baina ya wanachama wa TAA na watu wa mataifa mengine.

Wakati huo baadhi ya viongozi wa TAA walikuwa wakifahamika kwa misimamo mikali. Miongoni mwao alikuwa Stephen Mhando na Hamza Mwapachu. Wakati huo Mwapachu alikuwa akiandika katika The Sentinel, jarida la Fabian Society lililokuwa likichapishwa London.''
(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951, (Nyaraka za Sykes).
 
Historia gani huandikwa ya upande mmoja? Wapi Julius Nyerere aliwahi kutoa maoni au kuhojiwa na Mohamed Said ikizingatiwa kitabu chake kimetoka Mwalimu akiwa hai? Hakukuwa na umuhimu wa Rais wa TANU kuhojiwa juu ya historia ila ikawa mhimu mjukuu wa Kleist Sykes Mbuwane kuhojiwa na kutumia nyaraka zinazoitwa za baba yake?
Yericko,
Kwa kweli mimi nilikuwa na taarifa zote za Mwalimu Nyerere kuhusu
TANU kwanza kutoka katika vitabu na ''lecture,'' za walimu wangu Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam sikuhitaji chochote ambacho sikuwa sikijui
kutoka kwake.

Maisha ya Mwalimu Nyerere katika TANU yalikuwa yameandikwa na
Chuo Cha Kivukoni na yakijulikana.

Sijui wewe ungependa niende kwake nimuulize kitu gani?
Ningependa kusikia mawazo yako.
 
Umepiga kwenye mfupa hapa ataugulia sana
Yericko,
Kitu gani kikufanya wewe uwe na uhakika kiasi hiki?
Hebu soma jibu langu hapo chini:

Wana Majlis,
Nadhani katika jina langu linawapelekea wengi kunifikiria kinyume nilivyo
kuwa hiki siwezi kuwa nafahamu.

Nacheka sana.

Nilikaa jirani na Johns Hopkins University Washington wala sikuwa na
uhusiano na chuo ila kwenda hapo kuswali sala ya Ijumaa.

Tukisali katika darasa maana hakuna msikiti hapo.
Mwenyeji wangu yeye bingwa mtafiti ndiye kanipeleka hapo.

Huyu ndiye aliyeniingiza katika dunia ambayo sikupatapo kudhania kuwa
ipo.

Tukiwa nyumbani nasomeshwa.
Ndani ya gari nasomeshwa.

Mezani tukila nasomeshwa...

Nadhani namshangaza sana huyu jamaa.
Allah anapotoa haesabu anakumwagia.

Johns Hopkins hapafungwi 24/7 mwaka mzima na taa hazizimwi.
Lipo jingine nitamweleza siku nyingine In Shaa Allah.

Huyu sahib yangu humpelekea haya nipatayo hapa anieleze kwa
nini inakuwa hivi kuwa watu wamekuwa wakiamini uongo lakini
siku walipopewa kweli si tu wameikataa lakini pia wameghadhibika.

Aliniletea jibu lenye maneno mawili.

Kasema hao wamepata mshtuko na huo mshtuko umewasababishia
maradhi yaani wana ugonjwa.

Nikamuuliza nini dawa yake?
Akasema wanahitaji, "therapy."

Maradhi yenyewe ni haya:
bila elimu ya kanisa katoliki saa hizi ungekuwa mpunga madogoli km sharif majini!
unakuja unavimbisha kishwa km ngamia,wewe mkigoma huna shukrani!

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola.
 
Kuna siku miaka kadhaa iliyopita uliahidi utakuja na kanda ya "baba" ko wakati anaaga Diamond Jubilee, unakumbuka? Iko wapi na miaka mingapi sasa?

Kuna siku ukapinga kuwa Chief Mkwawa hakuitwa Abdallah, ukasema utakuja na facts kutoka Iringa, umekuja nazo?

Kuna siku ulidai Julius Nyerere ni babako mzazi, unakumbuka? Andrew Nyerere akaja kukuumbuwa.

Kuna siku kuna kijana alifunguwa uzi humu humu JF kuwa umemtapeli pesa zake. Unakumbuka?

Bado huna haya?
Teh teh teh!

Nilicheka sana siku hiyo alivyokuwa muongo akajifanya yeye ni mtoto wa Mama Maria, akienda Musoma ataleta picha za Mzee wake Nyerere tuone alivyokuwa ananunuliwa suti na Maliale.
 
