Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

ilinivuruga sana kisaikolojia asee,nilipata tabu and i was still young,i mean bado akili haikuwa imepata mishtuko ya aina hyo ya vifo vya kutisha.nilikuwa bado sijajua mambo haya ya mitandao so taarifa hazkuwa znatufikia kiulaini kama kipind hichi,, rip wote,jaman nimepata huzuni,nimekumbuka hilo tukio
 
aliyekuwa mwalimu wangu wa Physics pale Makongo alipoteza familia nzima ktk ajali hii
 
Flaviana Matata ameanzisha foundation ya kusaidia vifaa vya uokoaji melini. Huwa anajitahidi kutoa maboya na mambo kama hayo, lakini ni ka foundation kachanga na uwezo wake bado. Na yeye alipoteza mama mzazi kwenye ajali hiyo kwa hiyo anafanya in good faith.

hivi leo hii likitokeaj janga kama hili tuna vifaa na wazamiaji wetu wenyewe?
 
Wavulana wa Ihungo je? Tena wengine ndio walikuwa wamemaliza form six. Kuna mzee mmoja alipoteza mwanaye pekee aliyetoka kijijini na kufanikiwa kufika high skul, alikuwa anatembea kwa miguu kutoka Igoma to mjini. Sikuwahi elewa kwa nini hakutaka kupanda gari kwa muda kama wa siku 3.

Pole sana Leornado, wasichana wa Rugambwa walituhuzunisha sana pia.
 
Naikumbuka familia iliyopoteza watu (nadhani) 22! Katika familia hii kuna mmoja alikufa na wakeze 2 pamoja na watoto wake kumi!! So sad!
 
Wapumzike kwa aman hakika mungu ni mkubwa...
 
Sio kumbukumbu ya kuzama mkuu ni ya kuzamishwa kwa mv bukoba
Maana ndugu zetu walikufa kwa uzembe tu
 
Maswali magumu sana..Serikali imefanya nini kuepusha ajari za namna hii? Je imeweka kitengo cha uokozi kama ikitokea Meli ikazama ziwani jinsi ya kuokoa watu? Je Bandari za Bukoba na Kemondo zimeimalishwa kuzuia watu wasiokuwa na ticket na wazamiaji kupanda Meli?..Je MV Victoria imefanyiwa lini matengenezo makubwa ili kuokoa roho za watu zisije angamia tena?..Usafiri wa Basi toka Bukoba kuja Mwanza ila changamoto ya Kivuko inajulikana? Kuna mhindi "inasemekana" alipiga simu Mwanza kwa wenzie na kutangaza mtu atayeokoa Maisha yake atapewa Nusu ya Mali zake ndo maana Wajanja wakakikimbilia kutoboa meli ili kumuokoa ili waweze kutajirika...Je serikali iliwachukulia hatua gani hao walitoa uamuzi wa kutoboa meli na kusababisha izame kabisa!??

Wapumzike kwa Amani watu wote walitangulia mbele ya haki!!!
 
Flaviana Matata ameanzisha foundation ya kusaidia vifaa vya uokoaji melini. Huwa anajitahidi kutoa maboya na mambo kama hayo, lakini ni ka foundation kachanga na uwezo wake bado. Na yeye alipoteza mama mzazi kwenye ajali hiyo kwa hiyo anafanya in good faith.
Mwaka juzi flaviana matata alimind baada ya kuleta msaada wa maboya(life jackets)500 za msaada serikali ikayazuiwa ailipie kodi,alivyilipia sijamskia tena mwaka jana,labda mwaka huu!
 
Mungu awapumzishe kwa amani wote waliopoteza maisha kwa uzembe wa watu wachache na pia awape nguvu wote walioondokewa na ndugu zao katika ajali ile..nakumbuka nilikuwa darasa la nne wakati huo
 
Hii ni kumbukumbu nzito sana. Wakati huo 1996, nilikuwa nasoma darasa la saba Nyamagana primary school na nilikuwa nasoma darasa moja na Haji Rume, Mtoto wa captain wa meli hiyo. Alikuja mwalimu mkuu, Mr. Paskal na kwa sauti akaita...Haji, Kuja hapa Baba!!....na kumpa taarifa ya ajali. Darasa lilitahamaki kwa taarifa hizo na wakati huo kama mnajua Nyamagana primary school iko pembeni ya kilima. Wanafunzi wengi tulienda kilimani angalau kuweza kuangalia ziwani kama tunaweza iona meli hiyo kwa mbali.

Kwa muda wa week nzima maeneo ya nyamagana yalizizima na shule ilikuwa haisomeki tena....Kibaya zaidi, kulitokea report ya misiba mingi mtaani nilioishi....

Wapumzike kwa amani..
 
Hivi majuzi niliipanda MV VICTORIA, meli pekee ya abiria iliyosalia kwa safari za Mwanza - Bukoba, aisee ni majanga! Meli hiyo ikiendelea kufanya safari zake bila kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu, watanzania tujiandae kupokea msiba mkubwa kuzidi ule wa MV BUKOBA! Eee.. Mungu baba igutushe serikali na ikaikarabati meli hii, nayo ikaepusha janga la kupoteza roho za watanzania wengine wengi zaidi, kwani meli hii ni kubwa na inabeba abiria wengi zaidi ya ile MV BUKOBA!
 
Pole sana Leornado, wasichana wa Rugambwa walituhuzunisha sana pia.

acha tu kaka, mama mzazi wa yule binti alichanganyikiwa akili kabisa akawa kichaa kumpoteza first born na tena asipate hata maiti yake aizike..it was a double tragedy to that family.
 
ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu wa mamlaka husika,na mpaka leo bado hatujajifunza kwani tumeendelea kushuhudia ajali nyingi tu za majini kama ile ya mv skargit.Wapumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom