Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
mv-bukoba.jpg

Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbwi pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uokoaji

RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.

Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.

Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.

Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.

MV+Bukoba+ikizama-250x148.jpg

Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama

Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi.Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.

Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.

Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani; na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.

Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa ‘kaburi' lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.

11.JPG

Makaburi ya Igoma ambako wahanga wa Mv Bukoba walikozikwa

Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano.
 
Bado nawakumbuka Theopista, Marando na Luciano, dah ilikuwa mbaya. Wapumzike kwa amani.
 
Wapumzike kwa amani marehemu wote, kwakweli ni tukio la kusikitisha hasa kwa watu waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo.
 
Namkumbuka Ali mwarabu tulikuwa tunasoma nae Nyanza primary, na imam wa masjid al asais makongoro nae kaburi lake lilikuwa ziwani, Mungu awarehemu!
 
Ilinisikitisha sana, I remember baba alinunua mkanda wa video (VHS) ya jinsi walivokuwa wanatafuta miili ya marehem. Nakumbuka serikali ya sauzi ilitusaidia wanamaji kusaidia uokoaji daah! I just can't remember to forget this terrible accident.
 
Binafsi nilikuwa Mwanza mwaka huo na niliongea na aliyekuwa Mhandisi wa MV Bukoba, ndugu Adolph.

1. Meli ilijazia mizigo Kemondo na aliyesababisha alikuwa Meneja wa Kemondo, Prosper Rugumila ambaye alikamatwa na kushitakiwa

2. Kapteni Jumanne Rume Mwiru alikuwa akisaidia uokoaji na wakati meli inazama walikuwa wakisogeza kivuko cha Kamanga kwa ajili ya kuivuta meli isogee nchi kavu na hapo uokoaji ungekuwa rahisi zaidi.

3. Meli ilizama ghafla kabla ya kivuko cha Kamanga kufika eneo la tukio baada ya wahuni kukitoboa meli kwa kutumia gesi wakiamini wataokoa jamaa zao waliokoa wanawasiliana kwa kutumia ‘simu maalumu’. Tukio hilo lilitokea bila ushirikishwaji wataalamu wakiwemo Kapteni na wahusika wa Kemondo walikuwa wakielekea kuivuta meli ya MV Bukoba.

Sasa, kwa mazingira hayo ulitarajia Nahodha na wataalamu wakimbilie kujizamisha wafe au wafanye jitihada nyingine kuokoa watu?

Kwanza ujue muda ule Kapteni alikuwa akitumika kupata taarifa muhimu za ramani ya meli kuokoa watu na alikuwa chini ya ulinzi. Baada ya maafa alifikishwa mahakamani na uamuzi ulitolewa (Mengine yako katika taarifa rasmi za mahakama).
 
RIP students from Rugambwa. We lost a family friend, she was a student at rugambwa boarded that ship.
 
Namkumbuka sana mzee Mlebya aliyekuwa Mhasibu wa TAC naye alifariki tuliwahi kaa wote Masaki pale Chole Rd. Mwenyezi MUNGU awarehemu wote.
 
Nakumbuka mambo mengi sana wakati huo.

Siku hii naikumbuka sana maana taarifa nilizipata nikiwa kwenye daladala natoka shule, siwezi kusahau watu walivyokuwa wanahadithiana kwa uchungu sana siku hiyo. Nilikosa raha siku nzima japo sikupoteza ndugu au rafiki wa karibu bali nilipoteza Watanzania wenzangu.

Nakumbuka picha na matukio mbalimbali ya wakati huo ikiwemo imani za kishirikina na upumbavu wabaadhi ya watu waliochangia kuipoteza meli na idadi kubwa ya watu waliokuwa wamekwama ndani.
 
Nakumbuka I was in primary school, tukapata taarifa tukiwa darasani, ilibadili maisha ya Watu wengi sana, kuna marafiki zangu walibaki yatima, kuna wazazi walipoteza watoto wao.

Very sad memory kwa kweli.
 
Dah, umenikumbusha mbali sana, nikiwa form two. Ila ile ajali kwa mara ya kwanza ilimleta Mkapa na Mrema kwa ukaribu, maana pale ndo waliposhikamana baada ya rafu za uchaguzi wa mwaka 1995
 
Kuna jamaa alikua fundi seremala kipindi hicho na nilimpatia oda ya kitanda. Alipotea ghafla na siku nilipokutana nae huyo bwana alikua tajiri wa kutisha.nilimkumbusha oda yangu na advance niliyompa akaenda kuninunulia kitanda kipya on the spot.
 
Je, tumeweza kujifunza lolote kutokana na ajali ile?hakika ni blah blah tu, walale kwa amani wahanga wote wa ajali ile, lakini vile vile napenda kuwapa pole nyingi na faraja wale wote ambao waliondokewa na wapendwa wao, na kuondoka kwao likawa pigo kubwa, Mungu wa rehema nyingi azidi kuwatia nguvu na ujasiri wa kusonga mbele, aamen.
 
Ilinisikitisha sana, I remember baba alinunua mkanda wa video (VHS) ya jinsi walivokuwa wanatafuta miili ya marehem, nakumbuka serikali ya sauzi ilitusaidia wanamaji kusaidia uokoaji daah! I just can't remember to forget this terrible accident.
Hivi leo hii likitokeaj janga kama hili tuna vifaa na wazamiaji wetu wenyewe?
 
Back
Top Bottom