Yericko,
Kwa kweli mimi nilikuwa na taarifa zote za Mwalimu Nyerere kuhusu
TANU kwanza kutoka katika vitabu na ''lecture,'' za walimu wangu Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam sikuhitaji chochote ambacho sikuwa sikijui
kutoka kwake.

Maisha ya Mwalimu Nyerere katika TANU yalikuwa yameandikwa na
Chuo Cha Kivukoni na yakijulikana.

Sijui wewe ungependa niende kwake nimuulize kitu gani?
Ningependa kusikia mawazo yako.
Zingatia kuwa historia yako unasisitiza kuwa ni yale yaliyofichwa na wanatanu wa Chuo cha Kivukoni,

Hivyo uliyoyaona na kuyafahamu ya Mwalimu sio uliyoyaandika, kwa namna gani unapata uthubutu wa kusema hukuona la maana toka kwa Mwalimu Nyerere na ukaona la maana toka kwa mjukuu wa Kleist?
 
Yericko ni hivi wala usijisikie vibaya wala kukupitikia kuwa nafanya dharau. Mimi mkononi nilikuwa na mswada wa Kleist Sykes ulioeleza maisha yake katika African Association kuanzia 1929 hadi alipofariki 1947. Isitoshe nina Nyaraka za Sykes kipindi cha wanae wako TAA baada WWII 1945 hadi walipounda TANU 1954. Nilikuwa na taarifa za kutosha kuhusu TANU kuliko walizokuwanazo Chuo Cha Kivukoni. Labda unifahamishe kipi nilichokosa kwa kutomhoji Mwalimu Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANU ilikuwaje iundwe na katibu bila rais ambaye wewe unampuuza?

Leo historia ya ccm katika 2010-2015 unaweza kuiandika kwakumtumia Kinana tu bila kumsikiliza Kikwete?

Kosa kubwa umemfifisha na kumdogosha mwasisi wa TANU bwana Julius Nyerere
 
Yericko TANU historia yake inakwenda nyuma kuanzia 1929 ilipoundwa African Association. Nimeeleza hapa jinsi Abdul na Chief Kidaha walivyokuwa wanajadili uongozi katika TANU hii ilikuwa 1950 halikadhalika nimeweka audio naeleza Abdul na Mwapachu walivyomjadili Nyerere Nansio kabla ya uchaguzi wa TAA wa 1953 uliomtia madarakani Nyerere. Baada ya uchaguzi ule wa 17 April 1953 ambao Nyerere alichaguliwa kuwa rais miezi 14 tu TANU ikaundwa. Katika mkutano wa kwanza wa TANU Arnautouglo Hall wengi wa waliohudhuria walikuwa hawamjui vizuri Nyerere. Mkutano huu ulihudhuriwa na watu kama ishirini na zaidi kidogo na aliyeuandika katika gazeti alikuwa Mashado Ramadhani Plantan ndani ya gazeti lake Zuhra.

Hili la Nyerere kuasisi TANU linakushughulisha sana lakini kwangu mie si jambo kubwa la kutufanya tusisonge mbele. Mimi kila nikipata fursa nitakueleza mambo yalivyokuwa kwani hiyo TANU iliishi ndani ya fikra za wazee wangu kwa miaka mingi. Hawakuzuka tu wakaunda TANU. Nimeieleza historia yao mara nyingi sana hapa Majlis.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANU ilikuwaje iundwe na katibu bila rais ambaye wewe unampuuza?

Leo historia ya ccm katika 2010-2015 unaweza kuiandika kwakumtumia Kinana tu bila kumsikiliza Kikwete?
Kosa kubwa umemfifisha na kumdogosha mwasisi wa TANU bwana Julius Nyerere
Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Yericko hili neno, "kudogosha," nimelipenda. Una fikra gani na wale, "waliofuta?"

Nyerere hakuwa Mtanganyika wa kwanza kwenda UN.

Kumbuka hilo.
 
Povu linakutoka nikafikiri umekuja na kitu kipya. Kumbe unatamani historia alivyoandika Mohamed Said iwe vingine.

Si uandike historia yako, uwaingize wote bila kuchukua chochote kutoka kwa Mohamed Said.

Thubutu.
 
Yericko hili neno, "kudogosha," nimelipenda. Una fikra gani na wale, "waliofuta?"

Sent using Jamii Forums mobile app
Yericko,
Abdul Sykes, ''alishirikishwa,'' katika kuunda TANU 1954.

Hii ndiyo raha niipatayo kila siku hata baada ya miaka 20 ya kutoka
kitabu cha Abdul Sykes.

Abdul anawakaribisha watu nyumbani kwake katika mikutano ya siri
ya kuunda TANU aliyekaribishwa ndiyo anakuwa kaasisi TANU na
mwenye nyumba anakuwa, ''kashirikishwa,'' na aliyemualika.

Inaleta raha sana moyoni kwangu.
Abdul alifikaje kuongoza TAA?

Jibu la haraka unaweza kusema kuwa hiyo African Association kaasisi
baba yake.

Ndipo Ahmed Rashhad Ali akamwambia Prof. Haroub Othman cha
ajabu kipi kwa Abdul kuasisi TANU?

Mbona hushangazwi kwa baba yake kuasisi African Association na Al
Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

Hakutosheka na jibu lile ikabidi aende kwa muhusika mwenyewe apate
kauli yake.

Matokeo yake ndiyo Prof. Shivji na jopo lake wanaandika sasa historia
ya Baba wa Taifa ili historia ikae vizuri.

Ibra kubwa ni kuwa jopo likaja kuzungumza na mwandishi awape habari
za Abdul Sykes na yeye akawapa nyaraka na picha za nyakati zile.

Jambo moja limezua jingine.

Wakati nafanya utafiti wa historia hii kila nilipomaliza mahojiano wale
wazee walikuwa wakinisomea dua kuiombea Mungu hii kazi ifanikiwe na
kweli dua zao zimekuwa makbul, yaani zimetakabaliwa, Allah kazikubali.

Huyu Abdul Sykes aliyefutwa katika historia ya TANU leo kila uchao yuko
midomoni watu wanamsoma na medali ya ''Mwenge wa Uhuru,'' kapewa.

Lakini Abdul aliingia vipi kuongoza TAA?

Ukitaka kujua inabidi urudi nyuma hadi mwaka wa 1947 Abdul akiwa na
miaka 23 alipoongoza mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam.

Hiki ni kisa kitamu sana.

John Iliffe aliandika paper, '‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’'
katika Tanzania Notes and Records," 71 (1970) nzima lakini mengi yalimpita
sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Mimi nikafanya utafiti kuhusu chama cha makuli na mgomo ule na nikaandika,
''Dar es Salaam Dockworkers Movement 1947-1950,'' sikumuhurumia Abdul
Sykes
bali huruma yangu ilikwenda kwa Iliffe.

Mkasa huu ndiyo uliomfikisha Abdul Sykes katika uongozi wa TAA 1950 na
akapata kuungwa mkono katika kuunda TANU 1954.

Vipi jambo muhimu la kihistoria kama hili lilimpita akashindwa kuona umuhimu
wake katika mustakbali na mwelekeo wa siasa?

Wana Majilis,
Someni kile kilichopitika Dar es Salaam kati ya mwaka wa 1947 hadi 1950 ambao
ndiyo ukajakuwa msingi ambao TANU ilikuja kujengwa juu yake:
  1. Mohamed Said: The Book: Excerpts...Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part One
  2. Mohamed Said: Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part Two
  3. Mohamed Said: Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part Three
 
Nyerere hakuwa Mtanganyika wa kwanza kwenda UN.

Kumbuka hilo.
Maalim Faiza,
Mhariri wa kitabu cha Abdul Sykes naambiwa alimweleza ''publisher,''
kuwa wote walioandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika si
kama hawakutaka kuandika vyema historia ile tatizo ni kuwa walikuwa
hawaijui historia yenyewe.

Wengi hapa wamegubikwa na kutoijua historia ya TANU na walipokuja
kuelezwa wamepata mshtuko uliowasababishia maradhi kama mtafiti
yule rafiki yangu niliyekuwanae Washington DC alivyosema.

Ngoja kwa mukhtasari nieleze vipi Abdul Sykes alivyolishughulikia tatizo
la Meru Land Case lililomfikisha Japhet Kirilo kuzungumza UNO 1952:

''Abdulwahid aliwasiliana na Earle Seaton mjini Moshi kutaka ushauri wa kisheria juu ya tatizo la Meru. Seaton alikuja Dar es Salaam na kukutana na Abdulwahid na uongozi wa TAA. Ilikubaliwa na pande zote mbili kuwa makao makuu ya TAA, Meru Citizenís Union ikiongozwa na Japhet Kirilo na Seaton lazima waunganishe shughuli zao katika kesi hiyo na kwa pamoja watume rufaa yao kwenye Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York.

Kwa sasa uongozi wa chama cha TAA ulitambua kwamba nusura yao ilitegemea uwezo wao wa kudhibiti na kushawishi matukio na maamuzi ndani ya Baraza la Kutunga Sheria. Ili kuweza kufanya hayo shinikizo lilitakiwa kuwekwa katika Baraza la Udhamini huko New York, nchini Amerika na siyo katika Ofisi ya Makoloni pale London Uiengereza.

Mgogoro wa ardhi ya Meru ni wa pekee katika historia ya Tanganyika. Ilikuwa kupitia katika mgogoro huo ndiyo Mtanganyika, Japhet Kirilo, akifuatana na Earle Seaton kama mkalimani na mshauri wa sheria, kwa mara ya kwanza alizungumza mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York, na kuonyesha udhalimu wa ukoloni. Mnamo November, 1952 Kirilo alizungumza mbele ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu.

Watu wa Tanganyika sasa walikuwa wanayachukua mapambano yao toka mipaka yao hadi kwenye kumbi za Umoja wa Mataifa, mjini New York kutafuta haki. Lakini Kirilo alirudi mikono mitupu. Rufaa ya mgogoro wa ardhi ya Wameru ilitupiliwa mbali.

Mgogoro wa ardhi ya Meru ni wa pekee katika historia ya Tanganyika. Ilikuwa kupitia katika mgogoro huo ndiyo Mtanganyika, Japhet Kirilo, akifuatana na Earle Seaton kama mkalimani na mshauri wa sheria, kwa mara ya kwanza alizungumza mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York, na kuonyesha udhalimu wa ukoloni.

Mnamo November, 1952 Kirilo alizungumza mbele ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu. Watu wa Tanganyika sasa walikuwa wanayachukua mapambano yao toka mipaka yao hadi kwenye kumbi za Umoja wa Mataifa, mjini New York kutafuta haki. Lakini Kirilo alirudi mikono mitupu. Rufaa ya mgogoro wa ardhi ya Wameru ilitupiliwa mbali.''

Wana Majlis,
Hayo hapo juu nakukumbusheni ilikuwa mwaka wa 1952.

Picha hiyo hapo chini nilipiga mwaka wa 1989 Usa River nje ya nyumba
ya Japhet Kirilo.

Aliyenipeleka hapa huyo aliye kwenye picha ni Abdulwahid Ally Sykes.

OxBBmPny9cYohxOR-_3u3lPv0kD3TdLicRKUalMnO-PreMHJrAsuNqq1P72v0xTvPErwpk60hPGifcIEtgxqg17cQJdEoz8aJ-H2Y6WMbaM4ZyEqb8jXR8PMI_uEs_Q2ZINnHBUdo67bZzmcCFBlLxQ-dgwLEQqb8V3afXXcWpdRNm46SDOVNSCagHM3qw14mTmTPVVhrb46Qf7DYSTXpF3U_pVLjIno4MYb4P_OWe6qIXALV12gwpu83uCr_QQXazTs6TssB0qIgkATHc5t2cQfKX6H6d3T-HgmQfWZucKiroriasEOWWOEm1TiGb2GSGVWHNoFbR2YJfuVjuNRzPqQNNPL9RaLp1Kg-FzfAkU3U_0l3sjVffLI0m9qjhj9mC-00r1JwB1ISYNe8ogtylK17wwAy9T6TCHmnBUue_l33L1b9P6SiwadSPigzfqgVz6jRc7e2pFKzCF45AMwOntb1bdn2aeVEFrqoZ5hpF7KDX4fhchFXWoC8HNlvQHxeSlQ43yyRXN5qU7tMsHfvV3tQbn_rZnkWzhqCcm9NrBKVd-eKvJJo1qfG-WBNAV39hG1jFA5mhmpYYgc7PHrg2_qq1ijN0fIRGKoQGKTz8bN83PqXUbA3Q=w839-h629-no
 
Back
Top Bottom